Wakenya ni lini mtazaa wakwenu?

Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
8,305
17,415
Ni ajabu sana kukuta mwanaume akimwomba mwanaume mwenzake ampe mimba mkewe ili amzalishe huku akiwa na uwezo wa kumpa mimba. Hicho ni kituko ambacho hata wanyama hawafanyi.

Chukulia mfano Simba, anapokuta jike lina watoto wa mwingine, kitu cha kwanza ni kuwauwa watoto wa dume jingine kabla ya kuanzisha familia yake.

Ni jambo rahisi sana kulielewa lakini cha kushangaza kuna jamii ya watu wanashindwa kabisa kuelewa hii kanuni ya asili.

Kwa miaka mingi majirani zetu wamekuwa wakiulea muziki wa "ragga" badala ya "kuvumbua" muziki wa kwao. Katika miaka ya tisini wakati sisi tunalea muziki wetu wa "bongo fava" wao walikuwa wana cheza ragga, wakiwaiga wa Jamaika kuimba kiingereza chao kibovu cha ragga.

Leo hii mimba tuliyoitungisha sasa ni mtoto mkubwa aliyefuzu kiwango cha shahada ya uzamili. Sasa wenzetu wanakuja kumshangilia mwanetu tuliyemlea na kumsomesha kwa udi na uvumba.

Wakenya ni lini mtazaa wa kwenu?

Wengi mnafikiri hamna waimbaji wazuri, la hasha... bali hamna muziki wenu kutoka Kenya. Jifunzeni kwetu wabongo kutengeneza kwanza muziki (genre) halafu ndiyo mtengeneze waimbaji mashuhuri kama kina Diamond na Ali Kiba.

Ni hayo tuu.
 
Kwa miaka mingi majirani zetu wamekuwa wakiulea muziki wa "ragga" badala ya "kuvumbua" muziki wa kwao. Katika miaka ya tisini wakati sisi tunalea muziki wetu wa "bongo fava" wao walikuwa wana cheza ragga, wanawaigiza wa Jamaika kuimba kiingereza chao kibovu.

Leo hii mimba tuliyoitungisha sasa ni mtoto mkubwa aliyefuzu kiwango cha shahada ya uzamili. Sasa wenzetu wanakuja kumshangilia mwanetu tuliyemlea na kumsomesha kwa udi na uvumba.

Wakenya ni lini mtazaa wakwenu?

Wengi mnafikiri hamna waimbaji wazuri, la hasha... bali hamna muziki wenu kutoka Kenya. Jifunzeni kwetu wabongo kutengeneza kwanza muziki (genre) halafu ndiyo mtengeneze wakina Diamond na Ali Kiba.

Ni hayo tuu.
Nyuzi kama hizi zinatambulika kama za kikhanithi na muandikaji zezeta. Nyambaaaafu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakenya nacho wapendea east africa kizuri huwa ni chao na watakwambia kipo kwao.wameweza mlima kilimanjaro watashindwa vingine
 
Mi nadhani kinachowaponza Wakenya kwenye muziki ni lugha!!

Lugha kwa maana ya kuendekeza kwao Kiingereza huku wakijifanya kukidharau Kiswahili!!

Unfortunately, Wakenya sio native English Speakers ingawaje wangependa wafahamike hivyo!

Matokeo yake, kwenye Kiingereza hawapo, kwenye Kiswahili hawapo! There's no way Mkenya anaweza kuki-master Kiingereza kama anavyoki-master native English speaker kiasi cha kuweza kucheza na maneno atakavyo!!

Ukitaka kufanya muziki vizuri, ni lazima uwe na uwezo wa kucheza na maneno ya lugha husika!

Bongo Flavor Artists kwa mfano... kuna maneno mengine hadi unaweza kujiuliza hili neo au haya maneno wameyatoa wapi!! Na hiyo ndiyo raha ya kutumia lugha ambayo you can command it jinsi utakavyo, na ndio maana wanaweza kucheza na maneno kadri wapendavyo na hivyo kutengeneza ladha fulani kwenye mashairi!

Bora basi wangekuwa na "Kiingereza chao wenyewe" na wakaki-master vizuri kama wa-Nigeria! Kinyume chake, there's no way a Kenyan artist can deliver the same English song flavor as Beyonce does!

Mbaya zaidi, hawana pia uwezo wa ku-deliver the same Swahili song flavor kama ambavyo anaweza kufanya mtu kama Beka Flavor!!!

Yaani Wapwa zetu wapo wapo tu!!!
 
Mziki wa Kenya ni moja kati ya miziki bora sana. Napenda wanavyoimba kiswa-nglish na lugha za kitaa kwao mfn. Matatu- dala dala, githeri- kande

Wasanii nguli wa hizo nyimbo kutoka Kenya ni Nyashiski, sauti soul na nameless

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Hivi bado kuna nyimbo za Kibongo maana kila nikiskliza mnachoita Bongo flavor huwa mumeiga kila kitu cha Kinijeria, tofauti tu ni kwamba mnaimba kwa Kiswahili, lakini mengine yote kama vile midundo, sauti n.k. vyote ni Nigeria.

Muziki huwa unabadilika bana, hata hao akina TID muziki wao haufanani na ule waka akina "2 proud" (Mheshimiwa) diplomatz, n.k.
 
Mziki wa Kenya ni moja kati ya miziki bora sana. Napenda wanavyoimba kiswa-nglish na lugha za kitaa kwao mfn. Matatu- dala dala, githeri- kande

Wasanii nguli wa hizo nyimbo kutoka Kenya ni Nyashiski, sauti soul na nameless

Sent from my SM-J530F using Tapatalk

Hayo ni mapenzi yako binasfi lakini takwimu hazioneshi hivyo.
 
Sasa huyu ndio atoe melody kama ya Chris brown kweli?

Wakenya wabakie kwenye kuandika tu English

Education inakua edukeshon badala ya edjukeish'n

Awa nashon ndio our nation 😂😂😂😂
 
Ni ajabu sana kukuta mwanaume akimwomba mwanaume mwenzake ampe mimba mkewe ili amzalishe huku akiwa na uwezo wa kumpa mimba. Hicho ni kituko ambacho hata wanyama hawafanyi.

Chukulia mfano Simba, anapokuta jike lina watoto wa mwingine, kitu cha kwanza ni kuwauwa watoto wa dume jingine kabla ya kuanzisha familia yake.

Ni jambo rahisi sana kulielewa lakini cha kushangaza kuna jamii ya watu wanashindwa kabisa kuelewa hii kanuni ya asili.

Kwa miaka mingi majirani zetu wamekuwa wakiulea muziki wa "ragga" badala ya "kuvumbua" muziki wa kwao. Katika miaka ya tisini wakati sisi tunalea muziki wetu wa "bongo fava" wao walikuwa wana cheza ragga, wakiwaiga wa Jamaika kuimba kiingereza chao kibovu cha ragga.

Leo hii mimba tuliyoitungisha sasa ni mtoto mkubwa aliyefuzu kiwango cha shahada ya uzamili. Sasa wenzetu wanakuja kumshangilia mwanetu tuliyemlea na kumsomesha kwa udi na uvumba.

Wakenya ni lini mtazaa wa kwenu?

Wengi mnafikiri hamna waimbaji wazuri, la hasha... bali hamna muziki wenu kutoka Kenya. Jifunzeni kwetu wabongo kutengeneza kwanza muziki (genre) halafu ndiyo mtengeneze waimbaji mashuhuri kama kina Diamond na Ali Kiba.

Ni hayo tuu.
For ze fasti taimu nimekubaliana nawe.

Ila Kenya bado Kuna mziki mzuri. Labda uwe mvivu au mnafiki ndio utasema hujauskia.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom