Wadada, Mkisalimiwa Jibuni Salaam, Sio Kila Salaam Ina Ubaya Ndani Yake.

Niache Nteseke

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
1,959
2,177
Salaam/Shalom.

Kuna hili suala huwa linanishangaza sana, utakuta unamsalimia mtu halafu matokeo yake huyo unayemsalimia utakuta anakuangalia tu.

Huwa najiuliza sana hili swali, hivi mkijibu salaam huwa mnapungukiwa na kitu gani dada zangu...?

Leo nilikuwa Mount Meru Hospital kwa ajili ya kupima COVID 19 coz kuna kasafari kidogo cha nje, basi nikasema hebu ngoja nitoke nje ya geti nikanunue maji ya kunywa then nirudi ndani na muda wa kuona wagonjwa ulikuwa umeshaisha na askari akawa anazuia watu wasiingie.

Basi wakati natoka nje nikapishana na mdada mmoja mweupeeee anaingia ndani kumuona mgonjwa wake, nikamsalimia yule dada akawa ananiangalia tu, basi nikapishana nae nikanunua maji nikawa narudi ndani.

Nafika getini nikamkuta yule mdada amezuiwa kuingia ndani kwa kuwa muda wa kuona wagonjwa ulishaisha, basi nilivyofika getini askari akaniambia MKUU INGIA INGIA nikapita zangu nikamuacha yule mdada anamsihi, anambembeleza na kumuomba sana askari wa getini amruhusu aingie ndani kumuona mgonjwa wake, lakini bila ya mafanikio hakuweza kuingia ndani.

Ningeweza kumwambia tu askari MRUHUSU AINGIE na askari asingeuliza mara 2, ila unaanzaje kumuombea msaada mtu ambaye hata salaam yako ameshindwa kujibu akabaki anakuangalia tu...?

Matokeo yake ikabidi arudi nyumbani kama alivyokuja. Hivi, mnaposalimiwa then mkajibu salaam huwa mnapungukiwa na kitu gani dada zangu...?

Badilikeni aisee sio kila salaam ina ubaya ndani yake salaam nyingine zina baraka ndani yake, hivyo msiwe wenye kujikosesha baraka wenyewe kwa kushindwa kujibu kitu kidogo tu dada zangu. SALAAM.

NAWASILISHA.
 
Uko kitengo gani hapo Mount Meru hospital hata ukimwambia mlinzi aruhusu mtu kuingia asiulize mara mbili?

BTW mara nyingi ukiona unasalimia mdada na hakuitikii ujue una muonekano wa hovyo

Joanah, umenifanya nimecheka sana and am still laughing. It means salaam ina masharti au mipaka ya kutolewa au kupokelewa Joan...?

Natumai unaishi na watu wenye mionekano ya hovyo kuliko unavyodhania, wengine ndugu zako, rafiki zako, watu wanaokuzunguka baadhi yao utakuta wana mionekano ya hovyo tu, unataka kusema wakikusalimia hauwaitikii...?
 
Uko kitengo gani hapo Mount Meru hospital hata ukimwambia mlinzi aruhusu mtu kuingia asiulize mara mbili?

BTW mara nyingi ukiona unasalimia mdada na hakuitikii ujue una muonekano wa hovyo
Ndy maana Yule dada pale dukani nikimsalimia huwa ananiangalia km nimepaka kinyesi usoni

Kumbe muonekano unachangia ili kujibiwa salamu ya mtoto wa kike

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Ndy maana Yule dada pale dukani nikimsalimia huwa ananiangalia km nimepaka kinyesi usoni


Pole sana kiongozi, actually sjui kwa nini wanakuwa na tabia hii, it doesn't value anything in their life instead, inapoteza Baraka mkuu...!

Kumbe muonekano unachangia ili kujibiwa salamu ya mtoto wa kike

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app

Ndio maana nikamuuliza Joanah hilo swali lakini nashangaa mpaka sasa hajanijibu mkuu...!
 
Mkuu hawa viumbe wanakera Sana,
Juzi kati nilikutana na dada mmoja kijijini kwetu ni miaka mingi sijaonana nae kwani alikuwa udsm anasoma

Basi bwana nikamuita kwa bashasha maana ni jirani yangu,,aliishia kunishusha tu duuh sikuamini aisee,,

Malipo apa apa duniani

#Jana kaja kuomba namba ya dada angu anatafuta connection nikamwambia ww hapa uondoke na ukiendelea kukaa napiga kelele unanishawishi tufanye ngono#

Kama alikaa tena
 
Binafsi ni afadhali Mtu anipite bila kunisalimia kuliko nimsalimie na asipokee salamu yangu !!

Pole sana Mkuu Niache Nteseke ila wadada wengi ni watu wa jinsi hiyo nadhani wanafikiri wasipoitikia salamu TOKA kwa ME basi hadhi yao inakuwa Bab-K....It's a stupidity behavior !!
 
BTW mara nyingi ukiona unasalimia mdada na hakuitikii ujue una muonekano wa hovyo


Mtu mwenye muonekano wa hovyo anafananaje!ni tabia za dharau na kimaskini kutoitika salamu ya mtu usiyemjua au kwa sababu siyo nadhifu,wakati mwengine anataka kukufahamisha uelekeo unaoelekea kwa muda huo siyo kuzuri rudi au labda umedondosha kitu.

Dunia hii siyo ya kuishi kwa maringo unapojiona wewe mzuri kuna sehemu ukiingia wanakuona kinyago tu ila huwa wanakusikiliza kwa sababu ni binadamu mwenzao!
 
Back
Top Bottom