Wizi, ufisadi na ubadhirifu ni maamuzi na matakwa ya nchi yetu. Watanzania msiumize vichwa vyenu

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,235
16,671
Wakuu,

Kila mwaka CAG anatoa ripoti zake na kuonyesha mambo yale yale na kilio kile kile.

Naomba mtambue kwamba wizi, ufisadi na ubadhirifu ni maamuzi ya nchi yetu hayo yawepo na kushamiri na vyombo vyote vya usalama vina bariki hayo kutokea ndiyo maana hayaishi!

Dola na baraza la usalama wa taifa na nchi kwa ujumla vingetokomeza haya kama tu visingeridhia haya kutokea kwa kuwa vipo na haya yapo basi wanayalinda ili yaendelee kutokea miaka hadi miaka!

Kama vyombo vya ulinzi na usalama vingeyachukia haya na kuamua ku deal nayo yasingetokea. Yanatokea kwa sababu dola imeamua kulinda watendaji wanayoyafanya hayo ndio maana hayaishi.

Tunapiga kelele weeee lakini kama yana baraka kutokea yatatokea tu hata tufanyaje.

Siku deep state ikiamua huu ujinga usiwepo hautokuwepo lakini kwa kuwa inaona na haifanyii kazi kutokomeza basi yataendelea kuwepo!

Nawashauri watanzania wenzangu tuelekeze akili, mawazo na nguvu zetu kwenye mambo mengine coz haya yana baraka ndio maana kila mwaka yapo!

Siku dola ikiamua yaishe hutoyasikia tena yapo kwasababu yamepangwa yawepo kama yalivyo!!

Haiwezekani awamu karibu zote yanaripotiwa mambo yale yale halafu hayafanyiwi kazi na yanaendelea kila mwaka!maana yake ni kuwa yana baraka za dola kutokea!

Mlale unono!
 
Dola manake ni chombo kinachoundwa na watu ambao anaweza kuwa wewe, mimi au yule, shida yetu kama Taifa na Afrika kwa ujumla ni UBINFSI. yani upo tayari kula fedha za kununulia madawa hospitali bila shida yeyote.
 
Kila mtu akiwajibika kwenye nafasi yake hilo linawezekana pia...!
Labda katika nchi ya kufikirika hilo lawezekana, la, kusingekuwa na Sheria na Mahakama. Kinachokosekana ni usimamizi thabiti wa sheria, kanuni na taratibu mithili ya mila na tamaduni zetu.
 
Hili linajulikana maana hata JK alisema kwa kejeli eti hajui kwanini sisi ni masikini.

Wanajua fika kuwa wataendelea na huu mchezo hata kama mtalalanika maisha Maadam hamfi kwa njaa basi wataendelea kufanya yao
Wizi, rushwa, uongo na utapeli ndio maamuzi yetu.
 
Labda katika nchi ya kufikirika hilo lawezekana, la, kusingekuwa na Sheria na Mahakama. Kinachokosekana ni usimamizi thabiti wa sheria, kanuni na taratibu mithili ya mila na tamaduni zetu.
Ndio maana nikasema kila mtu akiwajibika kwenye nafasi yake hilo linawezekana mkuu...!
 
Ni kwa vijana hasa middle class to take charge, ni vema hawa middle class wakarudi on the ground na kutambua kuwa corruption, nepotism, ufisadi na majanga kwa taifa na wakitambua hili waongoze vita dhidi ya mambo hayo, kulalama humu kwenye soft landing hakutaisaidia Tanzania yetu, ndio maana hizi royal families zitasumbua sana nchi yetu maana middle class wapo kwenye mijadala ya simba/yanga na mada pendwa ngono
 
Wakuu,

Kila mwaka CAG anatoa ripoti zake na kuonyesha mambo yale yale na kilio kile kile.

Naomba mtambue kwamba wizi, ufisadi na ubadhirifu ni maamuzi ya nchi yetu hayo yawepo na kushamiri na vyombo vyote vya usalama vina bariki hayo kutokea ndiyo maana hayaishi!

Dola na baraza la usalama wa taifa na nchi kwa ujumla vingetokomeza haya kama tu visingeridhia haya kutokea kwa kuwa vipo na haya yapo basi wanayalinda ili yaendelee kutokea miaka hadi miaka!

Kama vyombo vya ulinzi na usalama vingeyachukia haya na kuamua ku deal nayo yasingetokea. Yanatokea kwa sababu dola imeamua kulinda watendaji wanayoyafanya hayo ndio maana hayaishi.

Tunapiga kelele weeee lakini kama yana baraka kutokea yatatokea tu hata tufanyaje.

Siku deep state ikiamua huu ujinga usiwepo hautokuwepo lakini kwa kuwa inaona na haifanyii kazi kutokomeza basi yataendelea kuwepo!

Nawashauri watanzania wenzangu tuelekeze akili, mawazo na nguvu zetu kwenye mambo mengine coz haya yana baraka ndio maana kila mwaka yapo!

Siku dola ikiamua yaishe hutoyasikia tena yapo kwasababu yamepangwa yawepo kama yalivyo!!

Haiwezekani awamu karibu zote yanaripotiwa mambo yale yale halafu hayafanyiwi kazi na yanaendelea kila mwaka!maana yake ni kuwa yana baraka za dola kutokea!

Mlale unono!
Hao ni makada wa UVCCM unadhani watafanya nini?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom