Wachungaji na Mashehe wanafiki! - Mmevuna mlichopanda!

Serikali inajidanganya katika suala hili la kodi kwa mashirika ya kidini, yawe ya Kikristo ,Kiislamu au Bohora.
Inaelekea Serikali haijafanya utafiti katika hili na italijutia katika muda si mrefu ujao.
Viongozi wetu wengi wamesoma BURE katika hizi shule. Sasa tujiulize biashara iliyopo pale.
Kikwete kasoma nafikiri Lugoba Seminary,Nyerere ndo kabisa ikiwa ni pamoja na kufundisha shule ya Pugu Seminary.Siyo siri kuwa watakao athirika zaidi na msimamo huu wa kodi ni Kanisa la Katoliki ambalo lina miradi mingi zaidi ya kijamii.
Kwa hili basi serikali inbidi ikubali ya fuatayo-
1)Kanisa libadili msimamo wake wa jadi wa kutoa huduma za kijamii kwa bei nafuu na kufanya kibiashara
2)Kufunga huduma zote zisizoweza kujiendesha kibiashara
3)Hospitali kama KCMC,Bugando sasa ziwe private
4)Shule kama St Francis-Mbeya, Mazinde Juu,Kifungilo Girls,St Marian Bagamoyo ziwe private schools na zitoze ada istahiliyo kama hizi "International Schools " za Dar es salaam

Ni wazi kuwa msimamo wa madhebu yote ya dini ni kinyume na kufanya mambo kibiashara hivyo ufinyu wa mawazo ya kutakiwa kufanya shughuli zake kibiashara utaonekana muda si mrefu
Unategemea Mkulo alivyo kilaza atazingatia yote hayo???
ila hapa nahisi pia kuna kitu nyuma ya pazia na sasa wanajaribu kublow the horn
 
1. Huduma za jamii wajibu wa kwanza ni serikali!

2. Uganda na Kenya dini zote wanalipa Kodi kama wananchi wengine..kwa nini hapa Tz wasamehewe??

3. Maaskofu wanaishi maisha wa anasa/kifahari na wana mashangingi kama ya mawaziri..je kwa nini wasamehewe kodi??

Naona serikali imechelewa..zoezi hili Tz lingeanza mda mrefu!
 
kwa upande wangu option ni C

c. Wafunge baadhi ya huduma zao ambazo ni ngumu kujiendesha na kuziunganisha baadhi ya huduma zao kama wafanyavyavyo wafanyabiashara wengine na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.

watafute mbinu zingine za kuzalisha hela zao either by donations in the mosques and churches after all si wanajidai wanajali na wanakea kwa njia ya dini, sijui huruma au morally obliged then they should continue on the same line without any spececial favours from the government waumini wanao jali sana izo cause zao ndio wachangie mungu atawalipa baadae anyway, serikali wacha ikusanye kodi zake kialali.
 
Kwa maoni yangu hii ni hatua nzuri sana. I like it. Huu ni mrija ambao ulikuwa unatumiwa sana na wakwepa kodi. Vikija vitu vinaagizwa na kanisa so and so halafu mle ndani imejaa mizigo ya wafanya biashara. Hapana, dini zimepoteza uaminifu wake na lazima serikali izitoze kodi kumpunguzia mzigo wa kodi mlipa kodi wa kawaida.

Fikiria kwa mfanyakazi anayekatwa karibu asilimia 30 ya mshahara wake kama PAYE. Halafu mtu huyo huyo kila bidhaa anayonunua (kwa hela iliyobaki) analipa si chini ya asilimia 40 kama kodi za serikali.

Michango makanisani na misikitini (Zaka, harambee mbali mbali, sadaka, ujenzi wa kanisa, n.k) ni mzigo ambao umemwelemea mtu yule yule anayelipa kodi.

Taasisi za kidini zinasitahiri kulipa kodi kwa sababu kwanza zinatumiwa na wakwepa kodi wengi siku hizi na vile vile zimethibitisha kuwa zina matumizi mengi na makubwa ambayo si huduma. Mara nyingi huduma zimekuwa zikitumiwa kama kisingizio tu. Ni kweli yapo makanisa makubwa kama kanisa katoliki lenye shule nyingi, hospitali hadi vyuo vikuu. Lakini wanastahili kulipa kodi.
 
Hivi nani kasema hawa jamaa hawafanyi biashara, fuatilia ada za shule zao halafu linganisha na za serikali au watu binafsi.

Mathalani mkoani Mbeya; St Frances anda ni zaidi ya sh. 1.5m na ndio maana hivi sasa inachukua zaidi kutoka nje ya mkoa hususani Dar es Salaam kuliko mkoani humo, kwa shule za serikali ni 40,000 na watu binafsi ni kati ya laki nane na milioni moja.

