wakaka kama vile hamna mioyo ya kuumia

wakaka kama vile hamna mioyo ya kuumia

Nimeuliza vizuri tu unanijibu Kunya..

yawezekana sijaona ama nimesahau.
Kuna ubaya gani kunijibu bila kuniuliza maswali ya kwanini nzi anapenda choo...

Dearest....hasira ya nini leo?? calm down,please!
 
Utoto na ulimbukeni unakusumbua,ukikua utaacha!!
 
kama unafanya kazi serikalini au kwenye halmashauri hata haitakiwi uisome hii sredi
spendi wanaume wavivu wa kufikiri
Na nakwambia hivi , hata huyo unayemtaka hutompata , wanaume watakuwa wanakosha rungu hapo kwako mpk uje ustuke umeshazeeka zeeeeee!!!!!!Kwishneyyyyyyyyyyyyyyyy!!!!!!!
 
ipi tena dear!
nina Mmasai namwelewa na ananielewa sana
ila wakaka wakiona upo mkinya wanaanza kujisumbua kukujaribu

wakajaribu kwenye level zao kwangu nawaonea huruma wanavyoumiaga

Kama unawaonea huruma si unawaambia ukweli tu..

Kwamba unae unaempenda, na wao wachape lapa...
 
You will never walk alone.
Afrodanzi aliingia kichwakichwa kwenye mvutano wetu hajui tulipotokea,

Na wewe uwe na lugha laini kwa wadada utajaikimbia JF shauri yako
 
ulishindwa kutumia ustaarabu mwingine ili nijue kuwa hunitaki???
niliumia nipo serious ila kumbe MUNGU alikuwa ananiepushia balaa
Mungu ametunusuru wote, wewe huoni hiki kigezo cha M mbili per month ungesababisha nigeuzwe kontena la kubeba cocain kupeleka china? na usisahau kule wananyonga tu.
 
home arusha, mama mchagga baba mngoni


jaman wakaka hamuumiagi na hamjifunzi?

think of wewe ni mdada mkali/mzuri na umejiremba, hamna hamna umetupia viwalo vyako hata kama vya mtumba ila umechagua sana na umevitafuta masoko yote ya mitumba.

....anatokea mkaka kunako wapi sijui hata kama ofisi mmoja mnafanyia na anaanza kukurushia mitego yake.Ukimcheki huyo mkaka hana cheo, hana hela hata za urithi kwao, elimu labda mko sawa (first degree) au umemzidi yaan una professional bodies qualifications mfano CPA, ACCA.

Au mkaka mwingine unakutana naye shopping anajifanya kukuelewa sana mara ooh hiki na kile mwishowe anaomba namba ya simu , kama kawaida mie huwajibu akitaka kuniona ajage palepale aliponionea siku hiyo.

...huwa nacheka na kujiuliza huwa hawaumii hawa kaka zetu wanapokataliwa????
kwa nini wasiende kubahatisha kwenye level zao/matawi yao wanajileta kwa vinavyoelea???

Note: MKAKA KAMA HUNA SHULE, MJASIRIAMALI WA UKWELI, HUNA HELA usijisumbe hutapendwa hata uwe handsome kivipi.Ukihurumiwa kama ni handsome unapewa uroda mara moja kisha ujiondokee

Kukataliwa ni sehemu ya mchakato wa kutongoza. Na mara nyingi huwa tunakwenda tukijua kuwa uwezekano wa kukataliwa upo hivyo ikitokea haitupi shida sana. Pia tunajua kuwa mara nyingi nyie kina dada ni waelewa ukimkatalia mtu akaendelea kubembeleza huwa mnaishia kukubali.
 
hapana mdogo wangu, nikutakie kila la kheri inshallah upate zaidi ya 2mil, iwe 5mil.
hapana akiwa tajiri atanisumbua ndio maana milioni mbili namkubali, simaanishi eti lije jitu ni jitu la mihela nalikubali, namaanisha just to meet the minimum requirement of 2 kwa mwezi he will be ranked on the same level as anayepata hata milioni 10
 
Hivi degree moja inaweza kukufanya ujione so exceptional zamani bt not nowdays coz watanzania wengi tuu wanazo

Pili jua wapo wengi tu wenye hzo degree wameolewa/kuoa wasiokua nazo na wana maisha superb cha msingi ni kuangalia high q ya mtu kupambana na umaskini and how far amekuvutia cz at the end of the day kila mtu anataka aishi maisha mazuri n satisfied kwa kila angle
 
Marytina mie nimewagonga wenzako wenye jeuri kama ww, pamoja na umaskini wangu.

Sema wewe unakutana na washamba; ukukutana na maborn kama sisi lazima ukae
 
Last edited by a moderator:
hakunaga mapenzi jamaa kupendana ni zama za kale.
Mungu kaniumba kila nguo kunikubali so wakaka jiangalieni sio kila mmoja anajiletaleta tu bila kujicheki cv yake

Debe tupu haliachi kutika.
 
Na nakwambia hivi , hata huyo unayemtaka hutompata , wanaume watakuwa wanakosha rungu hapo kwako mpk uje ustuke umeshazeeka zeeeeee!!!!!!Kwishneyyyyyyyyyyyyyyyy!!!!!!!

Lisa,

Ivi una kituo cha ushauri, kama huna basi fungua haraaaka,

Bado!! fasta!!

