Wachezaji wa Ivory Coast, Nigeria na Afrika Kusini wapewa zawadi nono na serikali zao.

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
12,902
15,331
Pesa, nyumba na heshima zinatolewa kwa wanasoka kutoka Ivory Coast na Nigeria, baada ya mchujo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili. Kila mchezaji katika kikosi kilichoshinda cha Ivory Coast ataweka mfukoni $82,000 (£65,000) zaidi ya shilingi milioni mia mbili za kitanzania na kupata nyumba yenye thamani sawa na hiyo, ofisi ya rais ilitangaza. "Mmeleta furaha kwa Wana-Ivory Coast wote, jasiri, jasiri," alisema Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast, ambayo ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya Afrika nzima.

Kila mchezaji wa kikosi cha Nigeria amepata mojawapo ya tuzo za juu kabisa za nchi hiyo - Mwanachama wa Order of the Niger. Rais pia anawapa kila mmoja nyumba na kipande cha ardhi karibu na mji mkuu, Abuja.

Afrika Kusini iliyo nafasi ya tatu pia inatazamiwa kupokea takriban $52,000 (Zaidi ya shilingi milioni 130 za kitanzania) kwa kila mchezaji, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Haijabainika ni malipo gani ya pesa ambayo wachezaji wa Nigeria watapokea kutoka kwa mkoba wa serikali.

 
Si bora tumetoleea mapema. Jamaa wangepewa kadi ya CCM na fulana za nani kama Mama. Pesa za zawadi, TFF wangeenda kurekebisha ofisi zao pamoja na kukarabati nyumba ya Rais wa TFF.
 
Back
Top Bottom