Wakili ajitoa kesi ya Sabaya, asema analinda maadili yake

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,725
18,620
Wakili wa mmoja wa watu wanoshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha amejiondoa kumtetea mteja wake.

Wakili Fridoline Bwemelo amesema ameamua kujiondoa kumtetea mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Watson Mwahomange kwa kile alichodai kuwepo mgongano wa kimaslahi na kulinda maadili yake.

Bwemelo ameeleza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 7, 2022 mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi, Dk Patricia Kisinda.

Alidai kuna mambo ambayo mshitakiwa huyo alimtaka ayaeleze mahakamani lakini akaona asingeweza kufanya hivyo kutokana na maadili yake ya kitaaluma.

”Mimi kwa kiapo changu kama ofisa wa mahakama sikuwa tayari kukieleza hicho ambacho naona kitaende kinyume na maadili yangu kama wakili au ofisa wa mahakama,” amesema.

Chanzo : Mwananchi

====

KESI YA SABAYA: Wakili Fridoline Bwemelo aliyekuwa akimwakilisha mshtakiwa namba tatu, Watson Mwahomange, katika kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, amejiondoa kumwakilisha mshtakiwa huyo kwa kile alichodai kuwa ni kutokana kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi kati yake na mteja wake.

#AzamTVUpdates #KesiYaSabaya
 
Ilitakiwa mambo aliyoambiwa wakili na mteja wake umuulize wakili kisha uje na facts. Ndiyo utokee hapa jukwaani kuandika haya uliyoyaandika. Tofauti na hivyo tunakuchukulia kwamba wewe ni muongo tu.
 
Wakili wa mmoja wa watu wanoshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha amejiondoa kumtetea mteja wake.

Wakili Fridoline Bwemelo amesema ameamua kujiondoa kumtetea mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyuo, Watson Mwahomange kwa kile alichodai kuwepo mgongano wa kimaslahi na kulinda maadili yake.

Bwemelo ameeleza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 7, 2022 mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi, Dk Patricia Kisinda.

Alidai kuna mambo ambayo mshitakiwa huyo alimtaka ayaeleze mahakamani lakini akaona asingeweza kufanya hivyo kutokana na maadili yake ya kitaaluma.

”Mimi kwa kiapo changu kama ofisa wa mahakama sikuwa tayari kukieleza hicho ambacho naona kitaende kinyume na maadili yangu kama wakili au ofisa wa mahakama,” amesema.

Chanzo : Mwananchi

Kwa mtazamo wangu naona huyo wakili amepoteza sifa ya kuwa WAKILI. Kwasababu naamini wakili ni mtu anayesimama badala ya mtu mwingine katika kila hali, ili kuweza kumtetea. Angeweza kutumia weledi katika taaluma yake kueleza hicho alichoambiwa pasipo utata.

Kama mteja ameweza kumueleza, yeye ameshindwa vipi kueleza mahakama kwa namna isiyoleta mgongano?
Nadhani kuna wakati wakili anatakiwa kubeba dhamana ya mteja wake na ndio maana alikubali kumtetea. Au mawakili wasomi mnasemaje?
 
Sabaya naye asamehewee ili tuanze mmoja, hata kama ni chungu kumeza hii, ndiyoo ili pasiwepo na double standard
 
Wakili wa mmoja wa watu wanoshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha amejiondoa kumtetea mteja wake.

Wakili Fridoline Bwemelo amesema ameamua kujiondoa kumtetea mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyuo, Watson Mwahomange kwa kile alichodai kuwepo mgongano wa kimaslahi na kulinda maadili yake.

Bwemelo ameeleza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 7, 2022 mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi, Dk Patricia Kisinda.

Alidai kuna mambo ambayo mshitakiwa huyo alimtaka ayaeleze mahakamani lakini akaona asingeweza kufanya hivyo kutokana na maadili yake ya kitaaluma.

”Mimi kwa kiapo changu kama ofisa wa mahakama sikuwa tayari kukieleza hicho ambacho naona kitaende kinyume na maadili yangu kama wakili au ofisa wa mahakama,” amesema.

Chanzo : Mwananchi
Nini ni msimamo wa viongozi wa dini kuhusu Sabaya?
 
Sabaya alikuwa ni jambazi la kimataifa..

Nitailaani daima awamu ya tano kwa kutugawa watanzania kwa namna ambayo haijawahi kutokea.
images (1).jpeg
 
Walio kuwa wanamtuma kufanya uovu yaani ma-CCM, ndiyo leo hii wanao mkimbiza na tairi na petroli, hii siyo fair kabisa!

Kweli kabisa, wamegeuka yupo pekee yake. Alidhani watafungwa pamoja na Mh Mbowe, ili iwe draw. Sasa Mbowe kaachiwa kazi ipo kwake. Tatizo Sabaya alikuwa na kiburi Sana, anachopitia Sasa ni somo kwake.
 
Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom