Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,834
- 18,837
Wakili wa mmoja wa watu wanoshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha amejiondoa kumtetea mteja wake.
Wakili Fridoline Bwemelo amesema ameamua kujiondoa kumtetea mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyuo, Watson Mwahomange kwa kile alichodai kuwepo mgongano wa kimaslahi na kulinda maadili yake.
Bwemelo ameeleza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 7, 2022 mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi, Dk Patricia Kisinda.
Alidai kuna mambo ambayo mshitakiwa huyo alimtaka ayaeleze mahakamani lakini akaona asingeweza kufanya hivyo kutokana na maadili yake ya kitaaluma.
”Mimi kwa kiapo changu kama ofisa wa mahakama sikuwa tayari kukieleza hicho ambacho naona kitaende kinyume na maadili yangu kama wakili au ofisa wa mahakama,” amesema.
Chanzo : Mwananchi
Sabaya naye asamehewee ili tuanze mmoja, hata kama ni chungu kumeza hii, ndiyoo ili pasiwepo na double standard
Walio kuwa wanamtuma kufanya uovu yaani ma-CCM, ndiyo leo hii wanao mkimbiza na tairi na petroli, hii siyo fair kabisa!Tatizo sabaya ana kesi nyingi inabidi usubiri zote ziishe ndio utoe msamaha kwa pamoja.
Nini ni msimamo wa viongozi wa dini kuhusu Sabaya?Wakili wa mmoja wa watu wanoshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha amejiondoa kumtetea mteja wake.
Wakili Fridoline Bwemelo amesema ameamua kujiondoa kumtetea mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyuo, Watson Mwahomange kwa kile alichodai kuwepo mgongano wa kimaslahi na kulinda maadili yake.
Bwemelo ameeleza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 7, 2022 mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi, Dk Patricia Kisinda.
Alidai kuna mambo ambayo mshitakiwa huyo alimtaka ayaeleze mahakamani lakini akaona asingeweza kufanya hivyo kutokana na maadili yake ya kitaaluma.
”Mimi kwa kiapo changu kama ofisa wa mahakama sikuwa tayari kukieleza hicho ambacho naona kitaende kinyume na maadili yangu kama wakili au ofisa wa mahakama,” amesema.
Chanzo : Mwananchi
Walio kuwa wanamtuma kufanya uovu yaani ma-CCM, ndiyo leo hii wanao mkimbiza na tairi na petroli, hii siyo fair kabisa!
Nini ni msimamo wa viongozi wa dini kuhusu Sabaya?
[/QUOTE
Sidhani Kama hata Wana muda nae. Tatizo Sabaya ana damu ya kunguni.