Wachungaji na Mashehe wanafiki! - Mmevuna mlichopanda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachungaji na Mashehe wanafiki! - Mmevuna mlichopanda!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 13, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ati leo wanatishia kuandamana kwa sababu wataondolewa misamaha ya kodi! Leo wamecharuka na kugundua kuwa serikali inaweza kuwafanyizia wakiendelea kupiga kelele. Ati, kwa vile sasa misamaha ya kodi itafutwa kwa taasisi za kidini ukiondoa vitu vya ibada (Biblia, Qurani, tasbihi n.k) ndio wachungaji na mashehe wetu wamecharuka!

  Niliwaandikia karibu mara mbili kuwa wamelala kitanda kimoja na watawala na wamefurahia mahaba ya ufisadi. Ni wao wamekuwa wakiwaalika kila kukicha kwenye tafrija zao na kwenye matembezi yao hawakosi. Sasa leo wameanza kupiga kelele dhidi ya ufisadi na dhidi ya uongozi wanatarajia watawala wacheze chioda?

  Leo wachungaji na mashehe wanaanza kusimama na kunyoshea kidole ufisadi waziwazi wanatarajia kweli misamaha ya kodi iendelee?

  Walichofanya watawala ni kuwabeep hawa! Kwamba wakiendelea na kelele zao dhidi ya viongozi na kunyoshea kidole watawala wajue serikali ina uwezo na ubavu wa kuwafanya walipe!

  Sasa uchaguzi ni wao:

  a. Wapige magoti kwa viongozi wa serikali na kuwaahidi kuwa wakirudishiwa misamaha ya kodi hawatapiga kelele dhidi ya viongozi (a.k.a kujihusisha na siasa)

  b. Waamue kupandisha gharama za huduma zao za kijamii ili waanze kutengeneza faida kama taasisi nyingine za kibiashara na hivyo kuchangia kwenye pato la taifa. Baadhi ya huduma ambazo inabidi waongeze gharama ni pamoja na hospitali, kliniki, mashule na vyuo mbalimbali.

  c. Wafunge baadhi ya huduma zao ambazo ni ngumu kujiendesha na kuziunganisha baadhi ya huduma zao kama wafanyavyavyo wafanyabiashara wengine na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.

  d. Huduma zile za misaada (charity works) zisitishwe na kuacha serikali ifanye shughuli hizo kwa ufanisi vinginevyo wataweza vipi kutoa misaada ambayo wanaigharimia kama bidhaa nyingine. Nani ata offset gharama ya kuingiza, kutunza na kusambaza misaada hiyo. Of course, serikali ina uwezo huo! Sudan walijaribu!!


  Upande mwingine ni kuwa serikali isilegeze uzi bali ing'ang'anie msimamo wake tuone hawa wachungaji na mashehe watafanya nini zaidi ya kupiga mikwara. Najua jambo moja msitarajie Pengo kuandamana mitaani!!! Hata kina Kilaini msifikirie wanaweza kusimama na mabango!

  I know however, rafiki yangu Khalifa Khamisi wa Kwamtoro na wengine wanaweza kuonekana mitaani! Hawa kina Rev. Whoever hawana ujasiri wa kufanya hivyo!

  ===========================================

  Habari Leo
  Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini ameishauri serikali kupitia upya uamuzi wa kuyafutia msamaha mashirika ya dini na asasi za kiraia. Akizungumza jana na gazeti dada la Daily News, alisema taasisi hizo hazitengenezi faida na badala yake, zipo kwa ajili ya kuwainua watu wa kawaida ambao ni masikini. Alitoa mfano wa huduma za afya zinazotolewa hususan maeneo ya vijijini, ambazo nyingi hutolewa na taasisi za dini.

  "Serikali ilipaswa kukaa na wadau kwa ajili kupata ushauri juu ya hasara na faida ya kuondoa msamaha huo kabla ya kutangaza bajeti yake," alisema Kilaini. Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu (masuala ya dini) wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Mohamed Khamis alisema uamuzi huo unakwamisha sera ya Taifa ya kuwapa maisha bora wananchi.

  Alisema taasisi za dini hazitengenezi faida na nyingi zinategemea wafadhili. Alisema inapaswa itoe ruzuku kwa taasisi hizo, ili kuziwezesha kuendesha shughuli zake za kila siku. Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Dk peter Mwamasika, alisema maaskofu wako tayari kuandamana kupinga hatua ya serikali ya kuziondolea taasisi za dini misamaha ya kodi.

  Akizungumza jana Dodoma, Askofu Mwamasika alisema hatua hiyo ya Serikali ni ya hatari na inaweza kuleta mtafaruku usio na sababu za msingi na kuendelea kuwapa ugumu wa maisha wananchi wanaopata huduma kupitia shule na hospitali zinazomilikiwa na mashirika hayo ya kidini.

  Aliishangaa Serikali ya CCM inavyoanza kubadilisha mwelekeo wa utawala wake ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana nayo kuhudumia Watanzania. Aliongeza kuwa KKKT ikiwa sehemu jumuiya ya Kikristo Tanzania, inatambua wajibu wake wa kuhudumia mtu mzima yenye maana ya kiroho na kimwili na ndiyo maana inahudumia kwenye elimu, afya, vituo vya watoto yatima, walemavu na walioko katika mazingira magumu.

  Askofu huyo alisema wabunge na mawaziri na hata marais waliotangulia, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, watambue kwamba elimu waliyo nayo na afya walizonazo, zimetokana na vituo vya mashirika ya kidini, hivyo si vyema kudai kuwa ndio wanaochangia kuyumba kwa uchumi wa nchi.

  Alihoji: "Iweje leo kwenye karne ya 21 ionekane kwamba mashirika ya dini ndiyo yanayosababisha upungufu wa bajeti ya Serikali wakati mashirika ya dini yanachangia sehemu kubwa ya afya, elimu na huduma zote za jamii?" Alisema kupuuza mchango huo wa mashirika ya dini ni kuanzisha mtafaruku, "kwa hiyo tunawasihi wabunge, mawaziri, wanasheria, Rais watafakari kwa makini jambo hilo."

  Askofu Mwamasika alisema serikali kabla ya kutoa uamuzi kama huo ilistahili kwanza kukutana na viongozi wa dini na wazee kama ambavyo alivyokuwa akifanya Rais Julius Nyerere wakati alipotaka kufanya uamuzi mkubwa kama huo. Hata hivyo alisema hotuba ya Rais Jumatano wiki hii alipozungumza na wazee wa Dodoma, ililenga kuwaondolea shida Watanzania na kuinua uchumi wa nchi.

  Alisema Taifa liliipokea hotuba ya Rais kwa furaha, kwani ililenga kumkomboa mwananchi wa chini; lakini ya Waziri wa Fedha na Uchumi, iliona namna ya kunusuru uchumi ni kufuta msamaha wa kodi uliokuwa unatolewa kwa mashirika ya dini. "Kwa kweli Waziri wa Fedha amevuruga." Alisema KKKT inapinga hatua hiyo.

  "Nasema tunapinga na sisi maaskofu tumekubaliana kuwa kama Serikali haitabatilisha uamuzi wake tutaandamana hadi kwa Rais Kikwete, kwani hatuwezi kukubali watu wetu waendelee kupata shida wakati kaulimbiu ya Rais ni Maisha Bora kwa kila Mtanzania." KKKT ina hospitali 23, zahanati 139 na vituo vya udiakonia 19.

  Askofu Mwamasika alisema iwapo serikali itaendelea na uamuzi wake wa kutotoa msamaha wa kodi kwa mashirika ya kidini ina maana hospitali hizo zinaweza kufungwa. Naye Msaidizi wa Katibu wa Jumuiya ya Kikristo (CCT), John Mapesa, alisema alipokea simu nyingi kutoka kwa maaskofu wa madhehebu yanayounda jumuiya hiyo, wakitaka kujua kama jumuiya ifanye nini kuhusu bajeti iliyosomwa na Waziri.

  Mapesa alisema kitendo cha serikali kufuta msamaha wa kodi kwa taasisi za kidini kinarudisha nyumba juhudi zinazofanywa na mashirika hayo kuisaidia jamii wajibu ambao unastahili kufanywa na serikali.

  "Madhehebu ya kidini yanachofanya ni kuisaidia serikali, kwa hiyo ni lazima ikubali kuwa taasisi hizi za kidini ni wadau wakubwa wa maendeleo, hivyo ni lazima waendelee kuzilea," alisema Mapesa.

  Alisema anaamini serikali itafikiria upya uamuzi huo kwani unalenga kuvunja moyo hata wahisani ambao wamekuwa wanatoa fedha na vifaa vyao kwa ajili ya kuzisaidia taasisi za kidini ili ziweze kutoa huduma mbalimbali kama afya na elimu kwa jamii.

  Aliongeza kuwa huduma nyingi za makanisa zina mafanikio makubwa kuliko hata ambazo zinasimamiwa na Serikali, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuzipa taasisi hizo misamaha ili ziendelee kutoa huduma zao kikamilifu.

  Alisema haamini kuwa misamaha inayotolewa kwa mashirika ya dini ndio imesababisha uchumi wa nchi kuyumba au mapato kushuka, bali yawezekana kuna mahali ambako misamaha hiyo inatolewa kwa wingi na sasa kusingizia taasisi za kidini.

  "Nawaomba wabunge waliangalie jambo hili pale wanapokuwa wanajadili hotuba hiyo ya bajeti, kama wao wanajua na wanaona huduma zinazotolewa na zahanati au hospitali za kidini katika maeneo yao nadhani watapinga jambo hili," alisema.

  Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa, alisema yeye aliwahi kuwa kiongozi wa dini na anajua kuwa sehemu ambako kuna hospitali ya misheni, serikali haina huduma katika eneo hilo, hivyo kitendo cha kuzifutia misamaha taasisi za kidini ni kuleta umasikini kwa Watanzania.

  "Nchi hii ni kubwa, lakini kuna taasisi za kidini zimepeleka huduma kila kona, leo hii unazifutia misamaha ya kodi, si unataka zitoze fedha zaidi kwenye matibabu na kwenye shule, kwa hili hatukubali," alisema Dk Slaa. Juzi akiwasilisha bajeti ya Serikali, Mkulo alisema Serikali inapendekeza kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

  Ila alisema vifaa ambavyo vinaagizwa kwa ajili ya huduma za kiroho vitaendelea kupata msamaha wa kodi. Hata hivyo maaskofu wanasema mambo ya kiroho ni elimu, afya na akili, hivyo serikali inapaswa kufafanua vifaa vya kiroho inavyojua, "yawezekana wanasema Kurani na Biblia tu."
   
 2. H

  Honey K JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2009
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mhhh kwakweli katika mambo yamenishangaza ni hili! Pamoja na kuwa ni kama hujuma kwa wananchi, lakini naamini ni hujuma kubwa kwa CCM maana kama hoja ni maisha bora kwa kila Mtanzania, hii ni kukihujumu chama waziwazi coz itavuruga mpango wa kuleta maisha bora, coz maisha bora ni pamoja na afya bora na karibu, shule nk.
  Iko haja kwa wana CCM pia bila kujali ushabiki kulipinga hili bila kigugumizi.
   
 3. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #3
  Jun 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kweli hao maaskofu nk ni wanafiki sana. Si ndio hao walidai JK ni chaguo la Mungu? Walijuaje kama Mungu alikuwepo katika mchakato wa kumchagua uliojawa na ufisadi? sasa leo hii wanaanza kulalamika nini? ngoja wakome kwa kimbelembele chao. Mungu hawezi kuchanganywa na uchafu wa ufisadi uliokithiri halafu hao waliokuwa wateule wa kazi ya Mungu wakashiriki kupamba ufisadi, halafu wanatuhadaa nini sasa. ni kweli MMJ, wamefuna wapandacho. Hongera Mwanakijiji kwa post hii.
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nilishaonya huko nyuma kuwa hizi dini zetu ndo chanzo cha umaskini. Taratibu tutaelewana tu.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mi nafikiri hii option ndio nzuri.

  Kwa hivi sasa huduma za jamii zikizidi kuathirika kwa kukosa input ya mashirika ya kidini hata wale wananchi vipofu wa Busanda-type wataanza kupata mwangaza wa nani hasa ni mbaya wao. Hapo itawafanya waanze kupekecha vichwa vyao zaidi na kufanya maamuzi sahihi zaidi pengine.

  Kwa hali ilivyo sasa, hatua ya kuzitoza kodi mali za kidini ziingiazo nchini ufadhili kutoka nje kwenye huduma za kijamii utapungua au kuisha kabisa au kuhamishia shughuli zake kwenye nchi nyingine. Tukumbuke kuwa wahitaji ni wengi na hata hao wanaotoa misaada sio wote wenye uwezo wa akina Bill Gates, wanapotoa wanahitaji kuona matokeo ya kujinyima kwao.

  Wafadhili wengi hupitisha michango yao kupitia vyombo vya kidini kwa imani kuwa kuna urasimu kidogo, kwamba michango yao ya itawafikia walengwa bila urasimu wala upotevu wa kimuundo etc kwa kuzingatia hilo basi hakuna mfadhili atakayetoa nyenzo au fedha ilipie kodi kodi badala ya kuangalia atamsaidia vipi mwananchi mwenye uhitaji. Hata mimi ningekuwa mfadhili nisingeweza kutia ndururu kwenye system ya serikali yenye longolongo na iliyoshindwa majukumu yake.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nadhani unahitaji ku-revise chanzo cha umaskini nchini. FYI, Chanzo cha umasikini wa mtu mweusi ulianza hata kabla ya kuja kwa wakoloni na dini za kigeni.
   
 7. Mujuni2

  Mujuni2 Senior Member

  #7
  Jun 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sijawahi kuona post ya kushangaza Kama hii by MMJ yaani kwa tafsiri yangu ni kama unafurahia vile! Sasa swali Kama humu huwa tunajifanya ni wazalendo ktk hili tulitakiwa tupinge Kwa nguvu zote. mchango wa mashirika ya kidini as far as community development unaonekana hata Kwa kipofu. hivi sisi ambao tuko nje ya nchi tunapotoa kauli za kukejeli kama hizi za wakome, wanafiki n.k. Tunasahau kuwa bila ya hizo hospitals kuna wengine hata mama zao wasinge- deliver safely, angalia Peramiho,Bugando, na nyingine nyingi. hata shule wengi wa baby boomers wamesoma seminary regardless of their faith.Kama misamaha hakukusaidia wewe basi kaka, binamu, babu na bibi zako huko vijijini wamefaidika na wanaendelea kufaidika. kuna mambo ya kudhihaki lkn sio hili.
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hiyo kodi watakayotozwa na serikali si itatumika huko huko kwenye community development (kujenga mashule, kununua madawa nk.)?

  After all dini zingine (mfano ile dini ya Kakobe, etc.) ni private owned na hazina mchango wowote kwenye community development (hakuna cha hospitali, shule, nk - pesa yote wanaweka mfukoni).
   
 9. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Its a wrong move from the government, hata hivyo govt ina beep tu it won't erase tax relief to religious organisations. There is a lot of influence from the Vatican, Iran e.t.c. Ukiangalia investment ya religious organisations in TZ ni kubwa sana kiasi kwamba kusema walipe kodi itakaua a big blow!
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  urafiki na khalifa khamis umeanza lini? mwenyewe mbona anasema hakujui?

  na zaidi ya hayo anashangaa umetoa wapi wazo kuwa ataingia mtaani?
   
