Chatanda Kuchangia Mifuko 50 ya Saruji na Pesa Milioni Moja Gereza la Mbozi - Songwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

CHATANDA KUCHANGIA MIFUKO 50 YA CEMENT NA PESA MILIONI MOJA GEREZA LA MBOZI - SONGWE

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania Cde Mary Pius Chatanda( MCC) ameahidi kuchangia mifuko 50 ya cement na milioni Moja ya tiles Kwa ajili ya ujenzi wa jengo la matibabu katika gereza la Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe

Chatanda ametoa ahadi hiyo alipokuwa ametembelea gereza mala baada ya kupokea Taarifa ya uhitaji wa ukamilishwaji wa jengo tajwa kutoka Kwa askari wa magereza

Hayo yamefanyika wakati Chatanda alipokwenda kukabidhi vifaa mbalimbali Kwa lengo la kuwafariji wafungwa na mahabusu Kwa siku muhimu ya Wanawake Duniani

Aidha, Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amewatembelea Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Dkt. Samia SH iliyopo Namole - Halmashauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe na Kuwapa zawadi za Taulo za Kike zenye thamani ya Sh Milion 2.49

Vilevile, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda (MCC) akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Riziki Kingwande( MNEC ) wakiwa na Viongozi wa CCM na Viongozi wa Serikali Mkoa wa Songwe wameweza kutembelea Gereza la Mbozi na kutoa Msaada mbalimbali kwa wafungwa kwa ajili ya Kufariji Katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilayani Tunduma Mkoani Songwe.

WhatsApp Image 2024-03-09 at 18.23.46.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-09 at 18.23.46(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-09 at 18.23.47.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-09 at 18.23.48.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-09 at 18.23.48(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-09 at 16.18.07.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom