Dr Rugemeleza Nshala aliitwa polisi kwenda kuhojiwa, siyo kwa uchunguzi wa kutishiwa kwake, bali kwa yale aliyoyasema kuhusu suala la Bandari.
Sasa wala haieleweki kama alikwenda kuhojiwa, na kama alipewa masharti asiseme chochote kuhusu mahojiano hayo?
Katika hali ya kawaida, ilitegemewa vyombo vya habari vimfuate na kumuuliza maswali kuhusu alichoitiwa huko osisini kwa DCI; lakini hata waandishi wa habari na wao hawana hamu ya kupata tarifa wanayoweza kuwafikishia wananchi.
Kama wakili alipewa masharti ya kutozungumzia chochote baada ya mahojiano hayo, maana yake ni kwamba wakili huyo katishwa na kutishika, kiasi kwamba hata haki yake ya kupasha na kupata habari imeingiliwa.
Ni vigumu sana kuamini kuwa wakili msomi kama huyu anaweza kutishika kirahisi namna hiyo.
Kunyamazishwa kwake, kuna maana kwamba ameshughulikiwa na kukubali kusalimu amri katika jambo ambalo wengi waliamini kuwa katika nafasi yake, aliyoyazungumzia yalikuwa ya kweli na umuhimu mkubwa kwa jamii.
Sasa ananyamaza jamii imuelewe vipi?
Hata kama kasalimu amri, si ajitokeze na kusema kuwa hana hamu tena ya kuendelea na yale aliyokuwa ameyasema?
Kunyamaza kwake kunawafurahisha sana aliokuwa kawatupia lawama kuhusika na yanayoendelea na makubaliano hayo ya Bandari.