Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,292
Sasa hivi kuna lugha mpya imekuja tunapoona waheshimiwa wakiwa wamesinzia huku vikao vya bunge vikiendelea pale bungeni, kwa mfano gazeti moja la kilasiku kutoa picha ya muheshimiwa naibu waziri wa ushirikiano wa Africa Mashariki, Dk. Abdulla Juma Saadalla akiwa ameuchapa usingizi kabisa pale bungeni siku ya jumanne katika kikao cha kuchangia bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2011 -2012 lakini lugha ilyotumika pale ni kua alikua ANATAFAKARI jambo!
Haya tena siku ya jumatano gazeti hilohilo limetoa picha ya muheshimiwa waziri wa Nnchi,ofisi ya Raisi (Mahusiano na uratibu) Stephen Wassira naye kwenye picha gazeti la jumatano akiwa anaonekana ameuchapa usingizi kabisa, lakini lugha iliyotumika pale ni kua ANATAFAKARI!
Jamani wanaJF wenzangu nisaidieni kuhusiana na hii lugha!