Wadau wa nishati ya umeme; Swali kwa TANESCO kuhusiana na mgao

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,736
2,085
Nawasalimu na kazi iendelee..

Kuna karatiba fulani ka mgao wa umeme maeneo ya wilayani umeme huwa unakatwa jioni kuanzia saa 12 na kurudi either mid night au usiku wa manane.Sijajua sehemu nyingine Kama iko hivo.

Sasa ninavyofahamu sehemu nyingine wilayani hazina heavy duties nyakati za usiku.Hakuna magiant industry yanayofanya kazi nyakati za usiku.

Hata hivi viwanda vya wajasiriamali wadogo usiku huwa wanaenda kulala mfano hawa welders, carpenters, filter &tuners na wengine wengine nyakati za usiku wengi hawafanyi kazi.

Hata ofisi nyingi za serikali za umma na sector binafsi zinakuwa off usiku.
Kwa hiyo kifupi sehemu za wilayani usiku huwa hakuna mzigo mzito wa kazi unapigwa.

Sasa haka karatiba ka kukata umeme jioni au usiku kanakuwaje iii!?

Kapoje kapoje haka karatiba

Ina maana Hali ni mbaya Sana kuliko tunavyoona?
Haka karatiba kanakerakera kidogo.

Kumbuka hapa nazungumzia wilayani.Mwenye ufahamu na hili Karibu.

Alamsiki.
 
Mgao siyo wa Wilayani wala Mkoani ni wa kiTaifa.
Anayeratibu mgao, hajali hapa pakoje, kazi yake ni kukata tu.
Mambo mengine na shuhuli zenu mtajijua wenyewe.
 
Kumbuka umeme wote ni katika grid ya taifa. Ukinyimwa wewe huko waletwa kwetu tunakopiga kelele zaidi. Nyie endeleeni kukaa kimya mama anaupiga mwingi.

Habari ndiyo hiyo.
 
Load demand inapaswa kuwa kigezo kikubwa, kuna maeneo mengi ambayo ni makazi ya kawaida, inapofika saa 12 mpaka saa 1 jioni ndio load inaongezeka sana.

Raia wamerudi majumbani, wanaochemsha maji, wanaowasha heaters, AC, fans, cookers, etc.

Maeneo ya viwandani ndo wanapaswa kupigwa mgao wa kutosha kwakuwa wanao uwezo wa kuzalisha umeme wao ingawa watajifanya gharama za uzalishaji kupanda na kutaka kupandisha bei za bidhaa ingawa ukweli ni kwamba gharama hizo zilishawekwa kwenye hesabu za ushalishaji tayari.

Kwa akili hizi tunazoendelea nazo, mgao utaisha generation ya 16 kutoka sasa!
 
Naona jamaa ambaye yupo control amesizia maana Leo tarehe 16th tangia subuhi haja fanya mambo yake huku niliko naona bwawa limeaza kujaa jaa
 
Naona jamaa ambaye yupo control amesizia maana Leo tarehe 16th tangia subuhi haja fanya mambo yake huku niliko naona bwawa limeaza kujaa jaa
Ndogo maana nasema usiku mgao wangepotezea tu.
 
Hapa nilipo nina wiki sasa umeme haujakatika nadhani tumesahaulika ama tatizo limeanza kupungua.
 
Back
Top Bottom