Kenyatta: Serikali chapeni kazi msilaumu utawala uliopita

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Rais Mstaafu wa kenya Uhuru Kenyatta, ameiambia serikali iliyoko madarakani iache kuulaumu utawala wake kwa kushindwa kutimiza malengo iliyowaahidi Wakenya. Uhuru amesema serikali ya rais William Ruto inapaswa kushughulikia matatizo yanayowakabili Wakenya badala ya kutafuta sababu zisizo na msingi.

Matamshi ya Kenyatta yanajiri huku serikali ya Rais Ruto ikishindwa kudhibiti hali ya uchumi wa taifa ambayo imesababisha gharama ya maisha kupanda miaka miwili baada ya kupewa ridhaa na wakenya kuongoza taifa hilo lenye uchumi mkubwa Afrika ya Mashariki na Kati.

Rais Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua wamehusisha utawala wa Uhuru na gharama kubwa ya maisha ya sasa.

Alisema kila mara mtu anaposhindwa kufanya anachopaswa kufanya, wanalaumu serikali iliyopita. "Huu mwenendo hata kama mke amekataa kujifungua, tutalaumiwa sisi, lakini tumezoea hili,"

Mapema mwezi huu, Waziri wa Fedha Profesa Njuguna Ndung'u aliilaumu serikali iliyopita kuwa chanzo cha gharama kubwa ya maisha kwa madai ya kile alichokiita, makosa ya kiuchumi yaliyofanywa na serikali ya Rais aliyestaafu Uhuru Kenyatta.

Kama haitoshi, Wiki iliyopita, Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen nae pia aliilaumu serikali iliyopita kwamba ndiyo iliyohusika na ujenzi wa paa la kuvuja katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Alipokuwa akifanya kampeini Ruto aliahidi kupunguza gharama ya maisha, suala ambalo laelekea kumpiga chenga sasa.

DW Swahili
 
Huyu angekuwa anawasikia CHADEMA sijui angesema nini. 'Waache kukimbizana na kaburi?'

Kazi kweli kweli.
 
Serikali ya ruto kama ya the late. Utafikiri hawakuwepo kwenye serikali iliyopita
 
Back
Top Bottom