Wakazi wa mji wa Njombe wanatarajia kupata huduma ya majisafi, salama na ya kutosheleza kwa asilimia 100, kufuatia Mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa

Wakazi wa mji wa Njombe wanatarajia kupata huduma ya majisafi, salama na ya kutosheleza kwa asilimia 100, kufuatia Mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa

KIJICHO PEVU

Member
Joined
May 4, 2024
Posts
69
Reaction score
49
Wakazi wa mji wa Njombe wanatarajia kupata huduma ya majisafi, salama na ya kutosheleza kwa asilimia 100, kufuatia Mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya Dola za Marekani 15.7.

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amefanya ziara ya kukagua mradi huo ambao ni moja wapo ya miradi ya maji ya miji 28 ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua ya utekelezaji iliyofikiwa.

Akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, Mhe. Aweso amewahakikishia wananchi wa Njombe kuwa changamoto zote za upatikanaji wa maji ziko mbioni kuwa historia baada ya kukamilika kwa mradi huo.

Katika hatua ya kuongeza kasi ya utekelezaji, Waziri Aweso amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka, mamlaka ya kuchukua hatua kwa wakandarasi watakaoshindwa kutimiza wajibu wao kwa kuchelewesha mradi huo muhimu kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mtaka, ameipongeza Wizara ya Maji kwa ufuatiliaji wa karibu wa mradi huo ambao amesema ni tumaini jipya kwa wakazi wa Njombe.

Ameahidi kuwa mkoa utaendelea kulinda, kutunza na kuendeleza vyanzo vya maji kwa kupanda miti rafiki wa maji ili kuhakikisha miradi inakuwa endelevu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma Waziri amesema Serikali imejizatiti kuhakikisha ubora wa miradi yote ya maji unafikiwa kupitia usimamizi makini na wa karibu.

Pia amesisitiza kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya "kumtua mama ndoo ya maji kichwani" inazidi kutekelezwa kwa vitendo.

Mradi huo unatarajiwa kubadilisha maisha ya maelfu ya wakazi wa Njombe kwa kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa kila kaya.
 

Attachments

  • 29c404ab9eb044b2891d9f710a653d8f.jpg
    29c404ab9eb044b2891d9f710a653d8f.jpg
    126.3 KB · Views: 20
  • 1c0ab9f6bde541558616f406213d8ee1.jpg
    1c0ab9f6bde541558616f406213d8ee1.jpg
    115.2 KB · Views: 19
  • a8c3d9036b8347448831950ab54827e6.jpg
    a8c3d9036b8347448831950ab54827e6.jpg
    134.5 KB · Views: 21
  • 20250723_151802.jpg
    20250723_151802.jpg
    537.2 KB · Views: 17
  • e785bd64b27c4c98b98ded8939a1c9ae.jpg
    e785bd64b27c4c98b98ded8939a1c9ae.jpg
    156.1 KB · Views: 17
Back
Top Bottom