Wakenya wavamia Tanzania

Wakenya wavamia Tanzania

Mkitafakari hili nendeni Gikomba / Kikombaa soko kuu la mitumba Nairobi..... fanyeni census ndogo tu...... zaidi ya nusu wauza mitumba ni wachagga wa Rombo.
 
Hii issue ni ya kuchukuliwa seriously. Unajua kisa cha wale banyamurenge wa rwanda wanaopigana kongo ni nini?
Ni wanyarwanda ambao waliingia kongo kutafuta maisha. Wazawa wakawakaribisha wakawapa ardhi na makazi. Sasa wanadai haki zote jama wazawa na wanapigana vita na wakongo wenyewe
We should learn from mistakes za neighbours
 
Waishi kwa amani wasijimegee ardhi kinyemela......
 
Wakuu Jambazi na Tiba mmezungumza vizuri kabisa na mie ninaunga mkono comments zenu.. Bahati mbaya hawa wote ambao wanashambulia hapa hawajawahi hata kufika hapo Kenya na kuona wanaishije hapo watanzania.. Wanabaki na stori za vijiweni na kwenye kahawa.. Tatizo hapa labda liwe kwa wageni kupata nafasi za uongozi ndani ya nchi.. Lakini hilo la kuwa na wakenya wengi hapa ati sijui wanaringa na kujisikia ni kauli zinazotia ukakasi na zinazopatikana kwenye vijiwe vya kahawa tu.. Tuache chuki za kijinga.. Watanzania wamejazana kwenye manchi ya watu kuliko unavyodhania.. Na kwa taarifa tu ni kwamba watanzania tuna bahati ya kupendwa kokote tutakapoishi kutokana na historia yetu ya nyuma huko ya kuwa wakaribu.. Afrika ya kusini huko na vurugu zote hujasikia watanzania wameshambuliwa na wako wengi tu.. Unadhani ni bahati mbaya..? Inafikia wakati mtanzania anakuja kuambiwa afunge duka kwa kuwa kuna fujo zitatokea na anaambiwa na hao wanaofanya fujo.. Unadhani ni kwanini..? Kwa sababu wanakukumbuka ukarimu tuliowafanyia huko zamani..

Sasa tumeanza kuwa na chuki na hata majirani zetu..!! Tukiwamaliza hao tutageukana wenyewe kwa wenyewe..
 
Last edited by a moderator:
Tatizo mkifika nchi ya wenzenu bado mnaendeleza chuki na kujiona vilevile, tanzania wapo wengi wanaish hum, sionyietu kuna warundi,warwanda, nani aanze kushambulia wale walikimbia ukame kwao! wakileta unyang'au wao basi itakuwa imekula kwao maana wtz tunafaham dunian jirani yetu mnafiki na1 ni mkenya
 
Mchakamchaka ChinJa mchaka mchaka Chinja "Alisema, alisema, alisema Nyerere alisema, vijana wangu wote mmelegea, sasa tuanze mchaka mchaka Chinja!"
 
watanzania wako busy na masuala ya msingi,wakenya kila siku ni kujadili negative effect.watz tuko mob hapa kenya wala hamuwez kutuua mkatumaliza na wakenya wako mob tanzania hakuna atakae waua akawamaliza,intermarriage nayo ni kubwa sana, imagine nachapa dada zenu, present wenu mzazi willy mtuva kila siku yupo bongo kuangalia family yake
 
wabongo bado wamelala... mtu anaingia nchini anapewa na uanachama wa kisiasa..!!

Ccm ni zaidi ya uijuavyo twigwa wameondoka wakiwa hai uwanja wa ndege wenye ulinzi seuse binadamu wanaoishi hukoo porini?
 
Wakenya inabidi muwe wapole, mkiwa mnakuja tz njooni na vibali maalumu sio mnakuja mnachukua ardhi za wazawa na kulisha ng'ombe zenu... msiwe mnavunga wajuaji.. watanzania hatuwezi kuwafanyia vitendo vya aina hiyo ila kuweni wapole, acheni kupiga domo wakati tunawahfadhia ndugu zenu na makampuni yenu..
 
Tatizo mkifika nchi ya wenzenu bado mnaendeleza chuki na kujiona vilevile, tanzania wapo wengi wanaish hum, sionyietu kuna warundi,warwanda, nani aanze kushambulia wale walikimbia ukame kwao! wakileta unyang'au wao basi itakuwa imekula kwao maana wtz tunafaham dunian jirani yetu mnafiki na1 ni mkenya

Mnaishi kimajungu majungu na kila mtu, mara Malawi, mara Mnyarwanda, mara Mkenya n.k. Hadi Wazanzibar wana mashaka na nyie. Mshazoea kudanganywa majirani zenu ndio sababu ya kutoendelea kwenu na mkaingia. Haya anzisheni basi tuone mtaishia wapi. Wasouth ndugu zenu wamewaanzishia njia.
 
...Suala Sio Majungu!Suala Niwao Kuishi Kihalali Kama Sisi Wanavyotubania Kwao,

Watanzania wanaoishi kenya na kufanya biashara na kazi za kilimo wanaishi kihalali? hvi huko mashuleni mlienda kujifunza ujinga?
 
Uko right sosoliso. Hakuna sababu ya kumfukuza mtu anayejitafutia maisha kihalali as long as na sisi tunanufaika na uwepo wake. Muhimu ni idara ya uhamiaji kuwatambua tu.

Mbeya tushazoeana na wakongo, wazambia, wamalawi na hutasikia kelele
 
Last edited by a moderator:
Wakenya inabidi muwe wapole, mkiwa mnakuja tz njooni na vibali maalumu sio mnakuja mnachukua ardhi za wazawa na kulisha ng'ombe zenu... msiwe mnavunga wajuaji.. watanzania hatuwezi kuwafanyia vitendo vya aina hiyo ila kuweni wapole, acheni kupiga domo wakati tunawahfadhia ndugu zenu na makampuni yenu..

Mkenya akija na kuvunja sheria, zipo vyombo vya dola zinazofaa kuwakamata na kuwashtaki, sio kuandika vichwa vya habari kama "Wakenya wavamia Tanzania". Hiyo ni kuchochea, na sijui kama mna ufahamu kwamba mkilianzisha halitapoa bila kutafuna nchi zetu hizi.
 
Uko right sosoliso. Hakuna sababu ya kumfukuza mtu anayejitafutia maisha kihalali as long as na sisi tunanufaika na uwepo wake. Muhimu ni idara ya uhamiaji kuwatambua tu.

Mbeya tushazoeana na wakongo, wazambia, wamalawi na hutasikia kelele

Umeona Mkuu Lusajo11.. Yaani hii mipaka iliyochorwa na wakoloni ndo inataka kutugombanisha.. Hii ni chuki ambayo inapandwa na baadhi ya wanasiasa uchwara na haswa ukiangalia zinaripotiwa toka angle gani..
 
Last edited by a moderator:
Dhambi ya ubaguzi hii, mbaya sana. Leo unabagua wakenya ukishamaliza kuwabagua wakenya utahamia wapi? Lazima itakuwa kabila fulan la hapa nchini na ukimaliza hilo kabila sijui utahamia wapi?!
 
Wakenya ni watu wa kutumia fursa. Kwa sasa tanzania sio tena shamba la bibi bali shamba la marehemu. Bora bibi unaweza kumuogopa kama yupo shambani lakini shamba la marehemu halina mwenye! Watoto wamelitelekeza na kuzamia mijini!

Kama fursa zipo Tanzania na Watanzania hawataki kuzichangamkia we unatengemea nchi nyingne wazione nao waziache?
 
View attachment 245320

Gazeti la Jamhuri limeripoti kuwa Wakenya zaidi ya 280 wameingia Loliondo pamoja na Serengeti na kuishi kinyume na sheria.

Baadhi yao wamediriki hata kupewa uanachama wa CCM na kupewa uongozi mbalimbali wa chama hicho. Mkuu wa Wilaya amekiri kuwepo kwa wahamiaji haramu hao.

Mpaka sasa ni 17 tu ambao wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Majina yote jamhuri wameyaweka ili kuvisaidia vyombo vya usalama kuwashughulikia.

Maoni yangu ni kuwa hili suala ni nyeti sana hasa wakenya sio majirani wazuri kama tunavyowafikiri.

Kwao hawawezi kukuruhusu hata kupata eneo la biashara kirahisirahisi, waulize Watanzania wanaoishi mipakani watawapa majibu.

Hivyo viongozi husika walichukulie serious ili jambo waache virushwarushwa. waanze kuwashughulikia kama ile operation kimbunga.

hawo magaidi hawafai kabisa kukanyaga ardhi ya Tanzania. wakamatwe wote na kuswekwa jela...wapuuzi wakubwa!
 
Tatizo mkifika nchi ya wenzenu bado mnaendeleza chuki na kujiona vilevile, tanzania wapo wengi wanaish hum, sionyietu kuna warundi,warwanda, nani aanze kushambulia wale walikimbia ukame kwao! wakileta unyang'au wao basi itakuwa imekula kwao maana wtz tunafaham dunian jirani yetu mnafiki na1 ni mkenya
Kwamba sisi wakenya ni watu wa maringo mingi ni perception tu. Siyo ukweli.
Pengine mnatuchukulia hivo kwasababu huwa hatutumii sana hizo maneno za nidhamu kama: tafadhali, naomba,samahani,nakusihi nk, kama nyinyi wabongo.
Lakini hakumanishi tuko rude.

Kweli mimi nikikupata wewe Motochini umezirai barabarani, ninaweza kataa kukusaidia? Sisi pia binadamu na tunapenda kutreat other pipo the way we would wish to be treated.
 
Back
Top Bottom