Sakata Mkataba wa Bandari: Wakili Mwabukusi asema asiyetaka kukosolewa aondoke kwenye ofisi za Umma

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi ameachiwa huru majira ya saa 12 jioni (Julai 14, 2023) baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa saba katika Ofisi ya makao kikuu ya Polisi mkoa wa Mbeya.

Akizungumza na Jambo Tv baada ya kumaliza mahojiano yake na Polisi, Mwabukusi amesema aliitwa na Jeshi hilo akituhumiwa kwa makosa ya kutoa lugha ya chuki dhidi ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa akidaiwa kwamba alihamasisha jamii kuwa Waziri Mkuu asiaminike kwa wananchi juu Suala la uwekezaji wa bandari kuwa una faida, hoja anazosema amezitolea maelezo polisi.

Aidha Mwabukusi amesema kuitwa na kuhojiwa kwake kwa muda mrefu wa zaidi ya saa saba kunampa nguvu pamoja na mawakili wenzake kuendelea kuwatetea walalamikaji ambao wananchi waliofungua kesi ya kupinga mkataba wa Bandari kwa madai kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

"Niwaambie tu kwamba kwa hili la kuitwa na kuhojiwa inanipa moyo sana na sikati tamaa pamoja na wenzangu, msimamo wangu uko palepale, inanipa moyo kwani naelewa kwamba kumbe Meseji Sent and Derivery (Ujumbe umeenda na umewafikia)", Wakili Mwabukusi.

"Mimi ninachotaka kuwaambia wa-Tanzania 'Hatujakosea', tuko sahihi, msimamo wetu ni uleule na tupo tayari kufika kwenye vyombo vya kisheria kwa namna yoyote kwasababu ninaamini tutapita tena na tena kwenye uvuli wa mauti lakini tutafika kwenye ukombozi kamili", Wakili Mwabukusi.

"Tuna haki za kikanuni na kikatiba, na mtu yeyote asiyetaka kukosolewa aondoke kwenye Ofisi za umma akakae nyumbani kwake hatutamfuata lakini mtu anayevunja Katiba tutamsema, kwahiyo siogopi, hata mtu akiwa Mbunge, Waziri mkuu au Rais hiyo ni dhamana hii nchi ninyetu sote sio ya watu wachache lazima nisimamie msimamo wangu lakini na kulinda raslimali za Taifa kwa mujibu wa Katiba", Wakili Boniface Mwabukusi.

Naye Wakili wa Mwabukusi kwenye shauri hilo Wakili Phillip Mwakilima amewashukuru wanasheria mbalimbali walioshirikiana katika sakata la kuhojiwa kwa mteja wake (Boniface Mwabukusi) akiwemo Rais wa TLS na Balozi Dkt. Wilbroad Slaa.

Amesema Mwabukusi ameamriwa kuripoti tena polisi mwanzoni mwa juma lijalo.

Hata hivyo Wakili Mwakilima amesema wamejiandaa kumfungulia mashtaka Juma Homera ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa madai kuwa amewadhihaki wateja wao (Waliofungua kesi ya bandari) kuwa wanawatetea wezi pia anadaiwa kushindwa kusimamia nafasi yake ya Mwneyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama badala yake amesikika akisema waliofungua kesi ya kupinga mkataba wa Bandari anawakabidhi kwa machifu wa kimila ili wawashughulikie.

"Kwahiyo niiombe mamlaka yake (Mkuu wa mkoa Mbeya Juma Homera), Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ampeleke kwingine kama si kumuondoa kabisa maana kwa hili tu (kuwakabidhi waliofungua kesi kwa machifu) hafai kuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama", Wakili Phillip Mwakilima.

Mtuhumiwa Wakili Boniface Mwabukusi aliingia polisi saa 3:58 asubuhi na mahojiano yalimalizika majira ya saa kumi na dakika kadhaa lakini Wakili Mwakilima alieleza kuwa bado Mwabukusi anaendelea kuwa mikononi mwa Polisi licha ya kumaliza mahojiano hadi baadaye majira ya saa moja kasoro baada ya taratibu nyingine kukamilika hasa za kujidhamini hadi atakaporipoti Jumatatu ijayo Julai 17, 2023.

Chanzo: Jambo Tv

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Wewe kosoa hata masaa 24 ila kuwa na heshima kwa viongozi acha kebehi na dharau kwa viongozi wa nchi. Hakuna shida kukosoa lakini ukileta dharau na kebehi unatuma message gani kwa watu kwamba wadharau mamlaka? amani ya nchi muhimu kuliko maslahi ya chama au mtu binafsi ila kuambiana tuambiane hakuna shida, chungeni lugha za maudhi na dharau.
 
