Wahariri kuipigia makofi hotuba ya Lowassa

Wahariri kuipigia makofi hotuba ya Lowassa

uliwah kuona DAILY NEWS la zamani wakati Mkapa akiwa mhariri wa hilo gazeti? nenda maktaba au makumbusho yoyote ukaulizie alafu ulinganishe na la siku iz. utaona tofauti kubwa. ni sawa na barcelona na yanga
 
Ukweli ni kuwa katika zama hizi za leo Tanzania hakuna waandishi wa habari wenye viwango na weledi ukiwatoa wale Wazee akina Jenerali Ulimwengu na group lake wanaomiliki wa gazeti la RaiaMwema. Na wenyewe ndio wanaishia ishia hivyo kwa ku retire.

Na hilo wala halina kificho kwani ukitaka 'kupima' basi nunua magazeti ya Kenya kama vile (Nation, EastAfrica nk) na haya kwetu halafu ufanye tathimini ya kuanzia tahariri mpaka repoti za matukio halafu utajua nasema nini. Kwa kweli inasikitisha kwani fani ya uandishi Tanzania inasikitisha mno kwani imejaa wababaishaji na wabangaizaji. Na ukija kwenye taaluma (profession) hakuna kitu kabisa.
 
hata mimi nisie muandishi nisingeuliza hilo swali! kweli nchi hii haina waandishi wa habari, na ndo mana kipindi hiki badala ya kuripoti habari wao wanapiga kampeni na kuwachagulia wananchi wagombea
 
Tz mwandishi wa habari ni mtu aliyechukua masomo au mchepuko wa art au sanaa. Miaka ya Nyerere hawa walikuwa direct employment baada ya F IV
 
Wadau,nimeshangazwa na wahariri waliohudhuria mkutano wa Lowasa kupiga makofi kushangilia alichokua anakisema ENL...hapa sio bure.
Inaonyesha kuwa wako compromised na hawako neutral...wanafedhehesha
 
Wadau,nimeshangazwa na wahariri waliohudhuria mkutano wa Lowasa kupiga makofi kushangilia alichokua anakisema ENL...hapa sio bure.

Mimi nilisoma Nipashe ya kwamba yeye ndiye aliyewasafirisha kutoka Dar hadi Dodoma hivyo walikuwa naa haki ya kumpigia makofi.
 
KADA AFICHUA SIRI MBIO ZA LOWASA


Hata hivyo katika kundi hilo la wajumbe waliokwenda kwa Lowasa , mjumbe mmojawapo amezungumza na waandishi wa habari na kwenda bayana kuwa hakuwa akijua kinachoendelea


"mimi nilikuwa pale makao makuu, nikawakuta watu pale wapo na magari wanasema twendeni nikapanda gari nikaenda, nilipofika kule nikashangaa kuona mambo yanayoendelea. Hata zile shilling laki sita (600,000) zilizotolewa na Mukasa wala hatukuchangishana, alizitoa mwenyewe mfukoni mwake" Jacqueline Ngonyani mjumbe kutoka Ruvuma.


Chanzo Raia Tanzania

Toleo no. 0338
 
KADA AFICHUA SIRI MBIO ZA LOWASA


Hata hivyo katika kundi hilo la wajumbe waliokwenda kwa Lowasa , mjumbe mmojawapo amezungumza na waandishi wa habari na kwenda bayana kuwa hakuwa akijua kinachoendelea


“mimi nilikuwa pale makao makuu, nikawakuta watu pale wapo na magari wanasema twendeni nikapanda gari nikaenda, nilipofika kule nikashangaa kuona mambo yanayoendelea. Hata zile shilling laki sita (600,000) zilizotolewa na Mukasa wala hatukuchangishana, alizitoa mwenyewe mfukoni mwake” Jacqueline Ngonyani mjumbe kutoka Ruvuma.


Chanzo Raia Tanzania

Toleo no. 0338

Mtu na akili zako timamu upande gari usijuwe unapokwenda? Akajambe mbele huko asidhani kila mtu ni mpumbavu mwenzake.
 
Mtu na akili zako timamu upande gari usijuwe unapokwenda? Akajambe mbele huko asidhani kila mtu ni mpumbavu mwenzake.

Nikaambiwa panda gari, nikapanda. Hujui unaenda wap na kwa gharama za nan.....mking'olewa meno mnarudi kuanza kushusha lawama. Huwez kuniaminisha kwamba Lowassa alisafirisha Wahariri wote wale mpaka Dodoma bila wahariri hao kuhojikinachoendelea kuhusu gharama za huo mkutano. Wote walihongwa??? Haiwezekan Nonsense.
 
Skuizi gazet langu ni raia mwema hao wengine wakina MAWIO TANZANIA DAIMA'UHURU,MZALENDO,wapo kiitikadi zaidi
 
We unayejifanya kusema walipewa bahasha argue kwa constructive criticism tupeni mfano wa maswali angalau 2 tu ambae we unayejiita mwenye akili ungeweza kuuliza kaa hamna
Mkae kimyaa

Mimi ningekuwa Mwandishi wa habari ningemuuliza Je, Ndugu Lowasa wewe kama mgombea urais huoni kitendo chako cha kutoa fedha kwenye makundi mbalimbali ya jamii ni kama ushawishi kwa jamii hizo ili uonekane kama wewe ndio kiongozi unaefaa? Na je hii si sawa na kutoa rushwa? Hili kwangu lingekuwa swali la msingi sana. Nina uhakika yule mzee angepanic sana .
 
Mkapa aliposema kuwa Tanzania hakuna waandishi wa habari watu walikuja juuu sana. Juzi imejidhihirisha kwenye mkutano wa Lowassa na 'Wahariri'
. Mmoja wao aliuliza, Mheshimiwa unajisikiaje watu kukuita Edward?

Kwa mtazamo wangu ni aibu kwa mwandishi wa habari kuuliza swali la kipumbavu namna hii kwa mtu anayewania nafasi nyeti katika Taifa. Ni aibu kumwuliza mtu anayewania nafasi inayogusa maisha ya maskini walio wengi katika taifa hili. Ni aibu kuuliza swali la kijinga wakati nchi iko hoi kiuchumi.
NB. Mwenyekiti jukwaa la Wahariri mnaaibisha taifa.

Mkapa asante kwa kuuona ukweli huu.

Mkuu ukisoma maswali aliyoulizwa kupitia mahojiano yake na Mhariri wa Raia Mwema Gazeti toleo Na.407 ya Mei 27-June 2 2015 ni aibu tu.
Sijaona maswali ya maana kwenye maeneo muhimu sana.

Mfano.Aliulizwa suala la role Model zake kwenye siasa akajibu Nyerere na Nkrumah .
Akaongezwa swali juu ya hoja hiyo kuhusiana na kama atakuwa Raisi basi watu wategemee staili ya hao role Model zake lakini akaja na majibu mepesi kuwa anawapenda na ataendelea kuwa heshimu na atafanya kazi zake kwa mujibu wa Karama alizopewa na Mungu na mahitaji ya Changamoto na mazingira yaliyopo.

Hapo Mhariri akawa ameridhika na akarukia swali lingine la kipuuzi .

Unasemwa kwamba Wewe pengine ndiye mwanasiasa tajiri kuliko wengine wote hapa Nchini je una mali kiasi gani?.
Unaweza kuzitaja?


Sijui pengine Mhariri haelewi Role Model maana yake nini hasa.

Nilitegemea baada ya majibu ya Lowassa hapo Bluu Mhariri angemalizia alichotaka kukijua kuliko kuwaachia wasomaji .Muda huu ni wa watanzania kusikia toka kwa wahusika nini wanaamini na watakisimamia siyo hadaa hizi. Ni heri anayeweza hata kusema kinafiki kuliko anayeona kusema tu ni dhambi.

Mfano.
Lowasa alizungumzia Chamgamoto moja tu ajira kwa Vijana .Lakini huwezi kulizungumzia hili bila kutuelezwa ni namna gani Ufisadi utakoma ili kufanikisha upatikanaji wa Ajira. Kufa kwa Kiwanda cha Tairi Arusha na Viwanda vingine kulitokana na Ufisadi na mwisho kufa kwa ajira-Mhariri hili yeye hakuiona.


Shida yetu kubwa ni kwamba Wantaznia wengi na hasa wapiga kura wetu hawana uelewa wa kuhoji na kuchambua mambo hivyo ilitegemewa Vyombo vya habari kupitia Wanahabari kuwasaidia katika hili lakini imekuwa kinyume.

UKAWA andaeni Maono na Wanachoweza kukisimamia Wapinzani wenu na hasa CCM kuhusiana na Tanzania tunayoitaka pamoja na mtazamo au ilani ya Chama atakachokiwakilisha ili wimbo wenu uwe mmoja jukwaa kwa Jukwaa Nchi nzima naamini ujumbe utawafikia Watanzania.

Nimejifunza jambo mmoja kuwa Msipofanya hivyo na kama hali inavyojionyesha kupitia Vyombo vya habari hadaa hii itawapumbaza watanzania wengi kama ilivyotokea 2005.

Kurugenzi ya Habari

[h=3]Role Model[/h]
Role Model
“Role Model” is an individual whose activities and experiences provides a “model” around which others can understand the meaning of a concept or form of life at the level of their own individual practice. Indeed, it is difficult to see how an abstract concept can be integrated and understood by someone, until they can see how it can be “lived.”
 
Last edited by a moderator:
Skuizi gazet langu ni raia mwema hao wengine wakina MAWIO TANZANIA DAIMA'UHURU,MZALENDO,wapo kiitikadi zaidi


Mkuu hao unaowataja wako kimasilahi na ndiyo wa hatari kuliko wa Itikadi. Jisomee mahojiano yao Edo gazeti na.407 ya Mei 27-June 2 2015 ukurasa wa 12-13.

 
Kulikuwa na kamati ya maandalizi ilikuwa inaendelea hapa New Safari Hotel chini ya Mathias Manga na Papa King timbwili liliibuka baada ya Mathias Manga kusema ametumia mil 430 Kwa wahariri Wa vyombo vya Habari vyote nchini ambao tayari wako Arusha wakijiandaa na tamasha la kesho yaani leo Papa King alipinga mahesabu hayo kuwa walikubaliana watumie mil 220 iweje iongezeke kiasi hicho huku wakishindwa kuwaongezea wanafunzi Wa chuo cha Moshi ambao wamewalipa 10,000 kila mmoja licha ya kwamba walikuwa na manunguniko hali hiyo ilipelekea Mkurugenzi wa kampuni ya monaban kuingilia kati na kuhakikisha mambo yanaenda sawa... kuna maswali hapa ya kujiuliza kumbe wahariri wote Leo watakuwa stadium sheikh amri abeid ina maana hawawa amini waandishi wao je wanatuambia sisi wasomaji kuwa sasa tusi amini magazeti mpaka wahariri wawe eneo la tukio..
2. wanafunzi kulipwa 10,000 ili kusaliti watanzania na kwenda kumpigia makofi jambazi ambaye alipaswa kuchomwa moto kumbe nikiwa na 10000 naweza kupata hata visifuli vyao, hii inazidi kaiaibisha elimu ya mtoto Wa mtanzania eti mwanafunzi Wa chuo kununuliwa Kwa 10000 huu Ni utahira kabisa hata kama hamjapewa mkopo wenu...
3. Jambazi kama unatumia 430 Kwa wahariri tu siku ya kutangaza nia je mpaka ukamalize kampeni utakuwa umetumia kiasi gani? na utazirejeshaje hizo pesa...

Ama kweli Tanzania nchi ya kitu kidogo siyo wachungaji, masheikh, wahariri, waandishi, wanafunzi naomba Mungu awape ufahamu wakutambua mazuri na mabaya mmykatae jambazi kama nakama mbafanya hivyo kumalizua Nyumba zenu ombi langu msutumie kalamu zenu kuwapotosha watanzania...
 
Back
Top Bottom