Wakati tunajiandaa na Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020: Tanzania yaongoza Afrika usambazaji umeme Vijijini

Huu mradi ulianziishwa kisheria mwaka 2005 na kufadhiriwa na benki ya dunia wale mnaopiga mapambio ya awamu hii ndio imefanya hivyo acheni kupotosha....
 
Wakati Lisu anabwatuka hayo anachomeka simu yake kwenye umeme uliowekwa na selikali!

Ametembea kwa gari mikoa zaidi ya 10 sababu mikoa hiyo ina lami kila kona,

Huyu tutamchinja kwenye box la kura

Safari hii lazima hawa wanasiasa wa aina ya Lissu wapate somo na fundisho kuu litakalo kuwa shamba darasa kwa kizazi hiki na kijacho cha Taifa hili la Tanzania. Baada ya uchaguzi huu na kuhakikishia, No one in this nation will think that a fool is honourable or say that a scoundrel is honest.
 
Kwa Maoni yangu Kisiasa Duniani kote Mgombea hashindi kwa sababu ameleta Maendeleo;; Ndio maana Ccm imekuwa inashinda huko nyuma; sio kwa sababu ya Maendeleo bali ikikuwa inatafuta kura
MTU anayejitambua. Hata ungenunua kivuko au meli: Lakini ukagusa uhuru na utu wake ; "umempoteza " !!
 
Kwa iyo kama mnaweka umeme vijijini ndo mpige watu risasi??? Mbambikizie watu kesi??? Mteke watu na kuwaua?????

Mbona hilo la umeme vijijini alilianzisha Kikwete na yeye ndo aliweka hadi kwenye bajeti kodi kidogo ya mafuta iende REA ili kufanikisha haya mnayojisifia leo?????

Mbona kikwete hakupiga watu risasi??? Hakuminya uhuru wa watu???? Hakuteka watu na kubambikizia watu kesi????

Kwani Makaburu hawakuweka umeme vijijini South Africa??? Mbona waliondolewa????? Unajua South Africa hadi mwaka 1990 Mandela anatoka gerezani ilikuwa wapi kimaendeleo?????

Acha kabisa hizo, usileteleze kuchimbuliwa kwa makaburi hapa. Hata Yesu alifufua wafu na hakutaka kuchimbua mifupa iliyo makaburini. Na kwasababu hiyo ilipomlazimu aliamua kuingia na kukaa kaburini siku tatu.
 
Kwa iyo kama mnaweka umeme vijijini ndo mpige watu risasi??? Mbambikizie watu kesi??? Mteke watu na kuwaua?????

Mbona hilo la umeme vijijini alilianzisha Kikwete na yeye ndo aliweka hadi kwenye bajeti kodi kidogo ya mafuta iende REA ili kufanikisha haya mnayojisifia leo?????

Mbona kikwete hakupiga watu risasi??? Hakuminya uhuru wa watu???? Hakuteka watu na kubambikizia watu kesi????

Kwani Makaburu hawakuweka umeme vijijini South Africa??? Mbona waliondolewa????? Unajua South Africa hadi mwaka 1990 Mandela anatoka gerezani ilikuwa wapi kimaendeleo?????
Uliwahi kuona mandela anabwatuka kuponda miundombinu iliyowekwa na makaburu? Kwamba haifai haina maana?

Yeye alikuwa anadai uhuru wa kiutawala kwa watu wazawa wa SA!
SA leo kuna vyama vingi kama ilivyo hapa kwetu wanafanya shughuli zao ili washike ikulu, na harakati zao si za ukombozi kama zile za enzi za Mandela!

Hapa kwetu unaponda miundombinu ambayo wewe mwenyewe unaitumia kila siku eti haina maana kwa taifa.
Ndio maana tunahitimisha kwamba Lisu na chadema ni mbumbumbu badala ya kunadi nini utafanya kwa taifa zaidi ya haya yaliyofanywa na ccm kwa miaka 60 nyie mnakuja mnaponda tu kwamba hizo ndege, barabara, umeme nk havina maana yeyote kwa watanzania.

