Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,339
- 17,583
Ni ajabu sana kukuta mwanaume akimwomba mwanaume mwenzake ampe mimba mkewe ili amzalishe huku akiwa na uwezo wa kumpa mimba. Hicho ni kituko ambacho hata wanyama hawafanyi.
Chukulia mfano Simba, anapokuta jike lina watoto wa mwingine, kitu cha kwanza ni kuwauwa watoto wa dume jingine kabla ya kuanzisha familia yake.
Ni jambo rahisi sana kulielewa lakini cha kushangaza kuna jamii ya watu wanashindwa kabisa kuelewa hii kanuni ya asili.
Kwa miaka mingi majirani zetu wamekuwa wakiulea muziki wa "ragga" badala ya "kuvumbua" muziki wa kwao. Katika miaka ya tisini wakati sisi tunalea muziki wetu wa "bongo fava" wao walikuwa wana cheza ragga, wakiwaiga wa Jamaika kuimba kiingereza chao kibovu cha ragga.
Leo hii mimba tuliyoitungisha sasa ni mtoto mkubwa aliyefuzu kiwango cha shahada ya uzamili. Sasa wenzetu wanakuja kumshangilia mwanetu tuliyemlea na kumsomesha kwa udi na uvumba.
Wakenya ni lini mtazaa wa kwenu?
Wengi mnafikiri hamna waimbaji wazuri, la hasha... bali hamna muziki wenu kutoka Kenya. Jifunzeni kwetu wabongo kutengeneza kwanza muziki (genre) halafu ndiyo mtengeneze waimbaji mashuhuri kama kina Diamond na Ali Kiba.
Ni hayo tuu.