Wakili ajitoa kesi ya Sabaya, asema analinda maadili yake

Huyu Sabaya wamkandike miaka 30 mingine yaishe, tumechoka habari za kesi yake ya kujitakia kwa upuuzi wake mwenyewe!
 
Ungekuwa unayajua maadili yanayosimamia taaluma ya uwakili wala usingeandika hivi
Kwa mtazamo wangu naona huyo wakili amepoteza sifa ya kuwa WAKILI. Kwasababu naamini wakili ni mtu anayesimama badala ya mtu mwingine katika kila hali, ili kuweza kumtetea. Angeweza kutumia weledi katika taaluma yake kueleza hicho alichoambiwa pasipo utata.

Kama mteja ameweza kumueleza, yeye ameshindwa vipi kueleza mahakama kwa namna isiyoleta mgongano?
Nadhani kuna wakati wakili anatakiwa kubeba dhamana ya mteja wake na ndio maana alikubali kumtetea. Au mawakili wasomi mnasemaje?
 
Sabaya naye asamehewee ili tuanze mmoja, hata kama ni chungu kumeza hii, ndiyoo ili pasiwepo na double standard
Kua mkweli na nafsi yako yaan kwa kulinganisha kesi ya mbowe (labda) na ushahidi wa sabaya ni kweli sabaya anahitajika uraiani?
 
Ilitakiwa mambo aliyoambiwa wakili na mteja wake umuulize wakili kisha uje na facts. Ndiyo utokee hapa jukwaani kuandika haya uliyoyaandika. Tofauti na hivyo tunakuchukulia kwamba wewe ni muongo tu.

Wewe ni mmbeya tu. Unajua kitu kinaitwa attorney-client priveledges?? Moja yake ni kuwa mashauriano kati yao kwa siri ni haki yao. Hata Jaji/Hakimu wa kesi husikaa hawezi kutaka kujua lakini asiyehusika anataka ajue.

Nikukumbushe kidogo, umeshawahi kusikia chamber court?? Au umeshawahi kusikia jahi akiita mawakili ofisini kwake kuteta kidogo?? Sio kila jambo ni for public consumption!!!
 
Kulinda maadili maana yake kuna vitu alikuwa analazimishwa kufanya kinyume na taratibu za kazi yake, Sabaya atubu kwa Mungu wake na amuachie yeye hatma yake, aliyoyafanya alivuka mipaka.
Aende pia kuomba msamaha kwa kila aliyemtendea ubaya na kuwalipa wote aliyowadhulumu. Atafanyika kuwa mtu mpya.AMEN
 
Kulinda maadili maana yake kuna vitu alikuwa analazimishwa kufanya kinyume na taratibu za kazi yake, Sabaya atubu kwa Mungu wake na amuachie yeye hatma yake, aliyoyafanya alivuka mipaka.

Laiti watu wengi tungejua, hii ndo suluhisho la mambo na matatizo mengi tunayopiti
 
Wakili wa mmoja wa watu wanoshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha amejiondoa kumtetea mteja wake.

Wakili Fridoline Bwemelo amesema ameamua kujiondoa kumtetea mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Watson Mwahomange kwa kile alichodai kuwepo mgongano wa kimaslahi na kulinda maadili yake.

Bwemelo ameeleza uamuzi huo leo Jumatatu Machi 7, 2022 mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi, Dk Patricia Kisinda.

Alidai kuna mambo ambayo mshitakiwa huyo alimtaka ayaeleze mahakamani lakini akaona asingeweza kufanya hivyo kutokana na maadili yake ya kitaaluma.

”Mimi kwa kiapo changu kama ofisa wa mahakama sikuwa tayari kukieleza hicho ambacho naona kitaende kinyume na maadili yangu kama wakili au ofisa wa mahakama,” amesema.

Chanzo : Mwananchi

====

KESI YA SABAYA: Wakili Fridoline Bwemelo aliyekuwa akimwakilisha mshtakiwa namba tatu, Watson Mwahomange, katika kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, amejiondoa kumwakilisha mshtakiwa huyo kwa kile alichodai kuwa ni kutokana kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi kati yake na mteja wake.

#AzamTVUpdates #KesiYaSabaya
View attachment 2142582
Ni haki yake kujitoa
 
Sabaya naye asamehewee ili tuanze mmoja, hata kama ni chungu kumeza hii, ndiyoo ili pasiwepo na double standard
Double standards kivipi wakati kila mmoja ana/alikuwa na kesi yake?
Wataka kuchangaya nazi na palachichi?
 
Sabaya naye asamehewee ili tuanze mmoja, hata kama ni chungu kumeza hii, ndiyoo ili pasiwepo na double standard
Unamsamehe vipi jambazi ambaye bado ameshikilia mali za watu? Uanze moja na nani kwani kuna jambazi mwingine amesamehewa?
 
Kwa mtazamo wangu naona huyo wakili amepoteza sifa ya kuwa WAKILI. Kwasababu naamini wakili ni mtu anayesimama badala ya mtu mwingine katika kila hali, ili kuweza kumtetea. Angeweza kutumia weledi katika taaluma yake kueleza hicho alichoambiwa pasipo utata.

Kama mteja ameweza kumueleza, yeye ameshindwa vipi kueleza mahakama kwa namna isiyoleta mgongano?
Nadhani kuna wakati wakili anatakiwa kubeba dhamana ya mteja wake na ndio maana alikubali kumtetea. Au mawakili wasomi mnasemaje?
Kumtetea bashite au Sabaya mahakamani ni kumlia bure pesa zake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom