Waganga wa jadi 10 wapelekwa Kigoma kupambana na Wachawi, DC aweka ngumu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460

Wananchi wa Kijiji cha Sunuka, Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wameshirikiana na Serikali ya Kijiji kuchukua Waganga wa Jadi zaidi ya 10 kutoka Sumbawanga ili kukagua wachawi waliomo ndani ya kijiji chao wakidai ndicho chanzo cha utitiri wa vifo vya vijana katika mazingira ya kutatanisha.

Baadhi wa Wananchi walikusanyika na kuandama barabarani wakiimba “Tumechoka na uchawi” huku wakisapoti kile kinachofanywa na Viongozi wao.

Hata hivyo operesheni hiyo imepingwa vikali na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dinah Mathamani ambaye amezuiwa kuingia kijijini hapo ikiwa yupo kinyume cha mpango huo.

DC Dinah Mathamani amesema “Tumejadili na viongozi kuhusu suala hili, wale wanaojiita Waganda wanatakiwa kuondoka katika wilaya yetu, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na viongozi wanaoshirikiana nao.

Chanzo: UFM
 
Naunga mkono uamuzi wa wanakijiji. Kwa kuwa Serikali yenu inajifanya kutoamini uchawi japo wanakesha kwa Sangoma kutafuta vyeo. Basi wananzengo acha wawasake wachawi wenyewe. Na huyo DC aoneshwe advertise kidogo. Ajikute uchi ofisini.
 
Cheki mtu mzima anasema eti kuna mtu anakuwa mamba!! Waamini uchawi ni watu wapumbavu zaidi duniani.
Uchawi upo ndugu ndio maana hata jeshini wanafundishwa dark arts. Hata askari waliokua wanapambana na majambazi ya Kahama na Kibondo walikua wanatumia dark arts Ili kuwamaliza bila hivyo hata ungerusha risasi ngapi humuuwi.
 
Ni matokeo ya ujinga na viongozi fisadi waganga njaa. Ni hila viongozi wa kijiji kutaka kula hela kiujanja. Ujinga ni taabu tupu. Huku wanazuka mapastor wezi, huku wanazuka waganga wezi..ni balaa kila upande kwa mwananchi.
 
Uchawi upo ndugu ndio maana hata jeshini wanafundishwa dark arts. Hata askari waliokua wanapambana na majambazi ya Kahama na Kibondo walikua wanatumia dark arts Ili kuwamaliza bila hivyo hata ungerusha risasi ngapi humuuwi.
Hakuna uchawi wa kuzuia risasi. Hayo ni matokeo ya ujinga. Yalianza huko kwa Kinjekitile. Na si Kinjekitile tu, Wahindi wekundu walikuwaga nao na mganga aliyewadanganya kuwa ana dawa wakipigwa risasi na wazungu hazitawadhuru. Na zaidi ni kuwa jeshi hupingq vikali imani za kishirikina. Maana nirahisi sana kudemoralize jeshi linaloamini uchawi.
 
Kawasaidie watokane na Ujinga
Hakuna uchawi wa kuzuia risasi. Hayo ni matokeo ya ujinga. Yalianza huko kwa Kinjekitile. Na si Kinjekitile tu, Wahindi wekundu walikuwaga nao na mganga aliyewadanganya kuwa ana dawa wakipigwa risasi na wazungu hazitawadhuru. Na zaidi ni kuwa jeshi hupingq vikali imani za kishirikina. Maana nirahisi sana kudemoralize jeshi linaloamini uchawi.
 
Cheki mtu mzima anasema eti kuna mtu anakuwa mamba!! Waamini uchawi ni watu wapumbavu zaidi duniani.
Mzungu akisema kwao hakuna uchawi,siyo kwamba na sumbawanga nako, hakuna uchawi.Viongozi wako wa selikali wachawi wakubwa na washirikina halafu wewe unasema hakuna uchawi? Hata biblia imeandika juu ya uchawi, pitia kisa cha Filauni na Musa
 
Wamuulize Ally Hapi atawasaidia
Naunga mkono uamuzi wa wanakijiji. Kwa kuwa Serikali yenu inajifanya kutoamini uchawi japo wanakesha kwa Sangoma kutafuta vyeo. Basi wananzengo acha wawasake wachawi wenyewe. Na huyo DC aoneshwe advertise kidogo. Ajikute uchi ofisini.
 
Mzungu akisema kwao hakuna uchawi,siyo kwamba na sumbawanga hakuna uchawi.Viongozi wako wa selikali wachawi wakubwa na washirikina halafu wewe unasema hakuna uchawi? Hata biblia imeandika juu ya uchawi, pitia kisa cha Filauni na Musa
Uchawi haupo uzunguni wala wapi. Kuwa kiongozi wa serikali haimaanishi huwezi kuwa mjinga.
 
Hakuna uchawi wa kuzuia risasi. Hayo ni matokeo ya ujinga. Yalianza huko kwa Kinjekitile. Na si Kinjekitile tu, Wahindi wekundu walikuwaga nao na mganga aliyewadanganya kuwa ana dawa wakipigwa risasi na wazungu hazitawadhuru. Na zaidi ni kuwa jeshi hupingq vikali imani za kishirikina. Maana nirahisi sana kudemoralize jeshi linaloamini uchawi.
twende kigoma this week nauli na malazi juu yako then kuna mtu namjua akupe hyo dawa endapo itakuwa uongo nakurudishia gharama zako zote za usafiri na malazi.

baada ya kufanyiwa utajaribiwa kwa kila silaha unayotaka wewe kuanzia wembe,pange,visu,shoka,risasi nk

dawa hiyo inaitwa kidono tembea ndugu dunia ina mengi mno usiyoyajua
 
Uchawi haupo uzunguni wala wapi. Kuwa kiongozi wa serikali haimaanishi huwezi kuwa mjinga.
ULaya na Marekani uchawi umepungua sana baada ya wachawi wengi kuuliwa.

Huku Afrika ni watu viazi kama wewe ndio mnasababisha hawa wachawi waendelee kutusumbua kwa kuwatetea kuwa uchawi hakuna.

Pia Kama mtu anaeamini uchawi ni mjinga au uchawi haupo kwanini nchi hii kuna sheria ya kudhibiti uchawi -Witchcraft Act?

Wewe kama hujawahi shuhudia uchawi piga kimya tu sababu sisi wengine tuna shuhuda nyingi tu za uchawi.
 
Back
Top Bottom