Anyway unafaa kuwashauri wengine, "about the need for intergrated features in life consideration" wasifanye mambo machache kuwa muhimu wakati wa kuanza maisha,
Inawacost wengi sana ndo maana mawazo yako yaingie kwa wengine fastaa!
 
Nahisi pia wazazi wa karne hii wanawaambia binti zao kuwa watafute wanaume wenye uwezo, hawataki wale wa kuanza nao, Mm nakumbuka mama yangu alikuwa ananiambia kuwa mwanaume mzuri ni yule mlieanza naye kuchuma kila kitu, lakini si kuvikuta atakunyanyasa navyo.
Na ndipo hapo ukivunja glass anakuuliza unajua bei yake, hivyo nilinunu nikiwa Uingereza, sasa mwenzangu na mm umesomea ngumbaru Uingereza unaiona kwenye ramani.wapi na wapi. Akuuuuuu ndiyo maana mm niapata msamba mwenzangu life goes On.

Baelezee..
 
kama unafanya kazi serikalini au kwenye halmashauri hata haitakiwi uisome hii sredi
spendi wanaume wavivu wa kufikiri
Dah! hii kali kabisa, ngumu kumeza mtu atakayetoka serikalini hawezi kufanyakazi Private company hasa International Companies, nina rafiki yangu yupo serikalini kwa wiki sidhani kama anafanyakazi zaidi ya masaa 30. ni kweli ni wavivu na ni moja ya sababu ya nchi hii kuwa maskini.

Hati ya kumilikishwa kiwanja kimoja tu nimeipata last week baada ya process ya miezi 8. you're right.
 
Nahisi pia wazazi wa karne hii wanawaambia binti zao kuwa watafute wanaume wenye uwezo, hawataki wale wa kuanza nao, Mm nakumbuka mama yangu alikuwa ananiambia kuwa mwanaume mzuri ni yule mlieanza naye kuchuma kila kitu, lakini si kuvikuta atakunyanyasa navyo.
Na ndipo hapo ukivunja glass anakuuliza unajua bei yake, hivyo nilinunu nikiwa Uingereza, sasa mwenzangu na mm umesomea ngumbaru Uingereza unaiona kwenye ramani.wapi na wapi. Akuuuuuu ndiyo maana mm niapata msamba mwenzangu life goes On.

hahahha, bwana we! wacha tu maisha haya, lakini nashukuru niliolewa na wamaume niliempenda sana, sikuwa na wazo la pesa/mali kabisa, but Mungu amenijalia mwanaume mchakarikaji, mpaka hapa tulipo huwa nasema asante zirudi kwake, na hao ma ready made tayari wana wanawake mji mzima, ushindani wa kuvunja kiuno, wacha bwana, kuona maendeleo ya pamoja raha sana sana.
 
Note: MKAKA KAMA HUNA SHULE, MJASIRIAMALI WA UKWELI, HUNA HELA usijisumbe hutapendwa hata uwe handsome kivipi.Ukihurumiwa kama ni handsome unapewa uroda mara moja kisha ujiondokee

bolding,;lakini mapenzi ya kweli hayapo machoni mwa mtu au kwenye vitu alivyonavyo, yapo moyoni, inawezekana asiwe NA SHULE, SI MJASIRIAMALI WA UKWELI, HANA HELA lakini akapendwa tena kuliko huyo mwenye vyote hivyo,. watu tupo tofauti, sasa kama wanawake wote watawakimbilia wenye mali na elimu wale wasokua navyo waende wapi? na hao ni binadamu na wana haki ya kupendwa na kuheshimiwa kama wanaume wengine,.mbona mim nilimpenda machinga tena ambaye hakufika hata la saba wakati huo nipo form six, nimemzidi elimu mpaka kipato na mpaka leo twadumu kwa nguvu za maanan, twapendana asikuambie mtu., twasubiri tu kufunga ndoa soon suala la mapenzi bwana kwa tunaolijua haijalishi kitu bali ni utu,.waweza kuwa na vyoote hivyo lakini amani isiwepo,.. tuache ubaguzi kwenye mapenzi jamani, tupendane kweli kama tumeamua kujiingiza kwenye mapenzi,.mungu ndiye mpaji wa yote, hawezi kukuacha utaabike hadi mwisho, ipo siku tu atakuinua na wewe uwe kama wao wenye navyo,.cha muhimu ni uvumilivu, kama mmependana akiwa hana ndo wakati wa kushauriana ni jinsi gani utamsaidia kutokana na elimu au kipato ulichonacho na si kumtenga au kumdharau, huwezi jua atakua na msaada gani kwako huko baadae.
Bidada huo ni upepo utapita tu. Hapo kwekundu shosti, tuulize tuliotangulia na yakatufika, ndoa na urafiki nazidi kusisitiza ni vitu tofauti. Unaenjoy sasa ila ukifunga ndoa utaona mabadiliko. Ushauri wangu piga ua olewa na mtu anayekuzidi au kwa bahati mbaya muwe mnalingana elimu, utajiri na umri. Vinginevyo, kubali matokeo
 
Mhuuu! Tatizo iyo kiajabu ajabu bado,
Miyo ya watu wengine ni ya nyama, wewe uje uupasue ivi ivi, kama thread inavosema basi imi nina moyo wa kuumia, .....
........, Ngoja nisepe future ya hapa kwako haijajulikana!
nikusaidiaje tena jaman
au ni janja ya AFRODANZI??
 
Back
Top Bottom