Namna hii hata hapo chadema kuna watu wana akili kama kina Baregu unaona wamekaa kimya wanaona aibu kujichanganya na siasa za kihuni namna hiyo
 
Jamani umeme vijijini unawekwa na REA,REA unapata fedha kupitia kwa wateja wa Tanesco,ukinunua umeme wa matumizi yako unakatwa fedha za REA. Ni sawa na uchaguzi wa Kura za maoni zikizofanywa na ccm ,wale wagombea walichangishwa fedha za kuendesha uchaguzi na fedha Zoho hizo zilitumika kuwagawia wajumbe posho na vyakula na vinywaji,means CCM haikutoa hata sent tano kuendesha uchaguzi. Sasa ukiona mgombea ameteuliwa tarehe 22.8 ameteuliwa kutoka a na Niko iliyochezwa na wagombea wenzake na sio mtaji wa CCM.pua REA ni nguvu za wananchi. Someni muelewe

Tatizo lililotekea tanzania na ambalo watanzania hawakulizoea ni vitisho. Wafanyabiashara wafugaji,wakulima,watumishi,wasio na ajira nawateule wote wanatishwa kila kukicha.Hawajui kesho Nini kitatokea. Sasa imefika pahali watu hawataki Tena vitu wanataka UTu,upendo,na amani na wajue hatima ya maisha yao kesho.Watanzania wengi Sasa wanaishi maisha Kama ya digidigi porini.
Vitu vinaleta RAHA na si FURAHA. Vitu bila FURAHA ni bure tu kwani mtu anakosa AMANI ya moyo. Mfano, ukimfungia mtu katika nyumba nzuri na ukampa kila kitu cha raha (luxurious things) lakini umsiruhusu kutoka na kutembea mahali pengine, kuongea na watu na kuongea anachopenda pasipo kuvunja sheria nk, hawezi kuwa na furaha. Watu wanataka uhuru na maendeleo ya vitu ili wawe na RAHA na FURAHA pamoja. Mfano mkubwa ni jinsi Libya ilivyo kuwa wakati wa Gadaffi.
 
Uliwahi kuona mandela anabwatuka kuponda miundombinu iliyowekwa na makaburu? Kwamba haifai haina maana?

Yeye alikuwa anadai uhuru wa kiutawala kwa watu wazawa wa SA!
SA leo kuna vyama vingi kama ilivyo hapa kwetu wanafanya shughuli zao ili washike ikulu, na harakati zao si za ukombozi kama zile za enzi za Mandela!

Hapa kwetu unaponda miundombinu ambayo wewe mwenyewe unaitumia kila siku eti haina maana kwa taifa.
Ndio maana tunahitimisha kwamba Lisu na chadema ni mbumbumbu badala ya kunadi nini utafanya kwa taifa zaidi ya haya yaliyofanywa na ccm kwa miaka 60 nyie mnakuja mnaponda tu kwamba hizo ndege, barabara, umeme nk havina maana yeyote kwa watanzania.

Namna hii hata hapo chadema kuna watu wana akili kama kina Baregu unaona wamekaa kimya wanaona aibu kujichanganya na siasa za kihuni namna hiyo
Samahani una elimu gani???? Unajua historia ya ukombozi wa Africa Kusini???? Na umeelewa vizuri point yangu????? CCM kweli mmeishiwa vijana
 
Ndugu zangu,

Tutambue kuwa wapinzani wasiofunzwa na Magufuli watafunzwa na watanzania kwenye sanduku la kura.

Wakati wapinzani wakianza kampeni kabla ya wakati kwa kisingizio kuwa hakuna sheria wala kanuni inayokataza huku wakitukana na kubeza serikali ya awamu ya tano kuwa haijafanya kitu, sasa rasmi Tanzania yaongoza Afrika katika usambazaji wa umeme vijijini.

Sote tunatambua umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi

Hongera JPM
Hongera serikali
Hongera CCM

#2020 kura kwa John
Cabo Verde 93%
Comoros 81%
Gabon 93%
Ghana 82.3%
Mauritius 98%
Seychelles 100%
South Africa 91.2%
 
Cabo Verde 93%
Comoros 81%
Gabon 93%
Ghana 82.3%
Mauritius 98%
Seychelles 100%
South Africa 91.2%
Sijajua unalenga nini ndugu yangu. Anyway, taarifa hapa ni kuwa tunaongoza kwa usambazaji wa umeme vijijini, sijui Kama hilo unalikataa
 
Ndugu zangu,

Tutambue kuwa wapinzani wasiofunzwa na Magufuli watafunzwa na watanzania kwenye sanduku la kura.

Wakati wapinzani wakianza kampeni kabla ya wakati kwa kisingizio kuwa hakuna sheria wala kanuni inayokataza huku wakitukana na kubeza serikali ya awamu ya tano kuwa haijafanya kitu, sasa rasmi Tanzania yaongoza Afrika katika usambazaji wa umeme vijijini.

Sote tunatambua umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi

Hongera JPM
Hongera serikali
Hongera CCM

#2020 kura kwa John
Kusema serikali haijafanya kitu kumbe ndo hayo matusi hua mnasema mnatukanwa? Hahahahahah
 
Back
Top Bottom