SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,897
Katika mechi za mwisho hatua ya makundi katika mashindano ya AFCON 2023, Ivory Coast walikuwa wanahitaji Morocco ishinde mechi yake dhidi ya Zambia ili iweze kuinusuru Ivory Coast kuweza kuvuka hatua iliyofuata ya 16 bora. Na kweli, Morocco ilishinda 1-0 na Ivory Coast ikavuka kama best loser.
Toka wakati huo, watu wa Ivory Coast walianza kuishangilia Morocco katika mechi zake na baada ya Morocco kutolewa, wameendelea kuisifu na kuonyesha aina mbalimbali za mahaba kwa taifa hilo. Jana baada ya kuchukua ubingwa wa AFCON, waliishangilia sana Morocco baada ya bendera yake kuonyeshwa kwenye screen na kuna mchezaji wa Ivory Coast alizunguka uwanja mzima akipeperusha bendera ya Morocco.
Kwa nini nasema huu ni upuuzi uliopitiliza? Kuanzia mafanikio ya timu zao za taifa na ya wachezaji mmoja mmoja, Ivory Coast ni taifa kubwa katika ulimwengu wa soka, siyo tu hapa Afrika bali duniani kwa ujumla. Hawatakiwi kujidhalilisha kiasi hiki.
Pili, timu zote zinazojitambua zinataka zishindane na kushinda mechi zao zote hata kama ni za kirafiki au za kukamilisha ratiba. Morocco hawakuifunga Zambia kwa kuwa walikuwa wanataka kuwafanyia favor Ivory Coast bali walikuwa wanataka kushinda kwa sababu ni wajibu wao na kwa fahari ya taifa lao.
Iangalie Cape Verde ambao walienda mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Misri wakiwa tayari wameshafuzu ila walicheza kwa nguvu na jitihada utadhani wanapigania wasishuke daraja na wakalazimisha sare dhidi ya Misri iliyokuwa inaponea chupuchupu kutolewa. Hivyo ndiyo timu zote zinazojitambua zinavyotakiwa kucheza.
Embu waambieni Ivory Coast waache kujiaibisha. Matokeo ya mpira ndiyo yaliwavusha na siyo favor za Morocco.