Wadada, Mkisalimiwa Jibuni Salaam, Sio Kila Salaam Ina Ubaya Ndani Yake.

Nakumbuka mwaka Jana niliwahi msalimia mda mmoja njiani 'mambo dada angu' matokeo yake akanifyonya!! Halafu akanambia, "kawazoee hao hao Malaya uliowazoea"
Nikabaki najiuliza, kosa langu hapo ni lipi, Kuna mama mmoja alikuwa ni rafiki yake mama yangu, alikuja nyumbani, nikatambulishwa pale, yule mama akanambia "kama utaweza naomba nikupeleke nyumbani ukawe unanifundishia mwanangu"
Kweli, siku ya kwanza nimefika nikakakuta kavulana ka darasa la sita nikakafundisha, siku iliyofuata wakati namfundisha yule mtoto, yule mdada akaingia ndani, kumbe ni dada wa huyo mwanafunzi ninayemfundisha, mama yake akanitambulisha kwake!! Hiyo aibu iliyomjaa siku iyo bhana!! Nyie acheni tu!! Na Kwa hasira nilizonazo sikuwahi kuongea nae mpaka siku namaliza huo mkataba!! Ingawaje alikuwa ananipa salamu, ila namnyamazia tu!!

Sasa hebu imagine mkuu, unamsalimia mtu anakutukana na kukusonya hii ni tabia njema kweli...?

Sio utu hata kidogo ningekuwa ni mimi ningemwambia mama yake hakuna tuition mpaka huyu mwanao aniombe radhi kwa kunipigia magoti ndio tuendelee na masomo, laa sivyo masomo yangeisha siku hiyo hiyo aisee.
 
Kuna watu wengi tunapishana nao mitaani wana magonjwa ya akili. Magonjwa ya akili yako katika viwango tofauti tofauti.
Kuringa nako ni dalili mojawapo ya ugonjwa wa akili.

Unachosema kinaweza kuwa kweli kiongozi imagine unamsalimia mtu halafu baada ya kukujibu anakutukana, hivi inaingia akilini kweli...?
 
Nilichoandika sio mawazo,ni kitu kipo...mimi ni wa kike,nina marafiki wa kike wenye hizo tabia na wananipa hiyo sababu

Ninae rafiki hakubali salamu ya mwanaume asiye na gari
Kwake yeye mwanaume mwenye gari ndio mwenye haki ya kuongea nae

Ni ulimbukeni tu umemjaa angekuwa sio limbukeni asingekuwa hivyo.
 
Huyo rafiki yako ana dalili mojawapo za ugonjwa wa akili. Mpelekeni kwa mtaalamu wa magonjwa ya akili kabla hamjachelewa!

Mkuu umenifanya nimecheka kwa sauti sana aisee...!

Daaaaah hawa dada zetu wana matatizo sana na hawajijui kuwa wana matatizo vichwani mwao.
 
Kuuguza kunatia mawazo, yamkini hata hiyo salamu yako hakuisikia kwasababu ya kujawa na mawazo mengi hasa ukizingatia kuwa alikuwa amechelewa muda wa kuingia kumuona mgonjwa wake. Huyo dada alistahili huruma na sio lawama!
 
kumbe nimeusemea 💓....basi rowin anapenda kusalimia sana anapopishana nao....anajihisi ni mmojawao....vizuri salam iambatane na tabasamu...isipojibiwa basi atakuwa mgonjwa, kama mdau hapo juu alivyowakilisha...;)
🙃

Wow umenifanya nikupende bure my dear.

So lovely...!
 
Salaam/Shalom.

Kuna hili suala huwa linanishangaza sana, utakuta unamsalimia mtu halafu matokeo yake huyo unayemsalimia utakuta anakuangalia tu.

Huwa najiuliza sana hili swali, hivi mkijibu salaam huwa mnapungukiwa na kitu gani dada zangu...?

Leo nilikuwa Mount Meru Hospital kwa ajili ya kupima COVID 19 coz kuna kasafari kidogo cha nje, basi nikasema hebu ngoja nitoke nje ya geti nikanunue maji ya kunywa then nirudi ndani na muda wa kuona wagonjwa ulikuwa umeshaisha na askari akawa anazuia watu wasiingie.

Basi wakati natoka nje nikapishana na mdada mmoja mweupeeee anaingia ndani kumuona mgonjwa wake, nikamsalimia yule dada akawa ananiangalia tu, basi nikapishana nae nikanunua maji nikawa narudi ndani.

Nafika getini nikamkuta yule mdada amezuiwa kuingia ndani kwa kuwa muda wa kuona wagonjwa ulishaisha, basi nilivyofika getini askari akaniambia MKUU INGIA INGIA nikapita zangu nikamuacha yule mdada anamsihi, anambembeleza na kumuomba sana askari wa getini amruhusu aingie ndani kumuona mgonjwa wake, lakini bila ya mafanikio hakuweza kuingia ndani.

Ningeweza kumwambia tu askari MRUHUSU AINGIE na askari asingeuliza mara 2, ila unaanzaje kumuombea msaada mtu ambaye hata salaam yako ameshindwa kujibu akabaki anakuangalia tu...?

Matokeo yake ikabidi arudi nyumbani kama alivyokuja. Hivi, mnaposalimiwa then mkajibu salaam huwa mnapungukiwa na kitu gani dada zangu...?

Badilikeni aisee sio kila salaam ina ubaya ndani yake salaam nyingine zina baraka ndani yake, hivyo msiwe wenye kujikosesha baraka wenyewe kwa kushindwa kujibu kitu kidogo tu dada zangu. SALAAM.

NAWASILISHA.
Tumia hii formula
1.usimsalimie mwanamke ambaye humjui njiani,wala kumuongelesha.
2.salimia pale tu unapoenda sehemu na ni lazima usalimie,dukani,ofisini,unashida,umeitwa,umemuita mtu etc
 
umeeleweka sana....
Moja ya tabia yangu ndio hii naweza kutembea nisimsalimie mwanamke lkn mwanaume ata kusimama kwa ajir ya salam naweza ,ata sehem za huduma sana sana hiz za madukan itokee tu sina jinc ndio naenda kwa watoa huduma wa kike sio kama nawachukia au siwapendi ila wanawake zalau zimezd asa ukiwa na muonekano au hali fulan ambayo wanaichukulia si nzur
 
Moja ya tabia yangu ndio hii naweza kutembea nisimsalimie mwanamke lkn mwanaume ata kusimama kwa ajir ya salam naweza ,ata sehem za huduma sana sana hiz za madukan itokee tu sina jinc ndio naenda kwa watoa huduma wa kike sio kama nawachukia au siwapendi ila wanawake zalau zimezd asa ukiwa na muonekano au hali fulan ambayo wanaichukulia si nzur
basi nikajua unakimbia washirikina.....kumbe dharau tu...
ubinadamu wetu ndio unatufanya tuhukumu mtu kwa mwenokano wa nje...wengi wetu tunafanya bila kujijua (sijui ndio dharau kwa yule asiyevutia? )...na wale wanaovutia sijui tutasemaje? ila ni hukumu ile ile....
ni ngumu kuepuka....tuvumiliane tu...😉🙃
 
Mkuu huenda hakusikia, sio wote wana tabia hizo.

Au labda alikua na mawazo ya mgonjwa wake na huo mda alofika akijua huenda kachelewa na mgonjwa wake hatopata mlo wa mchana wa siku hiyo.

Kwa mimi naona ulimhukumu bure dada wa watu, na je ulimsalimia zaidi ya mara moja?? Kama sivyo basi we jamaa una kujiskia kwa kijinga na unapaswa kupuuzwa kwa hizi lawama unazomtupia bidada!!
 
Back
Top Bottom