Wacha walipe tu kwanza wao ndio waliowapotosha wananchi kwamba JK ni chaguo la Mungu
 
Kwani hiyo kodi serikali imeanza kukusanya leo wingi wa mapato haujawahi hata siku moja kureflect maisha ya mtanzania maskini hii ni nchi inayoongonzwa na takwimu bila kulinganisha na upandaji wa maisha ya mtu wa kawaida. watuambie wanapoteza ngapi kwa kutoa hiyo misamaha? na wakifuta misamaha hayo makusanyo yatamsaidiaje mtanzania wa kawaida, anayetembea kilometa kumi ili mkewe akajifungue salama kwenye hospital ya mashirika ya kidini?unaposema wachungaji/mashehe/mapadri wanaishi maisha ya anasa na kuonekana kwa magari ya kifahari huo ni mtazamo wa kimaskini sana.Lipi bora hawa mawaziri wetu mafisadi wanaohudumiwa na hela ya mlipa kodi, au maaskofu wanaotembelea magari ya misaada na kazi zao zinaweza kuwa quantified?
 
Hizi taasisi za dini zinazotaka kujiingiza katika mambo ya elimu ya uraia na mambo mengine poa tu kuzipiga kodi.Kuwe na guidelines fulani zikivunjwa taasisi inapoteza status yake kama taasisi ya dini isiyolipa kodi.Hatuwezi kuwa na kitu blanket tu kwamba "taasisi za kidini hazilipi kodi" au "zitalipa kodi", kwa sababu the former will open a door to abuse, the later has potential to for example, penalize some genuinely church oriented social work.Kanisa katoliki lina studio ya muziki pale Don Bosco, studio ile inafanya biashara, watu wa bendi na vikundi mbalimbali wanaenda kurekodi nyimbo pale.Hii ni biashara straight up na ni lazima ilipiwe kodi, kutolipia kodi mapato haya ni ku abuse status ya kanisa kama tax exempt. Hapo hapo Don Bosco kuna kituo cha vijana, wanakuja vijana kucheza soka baketball na mambo mengine, hii ni genuine social work na vifaa vya kwenye program kama hii kuvilipia kodi si halali kwa sababu si vya biashara.Kwa hiyo tunahitaji guidelines ya kuonyesha nini kitalipiwa kodi na nini hakilipiwi, sio some blanket bureaucratic decree from ten thousand feet above the ground.

Zaidi ya hapo serikali yetu inafanya mambo bila hesabu.Kwa kutaka kuhodhi huduma za misaada, serikali hii ambayo mpaka sasa hivi ina obligations nyingi sana na kuendeshwa kwa misaada, inajifunga nira isiyoweza kuibeba.Watakachokipata kwa kodi kitakuwa kidogo zaidi ya misaada ambayo taasisi za kidini zitatoa kwa wananchi.

Kwa hiyo the only way this would make sense is if the government cares more about the little tax that it would gain than the significant aid that the people of Tanzania will gain.

Kama serikali yetu inataka wananchi wa Tanzania wakose msaada wa ng'ombe ili kuhakikisha tu kuwa serikali inapata kodi ya kuku, nitakuwa siielewi kama inaweka maslahi ya wananchi mbele.

Halafu kama hivi ndivyo tunavyoenda basi serikali yetu inaonyesha haielewi neither ujamaa nor soko huria, inaonekana sasa tunaelea tu bora liende, what am I talking about "sasa" wakati Kolimba alishasema kitambo chama tawala hakina dira wala muelekeo. He is still being vinicated.
 
Last edited:
Watz ndugu zangu: Kenya na Uganda hii misamaha ya kodi ishafutwa siku nyingi..tujue pia we are heading towards EAF!

Kwa nini hapa kwetu inaonekana haiwezekani??

Walipe tu kodi..kama watu wengine!
 
Jukumu ya huduma za jamii ni la serikali!

Serikali wanaweza kuwajibishwa ktk kura kila miaka 5 kama hakuna hizi huduma au kama ni mbovu!

Je mashirika ya Dini wanawajibika kwa nani kama huduma zinakuwa mbovu??

Nchi kama China, Norway na Cuba..watoto wote au 95% kusoma shule za serikali na hata watoto wa mawaziri pia husoma huko2!

Pia tiba..hospitali nzuri inabidi ziwe za serikali..kwa vile serikali hukusanya kodi!

Tungeiwajibisha serikali ifungue Chuo Kikuu kila Mkoa!

Kwa nini serikali iwajibike kusamehe kodi watu binafsi??? Why???
 
