Ni kwanini maamuzi mengi ya Viongozi (Serikali) yanapingwa sana na wananchi walio wengi?

Heart Wood.

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
886
930
Ni kweli kuwa huwezi hufanya jambo la kuwafurahisha watu wote. Na si kila mtu atapendezwa na mambo uyafanyayo hata kama ni mazuri kiasi gani, Ila basi angalau mambo yaliyo mengi ufanyayo yapendezwe na walio wengi.!

Mie nachukulia JF kama case study. Ukiachana na watu wachache sana ambao wao walishajitanabaisha kama watu wa kusifia kila kitu, ila watu wengi sana hapa JF nimekuwa nikifuatilia michango yao huwa inaonekana kupingana sana na maamuzi mengi ya Serikali. Nimewahi pia kuwa member wa platform iliyoanzishwa hivi karibuni ijulikanayo kama ' clubhouse', nako nikakuta watu walio wengi sana wanapingana na maamuzi mengi au mambo mengi yanayofanywa na viongozi wetu.

Sasa huwa najiuliza, hivi hawa viongozi wao hupata wapi maarifa ya kufanya maamuzi ambayo yanakinzana kwa kiasi kikubwa na wananchi walio wengi? Fuatilia tu hata viweni, watu wengi huwa hawaridhishwi na matenda ya Serikali.

Mie nimewahi kuwa kiongozi tangu chekechea, shule ya msingi, sekondari, chuo kikuu na hata kazini. Kote huko nilikopita, kwa kiasi kikubwa watu walionekana kuungana nami ktk mambo yaliyo mengi isipokuwa watu wachache sana ambao huwa hawakosekani ktk jamii yoyote. Ila kwa asilimia karibia 90 wamekuwa wakikubalina nami. Sasa najiuliza, hawa viongozi wetu mbona wao mambo yao yanapingwa na walio wengi? Wao huongoza kwa maslahi ya watu wa aina ipi sasa?.

Suala kama rushwa na matumizi mabaya ya pesa za umma, hivi ni kweli Serikali pamoja na maarifa ya wataalamu wengi ilionao imeshindwa kabisa kuja na mkakati wa kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi? Ukinipa mimi hii kazi ya kuandaa mkakati madhubuti wa kupambana na rushwa na matumizi ya ovyo naweza kukuandalia na nikakukabidhi. Sasa kama mie mtu wakawaida nina mawazo haya, iweje hao wasomi wa huko maofsini wenye maarifa tele washindwe kila mwaka iwe kilio tu?

Hebu tazama maamuzi kama mswada wa marekebisho ya sheria ya watu wa Usalama wa Taifa, imepingwa sana na walio wengi humu. Uamuzi kama ule wa kujenga complex Ikulu ya Chamwino watu walihoji sana kuwa je hicho ni kipaumbele?. Tazama suala la mchakato wa katiba mpya linavyopelekwa, watu wengi wanahoji kama kweli serikali ina nia ya dhati.

Tazama namna fedha za TASAF zinavyogawiwa, watu wengi hawaridhiki na utaratibu huo. Suala la matumizi mengi ya anasa ya fedha za umma. Jinsi Serikali inavyoshughulikia nidhamu ya watumishi wa umma na suala la taarifa za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa pesa za umma, watu wengi hawaridhishwi na ukimya wa kutochukua maamuzi.

Watumishi wengi wanapiga soga tu huko maofsini na hawatoi huduma bora kwa wananchi. Malalamiko kila mahala. Hili nalo lisubiri mpaka vyama vya upinzani vishike madaraka? Mbona kukabiliana na nidhamu ya watumishi wa umma tena watu wachache tu katika nchi ni suala rahisi tu? Nini kinashindikana sasa? Mfano watu hujifanya miungu watu huko maofsini, kuna ugumu gani wa kudhibiti hali hii? Mpaka Yesu arudi tena ndio tuweze? Ajabu kabisa..

Mtazame Waziri kama Bashe akiwa Mbunge wakati hajawa Waziri, alionekana kama mtu mwerevu mwenye maono ya kuipaisha nchi yetu katika viwango vya juu sana. Ila kwa sasa ni waziri sijui wa Kilimo. Je, ni kweli kakifanya kilimo kuwa shughuli yenye tija kwa mkulima kama alivyokuwa na maono akiwa Mbunge? Nimemtaja huyu ila wapo wengi tu. Ukifuatilia viongozi wengi ni wasomi waliojipatia maarifa ndani na nje ya nchi, sasa mbona hawatumii hayo maarifa kuwasaidia ipasavyo hasa raia maskini huko vijijini na mijini?

Kuna mwenye kujua kwanini viongozi wetu hawafikii matarajio ya wananchi walio wengi?. Narudia tena, case study yangu ya haya niliyoyasema ni kupitia michango ya watu hapa JF na Clubhouse.
 
Chadomo ndio Wananchi walio wengi? Kwa mfano maamuzi yapi?
 
Wanaamua bila kushirikisha wananchi.

Maamuzi yaliyotokana na wananchi kamwe hayapingwi na wananchi.
 
Back
Top Bottom