wakuu hali iko hivi,
1. NYUMBA 12 zenye utata ziko plot no 2747 block x, along great north road, wanaofahamu mbeya ni maeneo ya nane nane mkoani mbeya
2. mwaka 1987, wizara ya ujenzi iliomba survey ya kiwanja hicho kifanyike, na survey ilifanyika na kuwa approved by director of survey tarehe 29/4/87, kwa jina la zonal garage and hotel, for the ministry of works. reference survey plan no E14/472/37.
3. mwaka 1990 contractor aliyepewa kujenga barabara ya igurusi-kwenda songwe alipewa eneo hilo akajenga nyumba za ma-ex patriates wake, ikiwa ni wale wa kampuni ya renadert na partzank put
4.contrator alipomaliza kazi alirudisha nyumba hizo kwa mwenyewe yaani wizara ya ujenzi, compound ina nyumba 12, ambazo wizara iliwagawia ao ili allocate kwa wafanyakazi wake
5, mpaka hapo kiwanja hicho hakikuwa na hati kwa kuwa serikali huwa haina au haikuwa na utaratibu wa kuwa na hati miliki za viwanja vyake
6. sera ya serikali ya kuuza nyumba zake ilipotangazwa nao hawa wakaomba kuuziwa na wakaukabaliwa, wako 12 na kwa sasa wanakaa na familia zao
7. mwaka 1998, inaonekana mama ana mkapa aliomba apatiwe mahali pa kujenga hiyo inayoitwa shule huko mbeya, na kwa kificho, huyu bwana anayeitwa j.d.zongo, ambaye ana kashfa nyingi sana za uuuzaji maeneo wazi, huko dsm hasa sinza alilietwa hapa mbeya kama afsa ardhi. ni wakati huo huo aliandaa mpango wa siri wakampa mama mkapa hiyo offer na yeye akachemka huko bongo hadi akapata hati miliki.
8. wakati huo anapewa hati, tayari hawa wafanyakazi walishauziwa nyumba na kwa taratibu walitakiwa wakishamaliza kulipa, kufanyike sub-division from hati kubwa ili kila mmoja apewe hati yake. sasa walipoenda huko mbeya city council ndipo wakakikuta hiki kitimtim, kuwa mmiliki ni huyu mama fisadi.
9. wenzetu hawa wakarudi kwa mmiliki yaani wizara kupitia tanzania building agency, wizara na tanzania building agency wakapatwaa na mshangao kuwa kuna mtu anamiliki eneo lao, tena liliko ndani ya eneo lingine la serikali ambalo kuna karakana maarufu ya mbeya roadworkshop, karakana ambayo wizara ilipata msaada toka norway
mpaka sasa wanarushwa danadana, na ndoyo maana wanaomba msaada wenu wana jf
useful contact
manager
tanzania buildng agency
phone 025-2502755
mbeya