Sasa hivi TANESCO hawazingatii tena ratiba ya mgao wa umeme

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Jamhuri ya Kenya iliingia complete power blackout 100% kwa siku 7, huku mafuta pia yakiwa yamekaushwa akiba ya taifa.

Kilichowasaidia ni Raila kutoa 3 days ultimatum umeme urudi na mafuta yawepo vinginevyo wanarudi barabarani.

Akaungwa mkono na wafanyabiashara pia ambao walikuwa wanaathirika pakubwa.

Ndani ya siku 2 za ultimatum umeme ulirejea nchi nzima.

Sasa hivi TANESCO hawazingatii tena ratiba ya mgao wa umeme. Kuna kata washa kata washa kwa juma zima.

Nishati zote 3 zinazobeba hatima ya taifa zimeathiriwa na kirusi cha siasa e.g. umeme, gesi na mafuta.

Zote hizi zinahusika na kuratibu uchumi na maisha ya watu ikiwemo hifadhi ya ikolojia (kusalimisha uoto wa miti).

Kwa TANESCO, mvua ni laana jua ni laana. Haijulikani majira gani ni baraka (yanawezesha uzalishaji na ugavi) kwa TANESCO.

TANESCO imefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ya hivi karibuni kwenye wizara ya nishati kukosa tija na mantiki.
 
Back
Top Bottom