Mtaka yote
Senior Member
- Nov 30, 2014
- 136
- 103
Wadau,nimeshangazwa na wahariri waliohudhuria mkutano wa Lowasa kupiga makofi kushangilia alichokua anakisema ENL...hapa sio bure.
Mkapa aliposema kuwa Tanzania hakuna waandishi wa habari watu walikuja juuu sana. Juzi imejidhihirisha kwenye mkutano wa Lowassa na 'Wahariri'
. Mmoja wao aliuliza, Mheshimiwa unajisikiaje watu kukuita Edward?
Kwa mtazamo wangu ni aibu kwa mwandishi wa habari kuuliza swali la kipumbavu namna hii kwa mtu anayewania nafasi nyeti katika Taifa. Ni aibu kumwuliza mtu anayewania nafasi inayogusa maisha ya maskini walio wengi katika taifa hili. Ni aibu kuuliza swali la kijinga wakati nchi iko hoi kiuchumi.
NB. Mwenyekiti jukwaa la Wahariri mnaaibisha taifa.
Mkapa asante kwa kuuona ukweli huu.
KADA AFICHUA SIRI MBIO ZA LOWASA
Hata hivyo katika kundi hilo la wajumbe waliokwenda kwa Lowasa , mjumbe mmojawapo amezungumza na waandishi wa habari na kwenda bayana kuwa hakuwa akijua kinachoendelea
"mimi nilikuwa pale makao makuu, nikawakuta watu pale wapo na magari wanasema twendeni nikapanda gari nikaenda, nilipofika kule nikashangaa kuona mambo yanayoendelea. Hata zile shilling laki sita (600,000) zilizotolewa na Mukasa wala hatukuchangishana, alizitoa mwenyewe mfukoni mwake" Jacqueline Ngonyani mjumbe kutoka Ruvuma.
Chanzo ni Raia Tanzania
Toleo no. 0338