Baba Joseph17
JF-Expert Member
- Jul 15, 2013
- 9,516
- 9,809
Ngoja wawakomeshe hao jamaa zako kwani walijitakia wenyewe, haiwezekani umtongoze binti kwa madaha ya kujifanya wewe ni ATM, unamkuta kijana anamtongoza binti kabla hajakubaliwa tu kaishaanza kumpeleka out za gharama, mara Mlimani city je siku akikukubalia si ndiyo utampeleka Kempisky! Nawapa bigup wasichana mnao wakomesha wahawa vijana
Kuna rafiki zangu 5 na work mates kama watatu wameachana na wachumba zao kisa wanapenda vitu vya gharama kubwa kuliko uhalisia wa maisha. Wanalalamika kwamba hao WACHUMBA matumizi ya kuwahudumia wao tu hata mwisho wa mwezi haufiki wanajikuta hawana kitu. Kuna wengine mpaka hata kukutana wanataka hotelini na jamaa anakuwa amepanga nyumba ambayo anaishi peke yake.
Kuna mwingine mpaka akawa anamshauri jamaa awe anafanya shopping ya vyakula vya kutumia super market. Wakiongelea kuhusu kuwekeza hawawaelewi, kuna mmoja ndo alikata mawasiliano kisa jamaa kanunua kiwanja na ye alikuwa anahitaji hela ili anunue vitu vyake. Nachojiuliza, ni kwanini siku hizi mdada ambaye unategemea kuwa mtaishi pamoja anakuwa mchunaji kuliko hata madada poa? Siku hizi hamna mawazo ya kujenga familia na hao wakaka mnaokuwa nao? why? Najua wapo wenye hela zao za kuhonga na kustarehe sana.! Cc@snowhite, Nyamayao Badili tabia @aspirin na wengineo wenye familia zao, enzi zenu za kuwinda na kuwindwa mambo yalikuwaje.?