Wahariri kuipigia makofi hotuba ya Lowassa

Wahariri kuipigia makofi hotuba ya Lowassa

Mtaka yote , asante sana kwa kuanzisha huu uzi na kwa kuona madhaifu ya waandishi wetu. Ni muda mrefu waandishi wetu wamelalamikiwa na niseme tu kuwa kwa kiasi kikubwa wanasaidia kuchelewesha mabadiliko katika nchi hii kwa kutofanya kazi yao ipasavyo. Na au kwa kutouliza maswali sahihi.

Kwenye mkutano wa Lowassa juzi, wengine walikuwa wanashangilia kwa kupiga makofi (pengine kufurahia kuwa mheshimiwa amejibu kama jibu lilivyoandaliwa). Sijawahi kuona popote. Ni dhahiri wengi walioitwa kwenye mkutano ule ni maswahiba wa Lowassa na waliitwa kumsafisha. Kwa kweli kazi ya waandishi wa habari si kusafisha watu but to call it what it is. Ni aibu kubwa na wahanga wakuu wa hali hii ni wananchi kwa kuwa hawapati taarifa sahihi bali taarifa zilizotiwa chumvi au zilizokuwa manipulated kwa lengo fulani. Hakuna mtu mwenye akili timamu na mwenye kuitakia mema nchi hii anayeweza kushabikia kilichotokea juzi kwenye mkutano wa Lowassa na waandishi wa habari. They all asked leading questions ili kumpa fursa mheshimiwa ajisafishe. Simply, pathetic. Haikubaliki.

Pasco , ulihudhuria mkutano ule?
 
Duh! Nadhani hili lilikuwa ni group lingine lililokwenda kumshawishi jamaa
 
Hivi Kibanda alishapotea eeee? Maswali ya kijinga kabisa yaani hata hayahitaji mtu kufikiri. Hizi shule hizi, taabu tupu tunaenda kutafuta sijui nini shuleni. Maswali gani hayo hata mtoto wa chekechea mengine anajua majibu yake?
 
Haya ndiyo maswali ambayo wahariri wetu walimuuliza Lowassa jana mjini Dodoma.

1.Mara nyingi nimekuwa nikisikia watu wanakuita Edward,na wewe unawanyamazia tu,huoni ni kama vile hawakupi heshima?

2.Huko mtaani kuna maneno mengi sana yanasemwa juu yako,mengi ya kukuchafua na mengine ya hovyohovyo,kwa nini umekaa kimya?

3.Kwa kipindi cha miezi kumi na mbili ,wewe na wenzako mlikuwa kifungoni,juzi chama chako kilitangaza kuwa adhabu yenu imekwisha,hebu tueleze nini sababu kuingia kifungo hicho?

4.Suala la afya yako limekuwa ni ajenda kubwa huko mtaani,leo tuko hapa,hebu tueleze kama inavyosemwa ni tofauti.

5.Nataka kujua chanzo cha wewe kutoka serikalini,ilikuwa ni nini?hivi ni kweli ulihusika kwenye sakata la Richmond au lilikuwa zengwe la
kisiasa?

6.Umewahi kunukuliwa mara nyingi ukisisitiza kuhusu elimu kwanza,tofauti na kauli mbiu ya serikali yan kilimom kwanza,huoni kama unapingana na mipango ya serikali?

7.Umekuwa ukilitazama tatizo la ukosefu wa ajira kama bomu linalosubiri kuripuka,pili umekuwa ukiitwa majina mabaya mara mwizi mara fisadi,lakini sasa hali ni tofauti,naona kama vile nyota yako inang'aa,siri ya jambo hili ni nini?.

8.Huko nyuma wewe na raisi Kikwete mliitwa Boys ii men,na wakati mwingine ulisema wewe na JK hamjakutana barabarani,hebu tueleze urafiki wenu ukoje?

9.Ipo dhana wewe kuwa ni tajiri sana na umejirimbikizia mali na wengine wanasema hilo linaweza kuwa kikwazo katika safari yako ya matumaini,nataka kujua chanzo cha utajiri wako.

10.Nini mtazamo wako kuhusu serikali ijayo,unafikiri serikali ya awamu ya tano inatakiwa ijielekeze kwenye ipaumbele gani?pili katika suala la uchumi unalitazama vipi suala la dola kuporomoka,pia unatoa tahadhari gani kwa ccm katika kuelekea uchaguzi mkuu?

11.Katika mchakato huu wa uraisi,ikiwa hutateuliwa na chama chako,nini plan B yako?

