Wafungwa wa Gereza la Kyela washerekea Sikukuu kwa kupewa msaada na Wadau

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
Taasisi ya Vanessa Foundation imetoa msaada wa hali na mali kwa wafungwa wa Gereza la Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, wakati wa Sikukuu ya Krismasi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea nao pamoja na kuisaidia Serikali jukumu la kuhudumia wafungwa hao.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Vanessa Ngesyenge amesema kila msimu wa Krisimasi kwa kushirikiana na wadau wamekuwa wakitoa misaada ya vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa katika Gereza la Wanaume.

“Vanessa Foundation kila mwaka imeweka utaratibu wa kuwaona wafungwa na kutoa vitu kusherehekea nao sikukuu ya Christmass, tumechagua kulisaidia kundi hilo kwa sababu limesahaulika kwenye jamii,” amesema Ngesyenge.

52f0fbe1-afad-4908-9fbe-23e323ea3957.jpeg


Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkuu wa Magereza ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Inspekta wa Jeshi la Magereza, gereza la Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Eliasi Chamungwana amesema wamepatiwa msaada wa mafuta ya kupakaa, sabuni, maji, juisi na miswaki ambayo ilikuwa ni uhitaji mkubwa.

“Tunaishukuru Vanessa foundation kujitokeza kwa wingi kuwa faraja kwao na kuwafundisha upendo kwa wengine hasa jamii hii ya wafungwa ambao inaonekana kutengwa sana maana watu wengi wanafikiri maumivu waliosababishiwa na watu hao, ameiomba jamii kuendelea kutoa misaada kusaidia wafungwa hao.
 
Hao wangepelekewa MCHELE na Ndondo basi.

Ivo vi juice mbwembwe tu
 
Hitaji kubwa la mfungwa ni sabuni.
Tunawashukuru hao wadau waliopeleka walichojaliwa
 
Back
Top Bottom