Wakenya wametupiga bao sana kwenye uwekezaji nchini

Kuna msemo wa kiswahili, huwezi kutajirika kwa jirani yako. Tusiwe na matumaini makubwa sana. UCHUMI WETU UNAKUWA NA KARIBU TUTAWAKUTA ILA TUKIWAACHIA TANZANITE, UTALII, DHAHABU NA MADINI MENGINE WATAZIDI KUSONGA MBELE.

Mkuu,

Msemo huo ndiyo msingi wa umasikini wenyewe.
Ili uwe tajiri lazima ukachukue kwa jirani.
Bila majirani utajiri wako hauwezi kuongezeka (ref. Ukoloni na mendeleo ya nchi za magharibi).
Ukoloni mamboleo ni muendelezo.
 
Kenya fursa ziko kibao hasa za usafiri wa mabasi mazuri ya daladala na mikoani bado kule vi hiace ndio daladala na vi bus vya safari ndefu ya mkoa hadi mkoa mikoa mingi tu..
Tanzania Bus investors fursa hiyo mnajua ki hiace kilivyo kidogo fikiria upande hiace toka Dar hadi Arusha utafika miguu imeganda kawekezeni kenya.Njia vinaenda vi hiace ziko kibao nendeni nairobi tu pale mtapata information zote kwa nacho yenu Hamuhitaji kuajiri expert
 
Wkaenyawanavipaji vingisana kuliko TZ
Sisi tumeweka Siasa za maji taka mbele.
Watanzania ni wajuwaji sana ,lakini kielimu tupo chini mno.
Hata hivyi ,hizo biashara zinazosifiwa ni za Wakenya mnajuwa ni wakenya wa jamii ganiwaliowekeza zaidi?
Mii nadhani Wahindi na pengine Wasomali,
sisi Waswahili tunasubiri Vibarua tuu.
Mitaji yetu midogo , Business management zetu ni Poor.
Mswahili kabakia mtu wa Kutumwa tuu na Kulipwaga mishahara.
Ongeza na Wakikuyu😃
 
Wakenya wana uchumi mkubwa zaidi yetu, pia wana wataalamu wa viwango zaidi yetu sababu elimu yao ni bora, na sio hapa kwetu tu, hao jamaa wametapakaa mpaka SA huko wana exposure ya biashara na wanaongoza mashirika na kampuni, kutaka sisi tuwe kama wao itachukua muda kidogo, nionavyo bora tujifunze toka kwao ili baadae na sisi tuendeshe mambo yetu.
Watz wangekuwa wanafikiria hivi,wangekuwa mbali sana,ata sisi wakenya tulijifunza kutoka kwa Wahindi na wasomali
 
Wakuu

Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.

Tanzania sisi sasa tuna kampuni 30 tu. Je, tumekwama wapi kama Nchi?

Nini kifanyike? Waalimu, Wahudumu katika hoteli nyingi ni Wakenya. Wapi wizara zetu na wale watoa maamuzi wanaweka mkakati wa pamoja juu ya hili?
Na hizo kampuni 30 si ajabu ukakuta 28 ni za watanzania wenye asili bara la asia.. sie tumekalia maneno tu hakuna tunachofanya productive

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Wenye mabasi kavamieni soko la kenya .Nairobi nk bado wanatumia vipanya kama daladala pia safari za mikoa mibus ya hovyo na vipanya vinaenda mkoa hadi mkoa maeneo kibao .Mabasi mazuri machache hasa ya kutoka Nairobi kwenda mikoa mingine ya kenya.Mazuri ni ya Mombasa Nairobi tu

Abood bus sevice ,Sauli nk kaavamieni soko la ndani kenya
Matatuu inajulikana worldwide
Imekuwa kivutio cha watalii

Bora sisi tungeacha chai maharage tu

Ova
 
Wakuu

Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.

Tanzania sisi sasa tuna kampuni 30 tu. Je, tumekwama wapi kama Nchi?

Nini kifanyike? Waalimu, Wahudumu katika hoteli nyingi ni Wakenya. Wapi wizara zetu na wale watoa maamuzi wanaweka mkakati wa pamoja juu ya hili?
sijakuelewa mkuu, sisi tuna kampuni 30 kenya au?
 
Matatuu inajulikana worldwide
Imekuwa kivutio cha watalii

Bora sisi tungeacha chai maharage tu

Ova
kivutio cha watalii malofa billy gate na mabilionea waweza panda chai maharage? na wanakuja mara moja moja tu mtu una suti utapanda chai maharage? kenya public transport bado haiko vizuri kabisa chama cha wamiliki wa daladala vamieni soko la kenya la ndani liko wazi mno nchi nzima.Vi hiace ndio eti usafiri wao
 
Wakuu

Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.

Tanzania sisi sasa tuna kampuni 30 tu. Je, tumekwama wapi kama Nchi?

