Mjue the Hungarian Lady Vampire au Blood Countess

Mjue the Hungarian Lady Vampire au Blood Countess

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,195
Reaction score
10,709
Habari za mchana wakuu, Bila shaka jumamosi njema sana leo. Naomba kuleta Uzi kuhusu bibi mkubwa mmoja ambaye kwenye soma soma za hapa na pale amenipa hamasa ya kushare nanyi historia ya maisha yake.

Karibuni.
Mnamo tarehe 7 mwezi wa Agosti mwaka wa 1560 dunia ilipata kumpokea mtoto wa kike katika familia yenye kulelewa na ufamle Wa Hungary kipindi hicho. Katika eneo la Nyírbátor , kwenye ufalme Wa Hungary. Wazazi wake wakiwa ni Baron George VI Báthory pamoja na Baroness Anna Báthory walimpatia Mtoto huyo jina la Elizabeth Báthory de Ecsed. Na alikuwa ni katika waheshimiwa ambao walikuwa wakipata msaada na hata ruzuku nyingi kutoka katika ufalme Wa Hungary.

Wanahistoria wengi wanadai kuwa wazazi wake Elizabeth walikuwa ni ndugu na hii ilipelekea Elizabeth kuwa na matatizo ya kiafya kama vile Kupatwa na Usingizi pamoja na kutoka damu puani. Elizabeth alianza kufundishwa ukatili tangu akiwa mdogo sana kwani alikuwa akishuhudia watu wakichinjwa na kutolea viungo vyao.

Ijapo baadhi ya wakazi Wa eneo lile wanadai kuwa familia ya Barron George VI walikuwa wakifanya mpaka ibada za kichawi hivyo matendo yao yalikuwa ni dhahiri.

Elizabeth alitolewa mahari akiwa na umri Wa miaka 10 na alipofikisha miaka 15 aliolewa na Ferenc Nádasdy , mtoto Wa Barron Tamás Nádasdy de Nádasd et Fogarasföld, na hii ilikuwa ndio mbinu ya kudumisha urafiki Wa kimipaka na kutokuruhusu utawala kuangukia sehemu nyingine.

Lakini kabla ya hapo inadaiwa kuwa Elizabeth alipata mimba akiwa na miaka 13 aliyopewa na mtoto Wa mkulima tu. Na kuondoa ile fedheha familia hii ya Barron George VI walimgawa mtoto Huyo kwa mwanamke ambaye alipewa pesa nyingi tu na kupewa maelekezo ya kutoka mji huo na kuelekea Wallachia. Lakini kutokana na hadhi ya Elizabeth ndani ya Ufalme huo alikataa kuchukua ubin Wa mume wake hivyo Bwana mdogo Nádasdy akachukua ubin Wa Báthory.

Katika sherehe hiyo ya harusi walihudhuria wageni zaidi ya 4500.
Elizabeth alikuwa anajua kuongea na kuandika lugha mbalimbali mfano: Kilatini, Kijerumani, Kigiriki pamoja na Kihangari.

Elizabeth_Bathory_Portrait.jpeg
Hii ndo picha pekee inayotumika kuchorea picha zingine za Elizabeth.

*Je alifanya nini mpaka aitwe Lady Vampire:*

Mara baada ya mume wake kuwa kamanda Wa Vikosi vya Hungary, alikaa muda mwingi na Mjomba wake pamoja na Shangazi yake ambao wote walikuwa wanafanya Matambiko ya kishetani (waabudu Shetani) na kwa vile Mume Wa Elizabeth alipenda kuwapatia mateso raia basi ndo ikawa ndo Elizabeth amepata mwanzo mwema Wa kufanya uchafu wake. Mbaya zaidi ni pale ambapo aliingiza mpaka baadhi ya njia za kutisha za kutesa watu.

Mfano: *the Iron Maiden* hii kitu ilikuwa ni noma sana kwani ilikuwa ni kama gogo Mfano Wa umbo la mwanamke ambalo ndani kumejaa misumari inayoangaliana hivyo akiwekwa binti humo basi ni maumivu yasiyo na Mfano lakini hii ndo ilikuwa ni furaha yake.

Pia kupitia ushauri Wa Shangazi pamoja na Mjomba wake ndo alipokuja na wazo la kuanza kuoga pamoja n kunywa damu za mabinti mabikira ili kujitunza urembo wake na shape. Mpaka anafariki inasemekana alihusika na vifo vya mabinti zaidi ya 650, hapo kuna waliokuwa wanachunwa ngozi wakiwa hai, wengine walichomwa sura zao na sehemu za siri kwa chuma chenye moto. Elizabeth hakuishia hapo alikuwa anaweza kumchoma Binti kisu hata cha tumbo na kukinga damu kisha kunywa damu.

IronMaiden.jpeg
*The Iron Maiden*

Mwisho wake:
Baada ya kuwa imejulikana baina ya wananchi, kukaanza maneno ya chini chini, lakini mdogo mdogo mpaka yakafika kwenye ufalme, Mara baada ya Waziri Wa kilutheran Bwana István Magyari alipopeleka mashitaka kwa niaba ya wananchi kwenye mahakama ya Vienna.

Ingawa baadhi ya viongozi walipinga hoja hizo lakini, uongozi Wa kifalme Wa Hungary kupitia Mfalme Matthias II ambaye alimtuma bwana György Thurzó , kwenda kuchunguza ishu nzima. Mwaka Wa 1610 mwezi Wa Machi, Bwana huyu aliwateua watu wawili wakakusanye ushahidi Wa kutosha. Katika kipindi cha mwaka 1610 na 1611, waliweza kukusanya ushahidi kutoka kwa mashahidi zaidi ya 300.

Ushahidi ulionesha kuwa wafanyakazi wa kike ndani ya familia ya Báthory walikuwa ni mabinti kuanzia miaka 10 mpaka 14, wengi wao walikuwa watoto wa wakulima, na walikwenda kufanya kazi kutokana na ahadi za kupata mshahara mzuri, kitu ambacho walikipata ila kwa muda tu, kwani baadaye mwana mama huyu alianza uchafu wake.

1_bcY9wvqAe5BU-i4lpYp3fA.jpeg
mchoro ukionesha baadhi ya mateso aliyokuwa anafanya kwa mabinti hao.

Kutokana na Makumbusho ya Jiji la Budapest inadai kuwa Vyuma vya moto vilitumika kwenye kuchoma chuchu za mabinti hao, na hats kuingizwa kwenye sehemu za siri. Wengine walifungwa nguo nyingi na kamba kisha siafu wekundu walikuwa wanawekwa ndani yao.

Ijapokuwa kuna watu wanadai lia kuwa Elizabeth alikuwa ni Cannibalisticbehavior. Alipatikana na hatia ya kuua kwa kudhamiria na cheo chake cha kuwa mtoto Wa Barron George VI kilimuokoa kuuawa.

Ijapokuwa hakufungwa jela alipewa hukumu na death by confinement ambayo ni kuweka mbali ya jamii yaani unakaa peke yako mpaka utakapokufa. Bi mdada huyu aliwekwa katika chumba kimoja chenye Giza Nene tensa chenye dirisha moja Dogo kwa ajili ya chakula tu.

Aliishi ndani ya chumba hicho kwa miaka minne tu. Mpaka siku moja alipomwambia mlinzi Wa kuwa "anasikia baridi sana" lakini Jamaa akamjibu kuwa "Lala tu Madam" asubuhi yake walikuta anekwisha kufariki. Elizabeth alifariki tarehe 21 mwezi Wa Agosti Mwaka Wa 1614 akiwa na miaka 54.

Asante sana kwa muda wenu.
Alikuwa ni mrembo Wa kiasi chake lakini ndo hivyo
Elizabeth%2BBathory.jpeg

I stand to be corrected anywhere........
Marejeo:
Cc. @Mshana_Jr @Malcom_Lumumba na wengine.....
 

Attachments

  • Elizabeth%2BBathory%2BFigurine.jpeg
    Elizabeth%2BBathory%2BFigurine.jpeg
    16.9 KB · Views: 151
Hiyo CV sio ya kitoto mkuu maana kufanya vitu hivyo inahitaji moyo aa kipekee
 
Hatari sana ila ndo maisha tu
 
Cha ajabu alikua demu,,angekua mwanaume nisinge shangaa sana,,
 
Uzi huu unanikumbusha mbali hasa naposikia neno Cannibalism, in fact 90% ya viumbe wa baharini na kwenye maji kiujumla ndio wana hii tabia ya Cannibalism , yaani tabia ya kuweza kula kipande cha mwili au mwili wote wa kiumbe mwenzako wa aina yako.

Kwa binadamu, inadhaniwa kuwa wachawi ndio wana hizi tabia za kula watu, na kwa maelezo ya mwandishi ni kuwa ELIZABETH BATHORY alikuwa anafanya ibada za kichawi.Hivyo ni ushahidi tosha kuwa tabia za wachawi ni kula watu.

Naomba kuuliza hivi UCHAWI na UKATILI ni nadharia mbili zanazoenda kwa pamoja? Maana nasikia wachawi wengi huwa wana roho ngumu za kikatili. Je hakuna wachawi wenye moyo wa huruma. Naomba majibu wakuu.

Nawasilisha
 
Uzi huu unanikumbusha mbali hasa naposikia neno Cannibalism, in fact 90% ya viumbe wa baharini na kwenye maji kiujumla ndio wana hii tabia ya Cannibalism , yaani tabia ya kuweza kula kipande cha mwili au mwili wote wa kiumbe mwenzako wa aina yako.

Kwa binadamu, inadhaniwa kuwa wachawi ndio wana hizi tabia za kula watu, na kwa maelezo ya mwandishi ni kuwa ELIZABETH BATHORY alikuwa anafanya ibada za kichawi.Hivyo ni ushahidi tosha kuwa tabia za wachawi ni kula watu.

Naomba kuuliza hivi UCHAWI na UKATILI ni nadharia mbili zanazoenda kwa pamoja? Maana nasikia wachawi wengi huwa wana roho ngumu za kikatili. Je hakuna wachawi wenye moyo wa huruma. Naomba majibu wakuu.

Nawasilisha
Wachawi wenyewe huruma tupo mkuu
 
Back
Top Bottom