Wageni wengine bwana du!

Wageni wengine bwana du!

Sio kutawaliwa mi nilitaka wewe free kuenjoy bila kuchupa mipaka
Haya maisha ku-enjoy ni kuwa na kazi unayoifanya kwa bidii na inakuingizia kipato kizuri cha kukuwezesha kufanya mambo yako mengine mengi. Kuangalia Tv siku nzima ndio inawafundisha kuwa wachapa kazi au inawadumaza?
Ushauri: Watafutie kazi hapo kwako za kutosha, waambie kwa masaa 6 utawapa hata kahela fulani. Wapangie ratiba. Kazi masaa x, Tv masaa X nk. Na tv waangalie program ya maana sio kuwaangalia wasanii tu wanatingisha vikoki vyao siku nzima. Na kama hakuna kazi basi WAONDOKE. Wakakae na ndg mwenye kazi au kwa wazazi wao.
 
Nawasalimu!
Naomba nieleweke nyumba inayotembelewa ndo nyumba yenye baraka. Hivyo nisitafsiriwe kama mchoyo. Ipo hivi nimetembelewa na shemeji zangu wawili mmoja 15 na mwengine 17 hivi,japo nimeshangaa kwetu sio rahisi kutembelewa na shemeji kama dada yao hujamuoa kindoa,sasa kama tulivyo wengi maisha yetu mi naishi kwenye nyumba yenye vyumba vitatu ,kimoja ni stoo ya mpunga na mahindi nilihofia lock down,kwa hiyo natumia vyumba viwili kimoja w atoto na kilichobaki sisi.
Sasa kwa heshima nimeona niwahamishie w atoto sebuleni wao walale kwenye kitanda cha w atoto.
Mambo yaliyo nishangaza kwa ndugu hawa;kuangalia sinema zetu kutwa nzima hadi taarifa ya habari ya saa mbili usiku mpaka niwaombe zaidi ya mara moja ndo waniruhusu, hakuna anaenisalimia asubuhi tunatazama wakati mwingine Mimi huwasalimia,ajabu mmoja alimanusura akeshe kwenye tv bila kujali makelele pale Maana w atoto wamelala kwenye Kochi na kiufupi ni nyumba nzima , sasa kali ya mwaka dogo kagoma kushuka kutoka kiti (office chair)tulikuwa tukula nje kwenye kivuli ,nilipo jaribu kumwambia vipi dogo utakulaje uko juu hivyo kajibu "sili juu nakula chakula". Nikakaa kimyaa. Dogo kasogeza kiti juu ya jamvi. tukala hivyo hivyo.
Jamani sijui wengine mmewahi kuyapitia haya, kwa mbali natamani waondoke hata kesho. Adabu yao ipo chini sijui wamelelewaje?.N.a. dada yao anaangalia tu.
Nawasilisha
(copy &paste).
Wageni wako ni watoto kwanza, pili wamepata malezi ya hovyo. Simamia wanao wasiangukie huko, maana hata hamjaoana, sijui hiyo ni desturi ya wapi?
 
Siwezi vumilia ujinga Mimi jamn ningeshafukuza unatesekaje kwenye nyumba yako
 
Tafuta shamba uanze kwenda kulima nao siku mbili alaf ya 3 unawaachiza waendelee kukomaa nalo kila siku wataondoka wenyewe hapo nyumbani,,, ila ukiendelea kuwanunulia kifurush cha sinema zetu utateseka. Wataalikana ukoo
 
Mi tatizo naliona kwako na mkeo sio hao wageni.
Na ikiwa wana majibu ya namna hiyo na dada yao(mkeo) hana muda wa kuwakanya/kukemea jambo hilo basi ulipoenda kuoa heshima na ustaarabu ni msamiati mgumu sana.
Ongea na mkeo na usimamie unachokiongea kama MWANAUME. Hao wakiondoka watawaalika wengine mwishowe wanao utawalaza na magunia ya mahindi maana hata hiyo sebule watakuja wengine.
 
Unataka ushauri wa nini wakati umecopy na kupaste?
 