 11. e

  ejom Member

  #11
  Jun 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Hapa cha kufanya ni kupandisha gharama za huduma kama elimu, afya,nk halafu tuone madhala yake kwa jamii tukizingatia kuwa hospitali na zahanati nyingi za mathehebu ya dini zipo vijijini kwenye wapiga kura wengi wa CCM.Na hiyo itoa jibu halisi 2010.Kupandisha huku kuambatane na msamaha ulio tolewa.
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Serikali inajidanganya katika suala hili la kodi kwa mashirika ya kidini, yawe ya Kikristo ,Kiislamu au Bohora.
  Inaelekea Serikali haijafanya utafiti katika hili na italijutia katika muda si mrefu ujao.
  Viongozi wetu wengi wamesoma BURE katika hizi shule. Sasa tujiulize biashara iliyopo pale.
  Kikwete kasoma nafikiri Lugoba Seminary,Nyerere ndo kabisa ikiwa ni pamoja na kufundisha shule ya Pugu Seminary.Siyo siri kuwa watakao athirika zaidi na msimamo huu wa kodi ni Kanisa la Katoliki ambalo lina miradi mingi zaidi ya kijamii.
  Kwa hili basi serikali inbidi ikubali ya fuatayo-
  1)Kanisa libadili msimamo wake wa jadi wa kutoa huduma za kijamii kwa bei nafuu na kufanya kibiashara
  2)Kufunga huduma zote zisizoweza kujiendesha kibiashara
  3)Hospitali kama KCMC,Bugando sasa ziwe private
  4)Shule kama St Francis-Mbeya, Mazinde Juu,Kifungilo Girls,St Marian Bagamoyo ziwe private schools na zitoze ada istahiliyo kama hizi "International Schools " za Dar es salaam

  Ni wazi kuwa msimamo wa madhebu yote ya dini ni kinyume na kufanya mambo kibiashara hivyo ufinyu wa mawazo ya kutakiwa kufanya shughuli zake kibiashara utaonekana muda si mrefu
   
 13. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Viongozi wa dini wawe wajasiri kwa hili. Wasikubali kutumiwa na serikali kujipatia umaarufu isio ustahili! Katika kuonyesha wako serious - wafunge huduma zote za taasisi za dini hata kwa mwezi mmoja tu (najua watu watakufa kwa kukosa huduma - labda including me). Lakini nasema wafunge - hiyo itawatoa ujinga hata wananchi wanaodhani nchi hii bado iko chini ya Nyerere! Kama taasisi za dini zitafanya hivi - basi move ya serikali itakuwa ilikuwa ni 'a blessing is disguise'. Naamini watanzania wote (mpaka wasonjo) watajua maana ya kupiga kura na kuwa hata mtu wanayempigia kura ana matter!

  Lakini pia inawezekana serikali imeamua kutangaza hili ili watu wakilalamika tu iliondoe halafu ipate umaarufu (very cheap!). Na watu walivyo na papara serikali ikiondoa ikirudisha hiyo misamaha wataandamana kuipongeza na kuendelea kuwahubiria watu kuwa hii ndiyo serikali chaguo la mungu! Viongozi wa dini lazima watafakari kiini cha uamuzi huu wa serikali - na waihukumu kwa hilo. Ni vigumu kuamini watu wote huko serikalini ni blind kiasi hicho - kwamba serikali inaweza ku-operate bila support ya taasis za dini! Au kuamimi kuwa serikali (kundi la watu wachache - clique ya ufisadi!) iko juu ya kila mtu! Serikali hii inawezekana inafanya mambo ya Gobachev (working for the enemy) bila kujua!

  Sitaki serikali iachwe kwa hili, sitaki asingiziwe Mkulo na JK aachwe!, sitaki serikali ikibadili msimamo ipate credit!, sitaki kusikia maaskofu wanaandamana kupinga budget halafu tena waje waandamane kuipongeza serikali kwa kuwakubalia 'ombi lao', sitaki,........ sitaki,......... sitaki........grrrrrrrrrrrrr!
   
