Hii hapa ratiba ya Hatua ya 16 Bora ya AFCON 2023 Nchini Ivory Coast

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Baada ya Tanzania kushika nafasi ya mwisho katika Kundi F na kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataofa ya Afrika (AFCON2023), ratiba ya Hatua ya 16 imejulikana.

Timu ambazo zimeingia hatua hiyo kupitia nafasi ya Mshindi wa Tatu Bora ni Guinea, Namibia, Mauritania na wenyeji Ivory Coast.

Januari 27, 2024
Angola vs Namibia
Nigeria vs Cameroon

Januari 28, 2024
Equatorial Guinea vs Guinea
Misri vs DR Congo

Januari 29, 2024
Cape Verde vs Mauritania
Senegal vs Ivory Coast

Januari 30, 2024
Mali vs Burkina Faso
Morocco vs Afrika Kusini
 
Mimi ile game yao ya kwanza mpira aliompigia ghana nikaona jamaa kuna kitu wanataka kufanya hii afcon
Wale wakija kukutana na timu kama Senegal au Morocco katika fainali utapigwa mpira mwingi saana.

Baada ya mechi na Misri nilienda kuangalia profile ya kila mchezaji waliyemtumia katika mechi zao zote 3 kujua wamezaliwa wapi, wana miaka mingapi na wanachezea klabu gani. Yaani mechi na Misri walipumzisha wachezaji kama 6 walioanza mechi 2 za kwanza na bado walikuwa wamoto balaa.

Wale wakienda World Cup watasumbua sana.
 
Baada ya Tanzania kushika nafasi ya mwisho katika Kundi F na kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataofa ya Afrika (AFCON2023), ratiba ya Hatua ya 16 imejulikana.

Timu ambazo zimeingia hatua hiyo kupitia nafasi ya Mshindi wa Tatu Bora ni Guinea, Namibia, Mauritania na wenyeji Ivory Coast.

Januari 27, 2024
Angola vs Namibia
Nigeria vs Cameroon

Januari 28, 2024
Equatorial Guinea vs Guinea
Misri vs DR Congo

Januari 29, 2024
Cape Verde vs Mauritania
Senegal vs Ivory Coast

Januari 30, 2024
Mali vs Burkina Faso
Morocco vs Afrika Kusini

Rais Tsishekedi yuko na timu ya Kongo kabla hawajaingia uwanjani na kaingia kwenye vyumba vya kibadilishia nguo pale uwanjani.Sisi yuko Mwijaku na baba Levo😅😅
 
Cape Verde sio waafrika wale kama Kina Cuadrado majina Yao tu yanaikana Afrika....Hakuna mwenye Jina la kibantu.
 
Cape Verde sio waafrika wale kama Kina Cuadrado majina Yao tu yanaikana Afrika....Hakuna mwenye Jina la kibantu.
Wana damu ya Cape Verde hilo ndiyo la muhimu. Sisi Diaspora wetu wanatuletea kina......wachezaji ambao viwango vyao havina tofauti na wale unaoweza kuwakuta huko Mpwapwa ndani ndani
 
Back
Top Bottom