Wakati Rais Kagame akitoka ziarani Tanzania, Rais Kenyatta nae atua Rwanda!

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,066
2,000
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amewasili Rwanda kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Rwanda Dkt. Richard Sezibera mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali.
Screenshot_20190311-182600.png

Mara baada ya kupokelewa Rais Kenyatta alijkwenda katika chuo cha mafunzo ya Kijeshi cha Gabiro, wilayani Gastibo ambako alikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Kagame pamoja na maafisa wa serikali kuu wa ngazi za juu na sekta binafsi na mashirika binafsi wanakutana Gabiro Ijumaa kwa ajili ya mkutano wa kitaifa wa viongozi (Umwiherero).

Akiwa nchini humo, Kenyatta anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais Paul Kagame.

Kenya ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inaongozwa na Rais Kagame.

Nchi mbili hizo zinamahusiano ya karibu katika Nyanja mbalimbali zikiwemo biashara, usalama, kujenga uwezo na uwekezaji miongoni mwa mengine.

Kwa mara ya mwisho, Rais Kenyatta aliwasili Rwanda mapema mwaka jana wakati wa mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika.

https://zanzibarleo.co.tz/2019/03/11/kenyatta-ziarani-rwanda/
 
Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
8,291
2,000
M7 na Kagame waache egoism, yaani kutumia matukio kuji propagate kwa misifa na kujiona wao ni kila kitu.

kitu kingine wanachukulia nchi zao kuwa personal properties.
Wote waliingia madarakani kwa mitutu na wamekuwa "wakishinda" chaguzi zote.
Both have overstayed their usefulness.
 
Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,167
2,000
Yaani Rwanda na Burundi shida.Uganda na Rwanda shida .Sudan kusini shida.Jumuiya ya Afrika mashariki imebaki Tanzania na Kenya ndio hawana shida na nchi nyingine

Kenya kuna shida kidogo, Uhuru na Ruto William Samoi hawaivi tena.. Raila is on spotlight..!! Alafu grand corruption inamsakama VP Ruto vibaya, sasa ni kuchafuana tu sbb urais unakaribia..!! Ha haaaa imebaki Tz tu ndio kuko shwari, na kama sio CCM imara ingekuwa shidaaa sanaaa
 
wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,784

Uimara wa CCM ni nguvu za dola na si vingjnevyo, badilini katiba pawepo na tume huru ya uchaguzi ndo utakuja hapa kuiongelea CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
6,438
2,000
Kenya kuna shida kidogo, Uhuru na Ruto William Samoi hawaivi tena.. Raila is on spotlight..!! Alafu grand corruption inamsakama VP Ruto vibaya, sasa ni kuchafuana tu sbb urais unakaribia..!! Ha haaaa imebaki Tz tu ndio kuko shwari, na kama sio CCM imara ingekuwa shidaaa sanaaa
Watu wanajadili migogoro baina ya nchi na nchi ww unaleta mambo ya Ruto? Unaakili kweli?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom