Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 1,914
- 6,029
Majira ya Saa 5:00 Usiku kutapigwa mchezo wa Fainali ya AFCON 2024 ambapo Nigeria atawavaa wenyeji Ivory Coast.
Ni mchezo unaovuta hisia za wengi hasa kutokana na viwango vya timu zote mbili. Nigeria ikionekana ni timu iliyokamilika huku Ivory Coast unyumbani ukiwasaidia.
Kura yako unampa nani kuibuka na ubingwa?
Tukutane hapa kuanzia saa 5 usiku, huku mechi ikiwa mubashara Azam Tv, Star Times, DStv.
=========
Timu ya Taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kubeba ubingwa wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa kuifunga Nigeria magoli 2-1 katika Fainali, ikiwa ni ubingwa wao wa tatu kutwaa baada ya kufanya hivyo Mwaka 1992, 2015 na sasa 2024.
Licha ya Nigeria mbayo imetwaa kombe hilo mara 3 kutangulia kufunga kupitia kwa William Troost-Ekong dakika ya 38, wenyeji wa michuano hiyo walipambana na kusawazisha kupitia kwa Franck Kessié dakika ya 62 kisha kuongeza la pili dakika ya 81 mfungaji akiwa ni Sébastien Haller.
Ivory Coast ilianza michuano hiyo kwa kusuasua, ikipita katika Kundi A kuendelea na Hatua ya Mtoano licha ya kushika nafasi ya Tatu.