Wageni wengine bwana du!

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,050
1,220
Nawasalimu!
Naomba nieleweke nyumba inayotembelewa ndo nyumba yenye baraka. Hivyo nisitafsiriwe kama mchoyo. Ipo hivi nimetembelewa na shemeji zangu wawili mmoja 15 na mwengine 17 hivi,japo nimeshangaa kwetu sio rahisi kutembelewa na shemeji kama dada yao hujamuoa kindoa,sasa kama tulivyo wengi maisha yetu mi naishi kwenye nyumba yenye vyumba vitatu ,kimoja ni stoo ya mpunga na mahindi nilihofia lock down,kwa hiyo natumia vyumba viwili kimoja w atoto na kilichobaki sisi.
Sasa kwa heshima nimeona niwahamishie w atoto sebuleni wao walale kwenye kitanda cha w atoto.
Mambo yaliyo nishangaza kwa ndugu hawa;kuangalia sinema zetu kutwa nzima hadi taarifa ya habari ya saa mbili usiku mpaka niwaombe zaidi ya mara moja ndo waniruhusu, hakuna anaenisalimia asubuhi tunatazama wakati mwingine Mimi huwasalimia,ajabu mmoja alimanusura akeshe kwenye tv bila kujali makelele pale Maana w atoto wamelala kwenye Kochi na kiufupi ni nyumba nzima , sasa kali ya mwaka dogo kagoma kushuka kutoka kiti (office chair)tulikuwa tukula nje kwenye kivuli ,nilipo jaribu kumwambia vipi dogo utakulaje uko juu hivyo kajibu "sili juu nakula chakula". Nikakaa kimyaa. Dogo kasogeza kiti juu ya jamvi. tukala hivyo hivyo.
Jamani sijui wengine mmewahi kuyapitia haya, kwa mbali natamani waondoke hata kesho. Adabu yao ipo chini sijui wamelelewaje?.N.a. dada yao anaangalia tu.
Nawasilisha
(copy &paste).
 
kama wametoka vijijini ushamba unachangia bt kama ni mjini basi kwao hamna mazingira kama yako hivo wavumilie tu.
 
Nimecheka sana.Ila pole.
Moja ya kitu huwa sipend na haitatokea kuzoea ni suala la kubadilishiswa utaratibu wa maisha nyumbani kwangu. Never.. mbal na wagen , ma hauz girl pia wana hiz tabia kisa tu ukiwakosoa wanatishia kuondoka.Kwangu nilikataa..

Mama mkwe wangu (ni mnyakyusa kweli kwel,ila mi wale wa mhin so sijui mambo kibao) alikuja home kuuguzwa .bwana wee nilivumilia ila nikasema noo.😂😂😂 ikabid anizoee tu.
 
Nawasalimu!
Naomba nieleweke nyumba inayotembelewa ndo nyumba yenye baraka. Hivyo nisitafsiriwe kama mchoyo. Ipo hivi nimetembelewa na shemeji zangu wawili mmoja 15 na mwengine 17 hivi,japo nimeshangaa kwetu sio rahisi kutembelewa na shemeji kama dada yao hujamuoa kindoa,sasa kama tulivyo wengi maisha yetu mi naishi kwenye nyumba yenye vyumba vitatu ,kimoja ni stoo ya mpunga na mahindi nilihofia lock down,kwa hiyo natumia vyumba viwili kimoja w atoto na kilichobaki sisi.
Sasa kwa heshima nimeona niwahamishie w atoto sebuleni wao walale kwenye kitanda cha w atoto.
Mambo yaliyo nishangaza kwa ndugu hawa;kuangalia sinema zetu kutwa nzima hadi taarifa ya habari ya saa mbili usiku mpaka niwaombe zaidi ya mara moja ndo waniruhusu, hakuna anaenisalimia asubuhi tunatazama wakati mwingine Mimi huwasalimia,ajabu mmoja alimanusura akeshe kwenye tv bila kujali makelele pale Maana w atoto wamelala kwenye Kochi na kiufupi ni nyumba nzima , sasa kali ya mwaka dogo kagoma kushuka kutoka kiti (office chair)tulikuwa tukula nje kwenye kivuli ,nilipo jaribu kumwambia vipi dogo utakulaje uko juu hivyo kajibu "sili juu nakula chakula". Nikakaa kimyaa. Dogo kasogeza kiti juu ya jamvi. tukala hivyo hivyo.
Jamani sijui wengine mmewahi kuyapitia haya, kwa mbali natamani waondoke hata kesho. Adabu yao ipo chini sijui wamelelewaje?.N.a. dada yao anaangalia tu.
Nawasilisha
(copy &paste).
Chomoa kadi king'amuzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom