Waheshimiwa Wabunge kulala Bungeni: Je ni kutafakari au kusinzia?

S Wassira huyu hapa: (Ndiye alikuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni):!

Wasira.jpg
 
Hiyo tie imeegemea "kitambi" au imepulizwa na feni ipo juu juu? mh hizi posho zingefutwa tu maana
 
Halafu watu kama huyu jamaaakistuka usingizini ndio huwa mstari wa mbele kupinga hoja mradi tu aambie " aliyetoa hiyo hoja ni Tundu Lissu" na huunga hoja hata kama hakuisikia mradi tu aambiwe aliyetoa hoja hii sasa ni January Makamba
 
KIBUGUMO nakuunga mkono!!! Mapumziko ni haba sana!! Watu wako kwenye ULABU hadi saa za usikiu mkubwa; wakiondoka waondoke na mzigo wa chumbani (bed room baggage)..Kweli asubuhi utayasikia yanayojadiliwa??? Ndiyo maana wengi wao hata MAKABRASHA wanayowekewa kwenye pigeon holes (visanduku kwa kila Mh kwa ajili ya documents) huwa hazisomwi!! Toka lini mtu kama siyo JINIASI akaweza kusoma mambo muhimu na kuyaelewa wakati yu KILAJI CHAKARI??!! MUNGU SAIDIA Tz

hahahahaha kibugumo pale tambaza!!
 
Wanaingia kwenye mijadala wakiwa tayari wamekula supu za kuku na nyama choma kwa wingi. Hivyo lazima watalala tu.
 
Acheni kumsingizia baba wa watu nyie watoto; hamuoni kuwa anafanya maombi ili bunge lipitishe bajeti ya akina magamba..........sasa kajakustuka, anakuta Mwiba mwingine; eti yule dogo wa CDM karudisha Shangingi.....ndoto ikawa kilio nusura ajikojol........
 
Sasa hivi kuna lugha mpya imekuja tunapoona waheshimiwa wakiwa wamesinzia huku vikao vya bunge vikiendelea pale bungeni, kwa mfano gazeti moja la kilasiku kutoa picha ya muheshimiwa naibu waziri wa ushirikiano wa Africa Mashariki, Dk. Abdulla Juma Saadalla akiwa ameuchapa usingizi kabisa pale bungeni siku ya jumanne katika kikao cha kuchangia bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2011 -2012 lakini lugha ilyotumika pale ni kua alikua ANATAFAKARI jambo! Haya tena siku ya jumatano gazeti hilohilo limetoa picha ya muheshimiwa waziri wa Nnchi,ofisi ya Raisi (Mahusiano na uratibu) Stephen Wassira naye kwenye picha gazeti la jumatano akiwa anaonekana ameuchapa usingizi kabisa,lakini lugha iliyotumika pale ni kua ANATAFAKARI! jamani wanaJF wenzangu nisaidieni kuhusiana na hii lugha!
Jamani Mzee Wasirra anasumbuliwa na UZEE msamaheni
 
Wanamdhihaki!! Sasa anatafakari nini? John Komba alitolewa hivyo akasema ati alikuwa anasali, sijui huyu atasemaje?

Twende mbele turudi nyuma huyu mtu amezeeka tangia enzi za Mwalimu. Huo ni ujumbe kwa Rais kwamba amechoka anahitaji kupumzika.
 
Ajabu ni kwamba wanasinzia lakini bado wanendelea kugonga meza bila hata kujua ni kitu gani kimeongelewa!



Na cha ajabu zaidi wanakuwa wa kwanza kusign form na voucher za mahudhurio na malipo ya posho (sitting allowance)!!!!
 
Back
Top Bottom