Mimi naungana nawe mmkjj. Wacha wakome na unafiki wao. Walisema ni chaguo la Mungu sasa kelele za nini? Tena walivyokuwa wajinga baadhi wanayoosha vidole kwa Mkulo kwani kuna la Mkulo na la Mkuu wa kaya? lao si moja?
Walikuwa hawajui yaliyo mbele yao maskini! Na kwa kweli baada ya kusikia kelele za viongozi wa dini I knew what will follow, lakini walivyokuwa na macho ya kuangalia karibu wao hawakuona. Wamechezeshwa mchezo.
Kweli taasisi za dini zimekuwa mkombozi katika maeneo mengi kuliko hata serikali yenyewe. Wa kuhumia ni nani? Ni serikali yenyewe + wadanganyika wenyewe.
Nimeshuhudia kwa hivi karibuni hospitali za dini zikipata shida hatakulipa mishahara minono maana walishindwa kuendesha shughuli kibiashara kwa kuonea huruma jamii. Hospitali za misheni wana huruma kama huna pesa wakati hospitali za serikali hawawezi kukutibu kama huna pesa. Tena hii ni official sio propaganda.
Hivi serikali imeona misamaha ya kodi kwa taasisi hizi za dini ni mikubwa kulinganisha sawa na misamaha waliokuwa kiitoa kwa wachimba madini kwenye mafuta? wameona ni sawa na misamaha ya kodi wanayotoa kwa mashirika ya simu?
Mimi bado najua kuna kundi lengwa hapa katika mkakati huu. Mwenye macho aambiwi ona. Si muda mwingi tutaona kilichokusudiwa.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika. Tunusuru na viongozi makanjanja.
 
1. Huduma za jamii wajibu wa kwanza ni serikali!

2. Uganda na Kenya dini zote wanalipa Kodi kama wananchi wengine..kwa nini hapa Tz wasamehewe??

3. Maaskofu wanaishi maisha wa anasa/kifahari na wana mashangingi kama ya mawaziri..je kwa nini wasamehewe kodi??

Naona serikali imechelewa..zoezi hili Tz lingeanza mda mrefu!

Mkuu, ukisema ni wajibu wa serikali kutoa huduma you are theoretically correct,

Lakini practically, I wish ungetembelea vijijino huko uone jinsi hizi taasisi za dini, wasilamu kwa wakristo, zinavookoa jahazi pale ambapo serikali haiwezi, na nachelea kusema ni kwa sehemu kubwa tu ya nchi hii!

Ningeomba mwenye data za idadi za shule, huspitali etc za taasisi za dini azilete hapa

Alternatively, nawashauri viongozi wa makanisa/misikiti wadai shule na hospitali zilizotaifishwa na serikali miaka ya 60 kwa jina la ujamaa...ndio!....msinitolee macho, si tupo kwenye ubepari sasa hivi? ni wapi tunafuata sera ya azimio la arusha?
 
Serikali inachofanya ni kupunguza nguvu zao na pia baada ya kusikia kelele zimekuwa nyingi sana juu ya masuala ya ufisadi!! kaka yangu Mzee mwanakijiji ukitaka kupata msimamo mzuri juu ya hili jaribu kumuuliza Askofu Mokiwa ambaye mara nyingi amekuwa ni mtu radical sana kwa serikani je sio wengine ambao mara nyingi wamekuwa waoga sana na wanafiki wakubwa, Mimi siwezi kushangaa kwa serikali kufanya hivyo wakati kuna mpango wa kufanya makanisa yaache kushabikia serikali na siasa ambayo kanisa Katoliki nimesema kuwa nitaanza kutoa elimu ya uraia kwa wahumini wake,kwa Mujibu wa chanzo kimoja anasema kuwa Mokiwa alisema kuwa Serikani inaongozwa na watu wanakumbatia ushetani ndio maana wanawafutia hata hizo Kodi?? Je wanasema juu ya hilo?? Mchango wa Hospitali hizi ni mkubwa sana hata kule Bulongwa wanajua hivi.
 
Mkuu, ukisema ni wajibu wa serikali kutoa huduma you are theoretically correct,

Lakini practically, I wish ungetembelea vijijino huko uone jinsi hizi taasisi za dini, wasilamu kwa wakristo, zinavookoa jahazi pale ambapo serikali haiwezi, na nachelea kusema ni kwa sehemu kubwa tu ya nchi hii!
Si hao walioko kwenye serikali ndio wanajitapa kikla siku kuwa wametekeleza ilani kwa kiasi kikubwa? Ina maana hayo mapungufu hawayaoni?
Hawa wameshajisahau kwa sababu kuna watu wengine (kama hayo mashirika ya dini) wanafukia mashimo huko vijijini badala yao
 
Viongozi wa dini wawe wajasiri kwa hili. Wasikubali kutumiwa na serikali kujipatia umaarufu isio ustahili! Katika kuonyesha wako serious - wafunge huduma zote za taasisi za dini hata kwa mwezi mmoja tu (najua watu watakufa kwa kukosa huduma - labda including me). Lakini nasema wafunge - hiyo itawatoa ujinga hata wananchi wanaodhani nchi hii bado iko chini ya Nyerere! Kama taasisi za dini zitafanya hivi - basi move ya serikali itakuwa ilikuwa ni 'a blessing is disguise'. Naamini watanzania wote (mpaka wasonjo) watajua maana ya kupiga kura na kuwa hata mtu wanayempigia kura ana matter!


