Je, taasisi nyeti za serikali zina uwezo wa kumudu mabadiliko yoyote ya uongozi yanayofanywa na wananchi?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
304
276
Wanabodi,

Kiongozi siku zote hawezi kutekeleza majukumu yake au ilani yake bila kushirikiana na taasisi mbalimbali serikalini. Hii ina maanisha kwamba mbunge yeyote lazima ashirikiane na madiwani waliopo jimboni mwake, pamoja na viongozi wengine ambao wapo chini yake ili kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Kathalika, Rais yeyote atakuwa kama gogo endapo mawaziri wake pamoja na viongozi mbalimbali hawa tekelezi wajibu wao ipasavyo. Ninaposema kwamba Rais Samia ameupiga mwingi, basi nitakuwa nime wapongeza wasaidizi wake wa karibu, mawaziri wote, na wawakilishi wa taasisi zote ambazo kwa namna moja au nyingine zimehusika katika mafanikio haya.

Kama unaamini kwamba viongozi bora huzaliwa na uwezo wa kuongoza basi tafasiri yako itakuwa inamhusisha mtu ambaye anaweza kutekeleza majukumu yake bila kusaidiwa sana na walio chini yake. Sambamba na hilo, kiongozi aliye tengenezwa huwa mfano mzuri kwa walio mzunguka na mara nyingi huonekana mwema hata kwasababu ya mema yaliyofanywa na wafuasi wake. Kama CEO wa Tanzania, Rais Samia anahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa watu wengi wanao jumuisha kampuni ya Tanzania.

Katika kuvuta shuka usiku wa manane na kupinduka kidogo, utashtushwa kwa kumwagiwa maji ya baridi baada ya kupata ndoto mbaya sana kuhusu Tanzania ya vizazi vijavyo. Kama rubani wa ndege aliyekosa rubani msaidizi, mifumo ya uongozi serikalini haiko imara kupokea mabadiliko yoyote yanayoweza kufanywa na watanzania kwenye sanduku la kura. Mifumo iliyo imara siku zote huwezesha chombo ambacho hutumika kwenye uongozi kufanya kazi bila kuegemea chama chochote cha siasa. Hii ina maanisha kwamba Ikulu kama taasisi, idara ya usalama wa taifa, polisi, uhamiaji, mamlaka ya mapato na taasisi zingine nyeti zinatakiwa zijiendeshe na ziweze kushirikiana na uongozi wa awamu yoyote serikalini.

Ili tufahamu kama taasisi zetu zitakuwa imara hata kwa muda wa miaka 30 ijayo, ni muhimu kufahamu ushawishi wa chama tawala kwenye uendeshaji wa nchi. Kwanza kabisa, vyama vya siasa hujiandaa kwa kila chaguzi kwa kuwa na ilani inayo orodhesha miradi inayopanga kutekeleza kwa awamu husika. Kama ilani hizi huandaliwa kwa malengo ya vyama vya siasa husika basi utekelezaji wa ilani hizi huingiliana na dira ya nchi. Nina amini kwamba serikali inatakiwa iwe na mipango binafsi inayo endana na bajeti yake kwa kila awamu ya uongozi. Kama ilani ni ya chama, utekelezaji wa ilani hii utahitaji matumizi ya rasilimali za serikali na utafanikiwa zaidi kama taasisi hizi nyeti zina egemea upande wa chama husika.

Tunapo tazama siasa zetu, ni vyema kama mwananchi yeyote ambaye amedhamiria kuwa tumikia wananchi wenzake apate nafasi hii bila ubaguzi wowote na kwa njia za staha. Kama kuna udanganyifu wowote unao sababishwa na taasisi yoyote, basi mfumo husika hauko imara na hauwezi kupokea mabadiliko yoyote yanayofanywa na wananchi.

Tukubaliane, hitilafu yoyote inayoweza kusababishwa na maamuzi mabovu kutoka kwa wananchi au sababu nyingine yoyote ni rahisi zaidi kurekebishwa kama mifumo ipo tayari kumpokea mwana siasa yeyote. vile vile, mifumo hii kuegemea upande wowote huashiria ubaguzi kwa watanzania wenye mtazamo tofauti na ni hasi kwa usalama wa Tanzania
 
Back
Top Bottom