Nini kifanyike? Waalimu, Wahudumu katika hoteli nyingi ni Wakenya. Wapi wizara zetu na wale watoa maamuzi wanaweka mkakati wa pamoja juu ya hili?
KENYA YUKO TU MBELE YA PAZIA UJUE KUWA NYUMA YA PAZIA HIZO ZOTE NI KAMPUNI ZA U.S.A NA U.K ZILIWEKEZA MITAJI KENYA WAKATI ZIKISUBILIA UJAMAA UANGUKE TANZANIA ULIPOANGUKA NDIO ZIKAVUKA MPAKA. FAIDA KWA WAKENYA NI KUWA ZILIWAPATIA UJUZI WA KUSIMAMIA MAKAMPUNI SASA BAADA YA KUJA TANZANIA HAZIONI SABABU YA KUIGIA TENA GHARAMA KUTOA UJUZI KWA WATANZANIA BALI WALETE WAKENYA WAKASIMAMIE KAMPUNI ZAO NA HAPA SERIKALI YA TANZANIA NDIPO INATAKIWA KUWA MACHO KWELI KWELI
 
Kenya ni Taifa kubwa la Uchumi Afrika Mashariki na Afrika.

Pili mnapokuwa na Rais dizaini ya Nyerere na Magufuli wanaotaka kufukarisha watu wao na kuwafanya tegemezi kwa serikali huwezi pata raia wabunifu,wathubutu na aggressive kwenye biashara .

Mwisho lugha ya biashara ni English ila hao wawili hapo juu wanashadidia kiswahili
 
Wakenya wana uchumi mkubwa zaidi yetu, pia wana wataalamu wa viwango zaidi yetu sababu elimu yao ni bora, na sio hapa kwetu tu, hao jamaa wametapakaa mpaka SA huko wana exposure ya biashara na wanaongoza mashirika na kampuni, kutaka sisi tuwe kama wao itachukua muda kidogo, nionavyo bora tujifunze toka kwao ili baadae na sisi tuendeshe mambo yetu.
Kama Taifa tufike mahala tuwe na sera za Uchumi na siasa ya uchumi inayoeleweka sio huyu anataka serikali ndio iwe kiongozi mwingine anataka private sector sasa hatuelewekagi tunataka nini hii nchi
 
Wakenya mambo ya viwanda walianza muda mrefu sana pia taratibu za kujali vya kwao ipo kwenye damu.

Wao waliwahi fursa huku kupitia lugha ya kiingereza ndio maana wengi walifanikiwa hata kama hajasomea lakini lugha inapanda aliheshimiwa.

Pia wabinafsi sana utawekeza Kenya lakini mkenya alifanya hiyo biashara lazima waende kwa mkenya kwanza. Mtizamo wangu
Kwa nini mnang'ang'ania kiswahili na centralization kama unajua haya?
 
Kuna msemo wa kiswahili, huwezi kutajirika kwa jirani yako. Tusiwe na matumaini makubwa sana. UCHUMI WETU UNAKUWA NA KARIBU TUTAWAKUTA ILA TUKIWAACHIA TANZANITE, UTALII, DHAHABU NA MADINI MENGINE WATAZIDI KUSONGA MBELE.
Unachekesha mkuu,miaka 5 iliyopita gap Kati ya Kenya na Tzn imeongezeka hiyo kuwakuta watakuwa wanakusubiria wewe?
 
Kwenye uchumi mkubwa zaidi yetu ni kweli japo tunaweza kuwapiku tuki maintain speed ya ukuaji wa uchumi ndani ya miaka mitano ijayo.

Lakini si kweli kuwa wana wataalam bora na elimu bora zaidi yetu, labda lugha ya kiingereza chenye lafudhi ya kikenya.

Jambo la msingi ni kuwa support watu wetu wanaojaribu ili wakue na kushindana na Makampuni ya nje. Hii iwe Sera rasmi kabisa.

Hilo tu.
Unachekesha,kuanzia leo jua kwamba gap imeongezeka hizo ndoto za kuwakuta sahau,Ghana walikuwa nyuma yetu leo vipi?

Pili kusaport private sector unajua ni kufanyaje? Ni pamoja na kuondoa vikwazo vya biashara na kuwa na kodi rafiki.

Nchi hii haieleweki siasa yake kwenye swala la uchumi na tuna viongozi ambao hawawezi kusupoort biashara.mfano wakati kuna mzozo wa biashara Kati ya Kenya na Tzn ,,wanasiasa uchwara kila mtu alikuja na tamko na kujitutumua ikaishia kutupa hasara
 
kenya wamewekeza vitu vidogo dogo kama maduka ya madawa na bar nkTanzania kampuni chache lakini za nguvu
Wewe huwa ni empty fuvu ,kama ni tuvitu tudogo hiyo value ya biashara inazungumza nini? Gawanya kwa idadi afu utapata jibu
 
Tanzania ilikuwa ina Uchumi mkubwa kuliko Kenya, kabla ya USSR kuanguka.

Vita ya Kagera ndio iliangusha uchumi wetu, lakini kuanzia miaka ya 2000 uchumi wetu umekuwa sana, na hadi sasa wametupita kidogo sana.

Elimu ya Tanzania ni bora mara 100 ya Elimu ya Kenya, hili nina hakika nalo sana sana.

Shida ya Tanzania, ni Simba aliyelala, Watanzania ni watu wa sawa tu, hawataki kuipenda nchi yao ya kuipigania.

Kenya huwezi kukuta duka la mkikuyu linauzwa na Mjaluo au asiyemkikuyu, hadi bank watu wanahudumiana kilugha, hii ni moja ya sababu ya hayo maendelo ya Kenya.
 
Issue me naiona resource zipo kwetu nyingi ndio maana wapo wengi kwetu..utaenda kenya ukafanye nini..
 
Back
Top Bottom