Wakati mwingine ni bora hata kutojua maamuzi ya ovyo yanayofanywa na watanzania wenzetu wenye dhamana ya kutuongoza. Inauma sana

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
253
629
Naandika kwa uchungu sana. Saa nyingine naona hata bora ningekuwa mhadzabe nisijue chochote kinachoendelea kufanywa na wenye mamlaka. Huu ufisadi unaovuja au kusikia kupitia CAG ni sehemu tu ya ufisadi mkubwa uliowahi kufanywa na unaofanywa na baadhi ya watanzania wenzetu wenye dhamana ya kutuongoza. Ukiona hadi Rais anawasihi wateule wake wale kwa urefu wa kamba zao ujue sio poa.

Karibu kila awamu ina matukio yake ya kuumiza watanzania. Yaani kila awamu lazima kuwe na makosa makubwa ya kugharimu watanzania wote. Mimi sikuwepo wakati wa awamu ya kwanza ila najua hadi 2009 kuna watu walikuwa wakilipwa fidia ya mabilioni kwa kudhulumiwa mali zao na serikali ya wakati huo. Awamu ya kwanza ilifanya maamuzi mengi yaliyomdidimiza zaidi mwananchi kiuchumi badala ya kumnyanyua. Kupigania uhuru kisha kuwasababishia umaskini wa kutisha watanzania haiingii akilini. Hadi leo nchi inalipa gharama ya maamuzi mabaya ya awamu ya kwanza.

Awamu ya pili nayo ndo kama awamu iliyofungua milango ya matukio ya upogaji wa kufuru. Uuzwaji wa Loliondo na mikataba ya ovyo kwenye umeme ilianzia kwenye awamu hii ya pili. Awamu ya tatu na ya nne ina matukio mengi ya kuumiza ambayo yatatugharimu milele. Awamu ya tano ilikuwa kama asali kwenye ncha ya kisu.. yaani utamu unausikia huku pia maumivu unayasikia. Hii awamu ilibomoa sana umoja wa kitaifa na kutuachia urithi wa Sukuma Gang.

Awamu ya sita chini ya Mama Samia Suluhu Hassan bado mpya na haina rekodi ya jambo lolote baya ingawa ripoti ya CAG inaonyesha upigaji upo. Swali ni je awamu hii itaweza kwisha ikiwa na unafuu kuliko zilizopita? Je, hii DP World itaichafua milele awamu ya sita au itaacha alama nzuri isiyofutika ndani ya mioyo ya watanzania? Kwa upande wangu naona DP World inaweza kuleta neema kwa watanzania endapo mkataba utazingatia maslahi ya pande zote ila pia unaweza kuwa mkataba mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu tupate uhuru. Uamuzi uko mikononi mwa wenye mamlaka ya kuamua kwa niaba yetu.
 
Awamu ya sita chini ya Mama Samia Suluhu Hassan bado mpya na haina rekodi ya jambo lolote baya ingawa ripoti ya CAG inaonyesha upigaji upo.
Taahira hili!.
jose-mourinho.jpg
 
Awamu ya sita tunaambiwa ndege zilizonunuliwa kwenye awamu ya tano zinatia hasara, lakini bado awamu ya sita wananunua ndege
 
Back
Top Bottom