Nawasalimu!
Naomba nieleweke nyumba inayotembelewa ndo nyumba yenye baraka. Hivyo nisitafsiriwe kama mchoyo. Ipo hivi nimetembelewa na shemeji zangu wawili mmoja 15 na mwengine 17 hivi,japo nimeshangaa kwetu sio rahisi kutembelewa na shemeji kama dada yao hujamuoa kindoa,sasa kama tulivyo wengi maisha yetu mi naishi kwenye nyumba yenye vyumba vitatu ,kimoja ni stoo ya mpunga na mahindi nilihofia lock down,kwa hiyo natumia vyumba viwili kimoja w atoto na kilichobaki sisi.
Sasa kwa heshima nimeona niwahamishie w atoto sebuleni wao walale kwenye kitanda cha w atoto.
Mambo yaliyo nishangaza kwa ndugu hawa;kuangalia sinema zetu kutwa nzima hadi taarifa ya habari ya saa mbili usiku mpaka niwaombe zaidi ya mara moja ndo waniruhusu, hakuna anaenisalimia asubuhi tunatazama wakati mwingine Mimi huwasalimia,ajabu mmoja alimanusura akeshe kwenye tv bila kujali makelele pale Maana w atoto wamelala kwenye Kochi na kiufupi ni nyumba nzima , sasa kali ya mwaka dogo kagoma kushuka kutoka kiti (office chair)tulikuwa tukula nje kwenye kivuli ,nilipo jaribu kumwambia vipi dogo utakulaje uko juu hivyo kajibu "sili juu nakula chakula". Nikakaa kimyaa. Dogo kasogeza kiti juu ya jamvi. tukala hivyo hivyo.
Jamani sijui wengine mmewahi kuyapitia haya, kwa mbali natamani waondoke hata kesho. Adabu yao ipo chini sijui wamelelewaje?.N.a. dada yao anaangalia tu.
Nawasilisha
(copy &paste).
Mimi hiyo Copy & paste ndio imenimaliza kabisa 😃😃😃😃😃
 
usiwachekee mwambie mke wako wanatakiwa wawe watii, au waondoke mara moja.

mimi dogo alianza kumchukulia poa shemeji yake, nikawambia dogo huyo siyo mke wako ni mke wangu mimi tu.
 
Sio copy n paste. Huyu yamemtokea mwenyewe. Ameoa kutoka familia duni isiyokua na malezi Bora. Yeye kaangalia sura na makalio. Acha ale mavi.
😋😋😋 Dah kama anakula mavi atakua anafaidi sana aisee.
Mambo yetu yaleee. 😋😋
 
Nimecheka sana.Ila pole.
Moja ya kitu huwa sipend na haitatokea kuzoea ni suala la kubadilishiswa utaratibu wa maisha nyumbani kwangu. Never.. mbal na wagen , ma hauz girl pia wana hiz tabia kisa tu ukiwakosoa wanatishia kuondoka.Kwangu nilikataa..

Mama mkwe wangu (ni mnyakyusa kweli kwel,ila mi wale wa mhin so sijui mambo kibao) alikuja home kuuguzwa .bwana wee nilivumilia ila nikasema noo. ikabid anizoee tu.
Ehee...tuelezee...... Funguka mama akeee tupate Cha kujifunza
 
Hao ningewaonyesha segere moja flani kwa vitendo tu bila maneno wangekimbia wenyewe.

NB:
Mke wako atakuwa anakudharua sana ndiyo maana wadogo zake wanakuchukulia poa.
Au labda anamsema kwa wadogo zake ndo maana wanafanya hivyo bila hofu ya shemeji yupo karibu
 
Jamaa mmoja alipokea mashemeji kama ww ila wao walikuwa wakiume, siku zikaenda siku madogo walikuwa wanaangalia match sa ta tano usiku laliga, jamaa alikuwa amelala mapema sa 3 sasa kushtuka, akawambia nenden mkalale kesho mtaangalia, sasa madogo walipopeleka taarifa kwa mama yao kwamba wananyanyaswa hawatakiwi waangalie TV, mama kapokea kama lilivyo anaona watoto wake wananyanyaswa,lkn Infact sio kwel, ila ndg ni kuishi nao kwa akili sometimes kama sio necessary wasije kuwatembeleen, ndugu ni lawama sana
Ikawaje baada ya mama kupokea hizo habari???
 
Kosa namba moja ni kuhamishia wanao sebuleni ili tu kina shem walale chumbani, inakera mno hii kitu,

Kuumia ili kuwafurahisha wengine niliacha maana hupati thawabu yoyote sababu ni unafiki na Mungu hajihangaishi na mnafiki

Familia ulikooa nidhamu yao iko chini sana, cha kufanya kwa vile ni viburi tafuta shamba wapeleke huko washinde huko mpaka jioni hakikisha wanarudi hoi, kwa muda wa wiki 1 halafu wape nauli wao na dada yao waende kwao kupumzika, ni dharau moja konki na watajifunza

Usijilegeze mbele ya mkeo Sasa vaa uso wa mbuzi ukilegea utajuta ukoo wote utahamia hapo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom