KERO Wahusika wa Sekta ya Elimu muwahurumie watu wa hali ya chini kwa hii michango...

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tarehe 6 na 7 mwezi huu wa tano kulikuwa na mitihani ya mock Wilaya.

Wilaya ya Mvomero watoto walichangishwa 'rim papers 10' kwa kila mtihani kwenye uhalisia wa matumizi, ni mtihani moja tu wa hesabu ulitumia karatasi nne. Mitihani mingine ilitumia karatasi mbili.

Karatasi zilizo zidi zilitumika kwa matumizi gani? Lakini pia kulikuwa na changisho la shilingi elfu moja kwa kila mtoto.

Kama hiyo haitoshi walimu wasimamizi wa mitihani kutopewa posho ya chakula na nauli ni utaratibu kutoka wizara husika?

Nawailisha.

IMG-20240507-WA0015.jpg

IMG-20240507-WA0018.jpg
 
Wazazi si mnavikao na walimu mashuleni hizi ndo kero za kuwasilisha huko nahisi utapata majibu sahihi.
Kila mkoa unapambana ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi cha msingi wazazi/walezi mshirikiane na walimu na mwisho kabisa mikoa mingine inachangia rim nzima kwa kila mwaka hili kuondoa hii adha ya kuchanga makaratasi mara kwa mara
 
daaah imagine Mtu anahoji karatas 4 nilizo changia zimeenda wapi? je ange ambiwa alete limu si angeenda wizarani kabisa

umasikini wa AKILI ni kitu kibaya zaidi kuliko umasikini wa FEDHA
Take care of the Pennies and the Pounds will take care of themselves.., watu wenye vingi wanabaki na hivyo vingi kwa ku-account vichache vinatumikaje..... Economy of scale michango midogo midogo kwa kila mtu mwisho wa siku inakuwa vingi...,Ndo-ndo-ndo si Churuchuru...., issue sio kilichofujwa ni kidogo au kikubwa issue ni ufujaji kama upo hautakiwi no matter udogo wake....
 
Back
Top Bottom