Rwanda ni Israel ya Afrika Mashariki?

NUMBER 10

Member
Aug 4, 2021
86
125
"Rwanda imekuwa kivyake, hivyo hatuogopi na hatutishwi." Hii ni kauli ya Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakati wa sherehe za kuupokela mwaka mpya wa 2024 uliofanyika mjini Kigali Rwanda .

Kagame anaongeza kwa kusema "Hatutishwi na uwezekano kwamba siku moja tutakuwa peke yetu tena. Tunapaswa kuwa tayari kila wakati.

Kuna wakati tutabaki peke yetu, lakini tutastahamili na kuishi vizuri tena zaidi ya nyakati zilizopita" Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Wachambuzi wa siasa za Afrika Mashariki mnasemaje kuhusu kauli hizi za Mkuu wa nchi.

 

Attachments

  • Screenshot_20240112_181002_Instagram.jpg
    Screenshot_20240112_181002_Instagram.jpg
    36.5 KB · Views: 8
Mkwara Kwa Burundi..... Ajaribu kumzingua kizimkazi aone shoooo yake.
Unafikiri ni vita dhidi ya Burundi!!?

Burundi na Bongo so tayari walishaungana !? So ndio maana ya kale kamsemo "hamieni Burundi"!!?yaani Burundi no sehem ya tz au hujui!!?

Burundi,Congo ni watoto wa Tz yaani kama Rwanda atapigana na Jao atakua anapigana na tz indirect way!!shtuka mkuu!!!

Ukimuona mrundi anatunisha misuli ujue anajivunia kaka yake !!

Ngoja tuone!!
 
Mbona PK anatoa ushauri mzuri tu kwa Raia wake?!
Mi sijasikia chochote kibaya hapo
 
Leo kajileta kwenye sherehe za mapinduzi akisindikizana na kaka yake M7,mimi mguu wake huu naona kama nikuja kuomba poo kwa namna fulani,maana kaona yupo kisiwani sasa
Yaani Kagame aombe nchi ya kijinga na wajinga kama hii! wewe unamsikia huyo jamaa yule ni mnyarwanda mmarekani akili kubwa sana yule jamaa.

Yule ni kachero muwakilishi wa Marekani ukanda huu! unadhani ameongea hayo maneno hajui anchoongea? .

Yule hana akili kama za marais wenu hawa wakina Kisekedi na Ndayishimiye wakupenda machawa! Kagame anataka no iwe no na yes iwe yes yaani mkono wa chuma hana mda wa kubembelezana.
 
Tuache wivu
Sio wivu, PK anawafunza watu wake ubinafsi. Katika hali ya kawaida Kirwanda hakiwezi kuishi peke yake na kuanzisha bifu na majirani zake muda baada ya muda.

PK akitaka asitake ni muhimu kuwa na mahusiano mazuri na jirani zake. Aidha, anapaswa kutengeneza mkakati utakaowanufaisha wanyarwanda kisaikolojia na kujitegemea pia, sio kuwajenga kujiona wao peke yao wanaweza kuhimili matokeo ya dunia wakiwa peke yao. Akiwajenga katika namna anavyoendelea wanyarwanda watajitukuza mbele ya mataifa mengine jirani na hatimae kutengeneza uwadui wa kudumu mioyoni mwao dhidi ya majirani zao.

.........Israel imezunguukwa na majirani zake ambao imewageuza kuwa maadui na mahasimu wakubwa wa maisha yao yote.
 
Back
Top Bottom