Kwakukusaidia ndugu yangu.. Taasisi za kidini hasa Katoliki (sijui sana kuhusu nyingine).. intention yao nikutoa huduma za kiroho na afya kwa jamii.. kusaidia binadamu awe tajiri au maskini.. ili mradi anahitaji msaada.. sasa wakigoma kutoa huduma kwasababu serikali imeamua kutoza kod huduma wanazotoa kwa jamii unafikiri watakuwa na tofauti gani na Hao serikali... wote watakuwa sawa.. malengo ya dini ni zaidi ya serikali.. si dhani kama serikali wanaweza kuwateteresha.. hizi dini nyingine zimedunda (survive persecution) kwa miaka 1000 mpaka 2000 sasa from serikali na uongozi ambao ulikuwa 100 times crue and inhuman... unaafikiri serikaliya tanzania inauwezo huo..
 
Tatizo mi naona sio Dini.. mi naona serikali vita wanayotaka kuanza towards viongozi wa dini kwasababu zozote zile wanazo ona wao sawa.. hiyo vita ni towards dini tena.. kwahiyo hapmserikali inaanzisha mgogoro na dini.. kwasababu hawa viongozi wa dini ni watu wakupita wanai represent dini... Sikatai kama katika viongozi wa dini kuna wegine ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo.. kwahiyo ni muhiu serikali ikatafakari intenntion zake..
kwasababu unajua kabisa usianzishe bif na dini.. Dini is a single most strong institution na it is very dengarous ukiichezea.. history inatufundisha if anything binadamu akipewa achague na dini.. atachagua dini.. sasa seikali hipo tayari kupima kama yenyewe na dini nani zaidi????
 
I have been always in support of KULIPA KODI...... however......
Tujiulize in the first place kwanini hizi taasisi za kidini zilipewa misamaha ya kodi...what was the rationale............
na sasa serikali kuondoa kodi what is the rationale..............

Hizi taasisi za kidini inatakiwa ziwe audited/assessed na iangaliwe ni shughuli zipi wazifanyazo zilipiwe kodi na zipi zisamehewe.....mfano zile shughuli ambazo ni huduma kwa jamii hospitali and the like.....serikali should think again....zile za kibiashara mfano radio stations and the like....zilipe kodi

Serikali itoe muongozo kwenye hilo ili kusitokee kutokuelewa............

Serikali pia lazima ikumbuke kuwa si kila biashara ifanyazo hizo taasisi ni kwa ajili ya manufaa kibiashara............inawezekana kabisa kuwa charge wanazotoza ni ili kugharamia shughuli za uendeshaji wa hizo shughuli.........na ndio maana hapo mwanzi nimesema hizo taasisi ziwe audited kujua what is what
 
Si hao walioko kwenye serikali ndio wanajitapa kikla siku kuwa wametekeleza ilani kwa kiasi kikubwa? Ina maana hayo mapungufu hawayaoni?
Hawa wameshajisahau kwa sababu kuna watu wengine (kama hayo mashirika ya dini) wanafukia mashimo huko vijijini badala yao

Mkuu MN, nadhani pia wanasahau nguvu ya hawa vingozi, wakiwaambia waumini wai wasiipe kura CCM 2010, si basi hakuna kampeni mbaya kama za kutoka madhabahuni na mimbarini mkuu

wao naona wamejisahau kama unavosema,, sasa wananchi wakijua ukweli wao ndo watawaadabisha sawasawa
 
Wana JF wanafki sana,

kwa hiyo unataka kusema Chadema wakipata kuongoza nchi watatoa misamaha ya kodi kwa taasisi zote zisizo za serikali?

Hizi tax exemptions ndio loop holes za kukwepa kulipa kodi. Imefika wakati taasisi za serikali nazo zilipe kodi. Hii kitu inaitwa tax exemption ifutwe kabisa kwenye sheria za kodi za Tanzania. Hata mshahara wa Rais nao uwe unakatwa kodi kama haukatwi

Wakatabahu.

 
Uwiano Maalumu,

Mimi huwa najiuliza: hivi Raisi, VP, WM, JM, Spika, Raisi wa Zanzibar..je hulipa kodi kiasi gani??

Je sii haki yetu sisi raia kujua ni kodi kiasi gani hawa wanalipa kila mwaka??
 
Back
Top Bottom