Wachungaji na Mashehe wanafiki! - Mmevuna mlichopanda!

Sasa niwape ya kwangu.

Kweli naona haya ni yakwako....see my comments below!


Kutumia kigezo cha taasisi za kidini kama sifa ya kusamehe kodi ni kosa kubwa maana humo ndani yao pia kuna ufisadi mkubwa. Misamaha inayotolewa ya kodi kwa taasisi za kidini kwa kiasi kikubwa bado iaishia kufaidisha watu matajiri na kuwaacha masikini wakiendelea kuteseka.

Comment yako ni very general....si kila taasisi liyopata msamaha wa kodi iliutumia kifisadi mtu wangu!

Nina mifano.
Hii mifano yako haiendani na ulichosema hapo juu!

Shule kama St Marian kule Bagamoyo, St Francis, St Mary Goreti ya Moshi na nyingine za namna hiyo zinazosifika zinaeleweka kuwa ni za taasisi za dini, kwa hiyo zinapata msamaha wa kodi.

Mkuu hivi ni misamaha gani ya kodi unaisema hapa....VAT, Corporate, import duty, w/tax au kodi ipi? au unaweza kunitajia ni shule zipi Tanzania hazijasamehewa kodi kwa mantiki hiyo mkuu wangu? taja hata moja tu!

Nijuavyo mimi hakuna shule hata moja Tanzania inayolipa kodi ukiacha indirect taxes through PAYE kwa wafanyakazi wao & withholding taxes kwenye malipo ya supplies wao na pia VAT, excise duty kwenye consumer goods kama simu, vinywaji, vyakula etc but they don't pay kodi ya mapato (corporate taxes) VAT kwenye direct supplies to the schools!

Soma hapa....from VAT Act 1997....Third Schedule..Special reliefs!(before budget ya juzi)

(10)(1) (1) The importation or local purchase by or on behalf of a registered religious, charitable community based, or other non-profit driven organization or institution, of goods or services intended to be used solely by the organization or institution for-

(c) the development, maintenance or renovation by the organization of projects relating to health, education, training, water supply, infrastructure or any other projects relating to advancement of the community

Pia soma hapa....from Second Schedule VAT ACT 1997...Exemptions (kabla ya budget)

1. Educational Supplies

Educational services provided by an establishment registered by the Government

Pia hii hapa....!

1. Books and newspapers

(1) Books, booklets, maps and charts.

(2) Newspapers, journals, magazines and periodicals

Lakini hebu nenda leo kwenye shule hizo kama utakuta mtoto wa masikini! Loh atafikaje humo, wamejaa watoto wa mafisadi tu!

Hi comment nayo ni to general......mimi mwenyewe nimesoma shule ya dini...japokuwa kuna ukweli kuhusu ada kuwa kubwa lakini ada inayolipwa hailingani kabisa na huduma zinazotolewa huko shuleni mtu wangu.....! Huko mtoto unapewa vitabu vyote vinavyo hitajika, unafundishwa vipindi vyote kama mtaala unavyotaka, unapewa mazoezi ya kutosha, unapewa muda mwingi wa kupumzika, unafuatiliwa mwenendo wako wa kitaaluma na kimaadili ukiwa shule na nyumbani, unapewa chakula cha kutosha...asubuhi, mchana, jioni...wakti mwingine hata chai jioni mnapewa, mnalala sehemu nzuri sana......!

Ukilinganisha ada unayolipa kwa kweli inakuwa ni kama faida tupu kwa mwanafunzi....!

Si kweli kuwa eti zimejaa watoto wamafisadi....no, ila huwa wanaangalia intellectual capabilities za mtoto kabla ya kuangalia fedha.....nakuhakikishia nenda na mamilioni yako huko kurobby ili upate nafasi ya mwanao kama hana uwezo hupati kitu!

Shule ada tu ni zaidi ya milioni, eti nao wanataka wasamehewe kodi, si ufisadi huo ni nini? Wanakusanya hela nyingi, karo aghali sana bado hawataki kulipa kodi? Walipe kodi kama wafanyabiashara wengine!

Rejea comment yangu hapo juu.....hakuna shule Tz inalipa kodi hizo unazosisema hapo labda unipe mfamo mmoja tu mkuu!

Hakuna anayezuiwa kufanya biashara. Kama taasisi za dini zinafanya biashara kama hiyo niliyoona kwenye hayo mashule niliyotaja, zilipe kodi kama wengine, wasitake kutuibia kila siku.

Tusichanganye mambo wakubwa....biashara zote zilizoachishwa na mashirika ya dini zinatakiwa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria zetu za kodi! Wewe mkuu unaangalia mashule na mahospitali tu.....nimekwambia hakuna hospital au shule yoyote nyingine Tanzania inayolipa kodi ziwe za binafsi au za serikali!

Ila biashara zinazoendeshwa na mashirika ya dini wanalipa kodi kama biashara nyingine yeyote....kwa mfano kama wanaduka, au kiwanda huko wanalipa kodi tu! Naona watu wamekalia elimu na afya.....hivi vitu viko exempted si kwa dini tu bali hata watu binafsi pia!
 