12.Ipo dhana kuwa wewe ni mtu wa visasi na inasemwa kuwa ukiingia madarakani utalipiza visasi kwa wabaya wako,unalizungumziaje hili?

13.Mtandao ulionao hauna tofauti na ule uliomuingiza Kikwete madarakani,seikali ya awamu ya tano itakuwa na tofauti gani na serikali ya
awamu ya nne?


My take,
Maswali ya kitoto sana,kuna mawili tu ambayo angalau yanahadhi ya mwanahabari aliyeiva.

Mengne utumbo tu
unategemea nini wakati kila mhariri naskia alipewa Laki Tatu NA wengine walisafirishwa NA Ndiege ! Si ndio maana walimpigia makofi! Tangu nizaliwe hii ndiyo mara ya kwanza kuiona hata Mwalimu alipokuwa anaita press conference pale Msasani walikuwa wanaenda ma chief reporters au senior journalists lakini these days editors wana chase stories na waandishi basi ni Ngumu kutofautisha editor ni nani na Mwandishi ni nani. Wahariri tujirekebishe! Hivi na Makaidi na Mtikila akiwaita mtaandika kama mlivyofanya kwa mzee Leigwanani
 
Edo ni kama Blatter....wanaosema watasema weeee....watakaonyoosha mikono kama Figo, haya.....
 
Weka hayo maini yako tuyaone siyo unaishia kupakazia tu?

Halafu weka na chanzo cha hayo maswali uliyoandika isije ngonjera Tu.
 
Weka hayo maini yako tuyaone siyo unaishia kupakazia tu?

Halafu weka na chanzo cha hayo maswali uliyoandika isije ngonjera Tu.

Povu la nin ndugu?
Kama unayo maswali mengine yaliyoulizwa unayoyajua wewe weka hapa ili haya yawe ngonjera
 
Wahariri walikuwa Moro ktk mafunzo ya BBC kuhusu Uchaguzi na walifanyia hotel ya Lowassa iitwayo Nashera mara yakaletwa majina maalum ya Wahariri NDIO MZEE waende Dodoma ktk press conf ya MZEE semina ikafa wakaenda huko. Sasa sijui walilipwaje maana kwahiyo unategemea wangeuliza nini? Na hapo muda haukutosha ungeshangaa lingekuja swali hili...Ukiwa Rais mwezi wa kumi utaendelea kuchangia makanisa au Tuambie baraza lako la mawaziri...Yaaani bahasha za kaki ni shida zimeharibu akili njema kuwa wehu.
 
Umeshapokea bahasha halafu ujifanye kuuliza swali la maana umuaibishe Lowasa utajuta kuzaliwa.bora hata angekuwa na akili basi kaulizwa maswali ya kijinga nae kayajibu kijinga .nimemwangalia clouds tv jamani huyu mzee ni wa kumuonea huruma hawezi hata kujieleza masikini ya mungu na hapo ndio kachaguwa maswali mwenyewe.
 
Wewe hukushangaa waandishi wanapiga makofi baada ya Lowasa kujibu kama inavyotakiwa. Teh teh Only in Tanzania.
 
We unayejifanya kusema walipewa bahasha argue kwa constructive criticism tupeni mfano wa maswali angalau 2 tu ambae we unayejiita mwenye akili ungeweza kuuliza kaa hamna
Mkae kimyaa
 
Hivi Kibanda alishapotea eeee? Maswali ya kijinga kabisa yaani hata hayahitaji mtu kufikiri. Hizi shule hizi, taabu tupu tunaenda kutafuta sijui nini shuleni. Maswali gani hayo hata mtoto wa chekechea mengine anajua majibu yake?

chekechea ya nchi gani hiyo na mimi nipeleke wanangu ndugu mantissa?
 
Mkapa aliposema kuwa Tanzania hakuna waandishi wa habari watu walikuja juuu sana. Juzi imejidhihirisha kwenye mkutano wa Lowassa na 'Wahariri'
. Mmoja wao aliuliza, Mheshimiwa unajisikiaje watu kukuita Edward?

Kwa mtazamo wangu ni aibu kwa mwandishi wa habari kuuliza swali la kipumbavu namna hii kwa mtu anayewania nafasi nyeti katika Taifa. Ni aibu kumwuliza mtu anayewania nafasi inayogusa maisha ya maskini walio wengi katika taifa hili. Ni aibu kuuliza swali la kijinga wakati nchi iko hoi kiuchumi.
NB. Mwenyekiti jukwaa la Wahariri mnaaibisha taifa.

Mkapa asante kwa kuuona ukweli huu.
 
Back
Top Bottom