Tutajie kebehi moja tu. Acha maneno
 
Wewe kosoa hata masaa 24 ila kuwa na heshima kwa viongozi acha kebehi na dharau kwa viongozi wa nchi. Hakuna shida kukosoa lakini ukileta dharau na kebehi unatuma message gani kwa watu kwamba wadharau mamlaka? amani ya nchi muhimu kuliko maslahi ya chama au mtu binafsi ila kuambiana tuambiane hakuna shida, chungeni lugha za maudhi na dharau.
Tuonyeshe dharau kwenye kauli za mwabukusi tukuunge mkono kwa hoja zako
 
Wewe kosoa hata masaa 24 ila kuwa na heshima kwa viongozi acha kebehi na dharau kwa viongozi wa nchi. Hakuna shida kukosoa lakini ukileta dharau na kebehi unatuma message gani kwa watu kwamba wadharau mamlaka? amani ya nchi muhimu kuliko maslahi ya chama au mtu binafsi ila kuambiana tuambiane hakuna shida, chungeni lugha za maudhi na dharau.
Mkuu Heijah, tenganisha kati ya "Mtu" na "Cheo". Viongozi wa Serikali ni wanachama wa CCM ambacho ni chama kinachoamini "Cheo ni dhamana".

Kwa sababu hiyo, kiongozi ("mtu") wa Serikali, akitumia vibaya cheo chake, kwa maana ya mamlaka na madaraka, siyo tu anakiuka "Imani" ya CCM pia Katiba ya JMT aliyoapa kuilinda, kuitetea, kuheishimu na kumwongoza katika maamuzi na matendo yake.

Kiongozi ni "mtu", kama watu wengine, mwenye sifa, ubora na udhaifu. Hayuko juu ya sheria
 
Wewe kosoa hata masaa 24 ila kuwa na heshima kwa viongozi acha kebehi na dharau kwa viongozi wa nchi. Hakuna shida kukosoa lakini ukileta dharau na kebehi unatuma message gani kwa watu kwamba wadharau mamlaka? amani ya nchi muhimu kuliko maslahi ya chama au mtu binafsi ila kuambiana tuambiane hakuna shida, chungeni lugha za maudhi na dharau.
Viongozi siyo Mungu!! Wasijiingize kwenye makosa makubwa kwa sababu eti ni viongozi.
 
Nyinyi mshukuru sana Mungu alimchukua JPM mapema angewarudisha kwenye mapango mlikotoka. Mama katukosea sana na huruma zake. Ingepita operation moja kabambe ndio mngeshika adabu mbwa nyie.

Hisia zako hazihitaji uwe na hasira.
Wao wakiwa mbwa sasa ww ni Nani?
Embu acha maneno ya kuudhi na kukebehi.
Sote ni Binadamu.
 
Viongozi siyo Mungu!! Wasijiingize kwenye makosa makubwa kwa sababu eti ni viongozi.
Hata Mungu kasema heshimuni mamlaka na hapa sijasema wasikosolewe hapana waambiwe lakini isiwe lugha ya kudharau mamlaka kwamba unatoka kwenye media unasema mimi siogopi mtu yoyote level yangu ma general, una maanisha nini? kila mtu akianza kudharau mamlaka itakuwa nchi hii? kosoa wala sio shida kwani lazima ufanye kiburi ndio uonekane shujaa.
 
Kakulalamikia? Au labda inakuzuia wewe kunywa mtoti wako asubuhi? Au inakupunguzia mafuta ya gari yako? Au inavunja ndoa yako, unaumia sehemu gani ndugu?
Sijaumia. Namshauri tu aende kitaaluma na aongeze uwezo wa kudhibiti hisia zake.

Awapo na hasira hatakiwi kuonyesha hasira yake kwa maneno yake. Ajifunze namna ya kutuliza hisia pale anapoongea hoja zake. Ajifunze kuondoa hisia kwenye hoja. Kama hoja ipo sawa haina sababu kuichanganya na hisia.

Hii itamsaidia yeye mwenyewe na wanaomzunguka kufanikisha malengo ya kuufuta mkataba huu haramu wa bandari.
 
Sijaumia. Namshauri tu aende kitaaluma na aongeze uwezo wa kudhibiti hisia zake.

Japanawapo.na hasira hatakiwi kuonyesha hasira yake kwa maneno yake. Ajifunze namna ya kutuliza hisia pale anapoongea hoja zake.

Hii itamsaidia yeye mwenyewe na wanaomzunguka kufanikisha malengo ya kuufuta mkataba huu haramu wa bandari.

Kama hujaumia acha mambo ya watu
 
Back
Top Bottom