Wanajamvi wenzangu,

Katika post yangu ya mwanzo niliafiki hatua ya serikali kuhusu kodi dhidi ya taasisi za dini. Nimemsikiliza Mama Kyendesya akichangia, mawazo yake yaliendana na yangu. Lakini nimetafakari usiku na kwenda mbali zaidi katika kuchambua suala hili hususani katika kipengere cha gharama za shule za taasisi za dini.

Nimebaini kwamba taasisi hizi hususani makanisa kama Roman Catholic, KKKT, Aglican na Moravian wanatoa huduma zaidi na justification ya hilo ni kama ifuatavyo;

Tuchukulie mfano wa St Frances ya Mbeya, ada ni shilingi milino 1.8 kwa mwaka ikiwa na wanafunzi 420 tu kwa kidato cha kwanza hadi nne. Hii ina maana kwamba makusanyo ya ada kwa mwaka ni shilingi milioni 756.

Shule ya Wazazi ya Mbalizi yenye ina wanafunzi 1,500 na ada kwa mwaka ni shilingi 800,000; Kwa maana hiyo makusanyo ya ada kwa shule hiyo ni shilingi bilioni 1.2 kwa mwaka.

Unapozilinganisha shule hizi mbili katika utoaji huduma kwa walimu na watumishi wake wengine, huduma kwa wanafunzi na mazingira ya shule zenyewe utabaini tofauti ya mbingu na ardhi, shule hiyo ya taasisi ya dini inaizidi kwa mbali sana hiyo shule nyingine.

Baada ya kuingia kwa undani kiasi hicho nakubaliana kabisa na wale wanaopinga hatua ya serikali kuzibana taasisi za dini, na kama wamebaini kuwepo kwa utapeli kwa baadhi basi wawashughulikie hao kama wahalifu.

Serikali yetu bado haijafikia hatua ya kutoa elimu bora kwa watoto wa wakulima kutokana na aina ya viongozi tulionao sasa, pengine huko bele tutakapopata watumishi wa wananchi.
 
Lakini nimetafakari usiku na kwenda mbali zaidi katika kuchambua suala hili hususani katika kipengere cha gharama za shule za taasisi za dini.

Naona Roho mtakatifu kakushukia usiku.....(joke)

Nimebaini kwamba taasisi hizi hususani makanisa kama Roman Catholic, KKKT, Aglican na Moravian wanatoa huduma zaidi na justification ya hilo ni kama ifuatavyo;

Tuchukulie mfano wa St Frances ya Mbeya, ada ni shilingi milino 1.8 kwa mwaka ikiwa na wanafunzi 420 tu kwa kidato cha kwanza hadi nne. Hii ina maana kwamba makusanyo ya ada kwa mwaka ni shilingi milioni 756.

Shule ya Wazazi ya Mbalizi yenye ina wanafunzi 1,500 na ada kwa mwaka ni shilingi 800,000; Kwa maana hiyo makusanyo ya ada kwa shule hiyo ni shilingi bilioni 1.2 kwa mwaka.

Unapozilinganisha shule hizi mbili katika utoaji huduma kwa walimu na watumishi wake wengine, huduma kwa wanafunzi na mazingira ya shule zenyewe utabaini tofauti ya mbingu na ardhi, shule hiyo ya taasisi ya dini inaizidi kwa mbali sana hiyo shule nyingine.

Watu wengi sana hili hawalioni.....ni muhimu kulinganisha gharama na huduma zinazotolewa huko!

Baada ya kuingia kwa undani kiasi hicho nakubaliana kabisa na wale wanaopinga hatua ya serikali kuzibana taasisi za dini, na kama wamebaini kuwepo kwa utapeli kwa baadhi basi wawashughulikie hao kama wahalifu.

Kama nilivyosema kwenye post yangu hapo juu...serikali haibani taasisi za dini kwenye mambo ya elimu, afya au community development etc educational & health supplies ziko na zitaendelea kuwa exempted kwa kodi nyingi sana na si kwa mashirika ya dini tu bali hata kwa watu binafsi wanaoendesha huduma hizo...tusichanganye mambo hapa!

Serikali imeondoa msamaha wa kodi kwenye supplies au importation ya goods au services ambazo hazitumiki kny ibada moja kwa moja kwa moja kama vile, magari ya kanisa au ya wachungaji, furniture etc
 
Serikali imeondoa msamaha wa kodi kwenye supplies au importation ya goods au services ambazo hazitumiki kny ibada moja kwa moja kwa moja kama vile, magari ya kanisa au ya wachungaji, furniture etc

Is there a better way to exemplify shortsightedness?
 
naona ndoa ya serikali ya wanadamu na dini bandia inaimarika zaidi muda huu kwa kupeana mahela na kila mmoja kumsifia mwenzake kama mume na mke wanavyofanya.
 
Back
Top Bottom