 14. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ni bahati mbaya sana kuwa hawa wachungaji wetu nao kwa muda mrefu wamesahau wajibu wao. Kazi kuu ya padre/mchungaji ni kufundisha na mafundisho hayo yanajumuisha mambo yote yanayosaidia ustawi wa kiroho. Wanachotakiwa kufanya sasa hivi si kuaandaa maandamano. Washikamane wote, wakatoliki, waprotestanti, wapentekoste, waislamu na wengine wote kuwaelimisha waumini wao jinsi ustawi wao unavyohusiana moja kwa moja na ushiriki wao katika kuchagua viongozi. Haiwezekani kuyatoza kodi mashirika ya kidini huku makampuni yanayotuibia madini yetu yakibebwa na hawa wakuu kuendelea kutunyonya.

  Wakatoloki wameonyesha njia, ni muda muafaka taasisi hizi za kidini kusaidia kuleta mabadiliko kwa kutumia nguvu kubwa ya waumini wao, muhimu ni wote kutambua kuwa adui yao wote ni mmoja.
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280
  Vipi ndo harufu ya mapinduzi ya Poland mwaka 1979? Tunaweza kufika huko? wako wapi kina Karol Wojtyla wetu?
   
 16. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mtakubali pale mtakapoona waumini wanafadhiliwa Iran na Saudi Arabia, hamtauliza swali?

  Ni vema wamefuta huo mwanya wa kukwepa kulipa kodi. Nani asiyejua kuwa hawa viongozi wa dini wamekuwa wakijitajirisha kwa kuhusisha biashara zao na misaada ya kidini ili kukwepa kodi? Ikifika wakati wa kuweka tathmini ya misaada iliyoingia bila kulipiwa kodi na kuwafikia walengwa ni chini ya asilimia 30. Mwenye kubisha alete data.

  Lipeni kodi.
   
 17. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
   
 18. e

  ejom Member

  #18
  Jun 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  sasa ni wakati wa kuungana mathehebu ya dini yote kuingoa CCM maaskofu masheh msiende ikulu kuomba msamaa urejeshwe hubirini namna ya kuingà CCM huo ndio utakua muaafaka
   
 19. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi sielewi kwanini tunalalamika sana.Pia naona kuna options mbili tu.

  1.Kama mashirika ya dini yana msaada mkubwa kwa wanakijiji wengi basi wao waongeze bei ama wasimamishe huduma zao effect yake itajulikana 2010.

  2.Na kama haya mashirika hayana effect kwa wananchi basi walipe kodi.Mfano shule hospital hata mimi naona walipe kodi tu.
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nilishatabiri hii misamaha itaondolewa kwao kwani nakumbuka wazee wa TRA walifanya study research kufuatilia miradi ya kidini wakakuta asilimia kubwa hailingani na uhalisia wa hiyo inayoitwa misaada. Yaani wanatumia asilia chini ya 20 kwa aslimia mia moja ya msaada. Mzee wangu ni mchungaji wa kanisa lake binafsi mahala fulani tanzania, najua ataathirika sana au hata kufunga huduma endapo atabanwa zaidi alipe kodi.

  Ila nikiangalia upande wa pili ni kwamba hawa makasisi wa dini wamekuwa mstari wa mbele kupokea mafungu makubwa ya matoleo kutoka kwa wahujumu mbalimbali huku wakiwajua. wanawaombea mna kunywa nao mvinyo. Pia hawa makaasisi wamekuwa wakiishi maisha tofauti na maadili ya kidini yatakavyo kwani wengi wamejijengea himaya kutokana na unaudited funds kutoka kwenye makusanyo mbalimbali.

  Mwanakijiji nakuunga mkono kuhusu unafiki wa baadhi ya viongozi wetu wa kidini ktk kuandamana. Wanahubiri maji huku wakibugia mvinyo.

  Kama mimi mtoa sadaka akatwa kodi je mpokea sadaka asikatwe kodi pia??? Ila itakuwa laana endapo serikali itaamua kukata kodi kwenye fungu la kumi.

  Mkulo awe wazi in details kuhusu maeneo ya kodi ktk taasisi hizi za kidini maana ameongelea shallow mno. aweke details kama alivyoichambua bhangi ops sigara na vilevi.
   
Loading...