Wakristo wenzangu mnakwama wapi?

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Ukristo ni dini na ni tamaduni ambayo inaongozwa kwa misingi ya biblia. Lakini cha ajabu kuna mambo ambayo tunafanya yanaacha midomo wazi.

Juzi kati hpa naangalia "Hawavumi Lakini Wamo" kipindi cha wasanii na waimbaji ITV kuna mdada mmoja mlokole fulani hivi anaimba wimbo wa "Yesu Atarudi" cha ajabu melody na instrument ni ya wimbo wa Harmonize "Atarudi" sasa nabaki kujiuliza tangu lini magharibi na mashariki zikakutana.


Mbaya zaidi yaani hta aina ya muziki wa madhehebu ya kikristo( isipokuwa) katoriki yaani kila kitu ni muziki wa dunia hadi kuchecha yaani makanisani hamna tofautu na disko. Tunakwama wapi?

Siku hizi madhabahu yanatumika kama majukwaa ya siasa. Yaani kana nimejosewa na fulani siku nikipata nafasi kusimama atanikoma. Nitasema udhaifu wake ili tu nimkomoe. Tunakwama wapi?

Siku hizi kila nchungaji anakuja na falsafa zake kuhusu mahusiano. Yaani kila mchungaji ni mtaalamu wa ndoa. Anaongea ili apate attention YouTube na kwenye mitandao mingine ya kijamii. Tunakwama wapi?Viongozi wa serikali wakikosea mnabaki kuwaangalia tu na kuwapigia makofi badala ya kukemea. Tunakwama wapi?


NI HAYO TU.
 
Ukiona huelewi ujue haya kuhusu, fanya yale unayoyaelewa, ya wakristo waachie wakristo wenyewe.
 
Siku za mwisho watu watajitafutia walimu makundimakundi ili wawafundishe wafundisho yadanganyayo/ya kuwafariji.Tena wataona kwamba kuna amani lakini kumbe amani haipo,ni amani ya shetani.
LAKIN Yakobo ametoa ole kwa wa walimu maana wao adhabu yao ni kubwa zaidi ikiwa watadanganya kondoo wa Bwana.

Siku hizi msingi wa bible ushapotea na kila mtu anafanya yake ya kumfurahisha.Ndipo siku ya hukumu kutakuwa na kilio na kusaga meno maana watu walifarijiwa ba uongo wa ibiris wakaona wako salama kwa Yesu kumbe sivyo.wao ni vuvuvugu na kanisa la mwisho ambalo ni la laodikia limepewa onyo kaa sababu ya uvuguvugu hivyo likitapwikwa ndipo watu watalia sana maana wataona bora wangekuwa wazinzi,wezi,waongo,ili wajifurahishe duniani lakin duniani wamejibana,na mbinguni hawaendi kwa hiyo wanaungana na makahaba ziwa la moto
 
Back
Top Bottom