Wakati Rais Kagame akitoka ziarani Tanzania, Rais Kenyatta nae atua Rwanda!

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amewasili Rwanda kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Rwanda Dkt. Richard Sezibera mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali.
Screenshot_20190311-182600.png

Mara baada ya kupokelewa Rais Kenyatta alijkwenda katika chuo cha mafunzo ya Kijeshi cha Gabiro, wilayani Gastibo ambako alikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Kagame pamoja na maafisa wa serikali kuu wa ngazi za juu na sekta binafsi na mashirika binafsi wanakutana Gabiro Ijumaa kwa ajili ya mkutano wa kitaifa wa viongozi (Umwiherero).

Akiwa nchini humo, Kenyatta anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais Paul Kagame.

Kenya ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inaongozwa na Rais Kagame.

Nchi mbili hizo zinamahusiano ya karibu katika Nyanja mbalimbali zikiwemo biashara, usalama, kujenga uwezo na uwekezaji miongoni mwa mengine.

Kwa mara ya mwisho, Rais Kenyatta aliwasili Rwanda mapema mwaka jana wakati wa mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika.

https://zanzibarleo.co.tz/2019/03/11/kenyatta-ziarani-rwanda/
 
M7 na Kagame waache egoism, yaani kutumia matukio kuji propagate kwa misifa na kujiona wao ni kila kitu.

kitu kingine wanachukulia nchi zao kuwa personal properties.
Wote waliingia madarakani kwa mitutu na wamekuwa "wakishinda" chaguzi zote.
Both have overstayed their usefulness.
 
Yaani Rwanda na Burundi shida.Uganda na Rwanda shida .Sudan kusini shida.Jumuiya ya Afrika mashariki imebaki Tanzania na Kenya ndio hawana shida na nchi nyingine

Kenya kuna shida kidogo, Uhuru na Ruto William Samoi hawaivi tena.. Raila is on spotlight..!! Alafu grand corruption inamsakama VP Ruto vibaya, sasa ni kuchafuana tu sbb urais unakaribia..!! Ha haaaa imebaki Tz tu ndio kuko shwari, na kama sio CCM imara ingekuwa shidaaa sanaaa
 
Watu wanajadili migogoro baina ya nchi na nchi ww unaleta mambo ya Ruto? Unaakili kweli?
 
M7 na Kagame waache egoism, yaani kutumia matukio kuji propagate kwa misifa na kujiona wao ni kila kitu.

kitu kingine wanachukulia nchi zao kuwa personal properties.
Wote waliingia madarakani kwa mitutu na wamekuwa "wakishinda" chaguzi zote.
Both have overstayed their usefulness.

Wakati hawa wawili nikikubaliana nawe uliyoyasema juu yao, ningekwenda mbele zaidi na kusema kwamba Uhuru Kenyatta nisingemchukulia kiwepesiwepesi katika mahusiano. Ndumila kuwili siku zote sio wazuri katika mahusiano yoyote.

Pili, na hata kama Kagame angekuwa rafiki yetu, sina shaka angetamani sana Kenya iwe ilipo Tanzania kwenye ramani. Nadhani hali hiyo ingetuliza roho yake vizuri sana; na nadhani ingekuwa hivyo Nkurunziza angekwishalizwa siku nyingi.

Kuna watu ambao ni 'snitches', hawa marafiki wawili ni 'snitches per excellence' katika eneo hili. Ukizubaa tu, unalizwa!
 
Kenya kuna shida kidogo, Uhuru na Ruto William Samoi hawaivi tena.. Raila is on spotlight..!! Alafu grand corruption inamsakama VP Ruto vibaya, sasa ni kuchafuana tu sbb urais unakaribia..!! Ha haaaa imebaki Tz tu ndio kuko shwari, na kama sio CCM imara ingekuwa shidaaa sanaaa
Inavyoonekana Kenyatta na Laila walikubaliana kukabiadhiana madaraka na wakati Rutto anajiona yeye ndiye mtu sahihi wa kumrithi kinyatta
 
Back
Top Bottom