Wachaga nini siri ya mafanikio yenu?

Wanaendaga kuoga dawa kila mwisho wa mwaka tarhe 25 december to jan 1 pia hufanya matambiko na ibada za kichawi ili mizimu ya babu zao iwape utajiri na wakija humu jukwaani hujifanya wanaponda sana mambo ya waganga na kujifanya wao ni watu wa mungu na degree zao za hapa na pale
Matambiko na kuoga dawa ( kwa waganga) ni tofauti sana. Kila kabila lina matambiko yake.
Hata uchawie vipi kama hujitumi huendi mahali. Na hapa ndipo wachaga wanafunika wanajitumw, nidham ya pesa, jicho la fursa
 
Hakuna ushirikina , ila kila jamii inapenda kuzipa desturi za jamii nyingne jina hilo ,wakiona desturi zao ni bora na sahihi zaidi .

Tufanye jina la desturi hiyo liitwe tambiko na sio ushirikina...
Je, kwa akili ya kawaida tu unaona ni sahihi kwa mwanadamu aliyehai, kwenda kuwaomba msaada wa kimaisha na mambo mengine wanadamu waliokufa (wafu)?
 
Mbona sasa Mamangi mnalewa sana?
Hiyo ni desturi tangu kale na kale pombe ni kinywaji kitakatifu kwenye mila na desturi za wachaga
1713711281209.jpg
 
Uliza
Niseme tu kwanza mimi sio mchaga na wala sina unasaba wowote na kabila hilo ila kiukweli nahusudu sana mafanikio ya wanaotoka kabila hili na kuwaomba watuanikie siri ya mafanikio yao.

Maana kama hizi shule wote tunasoma nao shule hizihizi tena wengi wao wala hawana maajabu huko madarasani ila wenzetu hawa mkikutana miaka kadhaa baadaye unakuta wewe upo hapa yeye yupo kuleee.

Siri nini wakuu? wengine tunakosea wapi?
wana Yanga mbege namkisusio
 
Tufanye jina la desturi hiyo liitwe tambiko na sio ushirikina...
Je, kwa akili ya kawaida tu unaona ni sahihi kwa mwanadamu aliyehai, kwenda kuwaomba msaada wa kimaisha na mambo mengine wanadamu waliokufa (wafu)?
Hizo ni mila na taratibu za hiyo jamii , je unafikiri ni sahihi kuomba Mungu asiye onyesha hata dalili uwepo wake?
 
Kama wadau wengi walivyochangia wenzetu wana nidhamu sana ya pesa ingawa wkt mwingine huenda ikaleta maradhi,,,, hawa jamaa kushinda mchana na karanga pakti moja sio ishu

Point kubwa wana nidhamu kubwa ya pesa na kujituma pamoja na kuinuana,,,, katika ukoo wengi wenu mkiwa vizur ni rahisi kutoboa kwakuwa huna majukumu kwa ndugu zaidi ya familia yako

Kinyume na koo ambazo wengi hawako vizur utabakia kusapoti sana ndugu kifedha na kushindwa kufanikiwa zaidi

Kuna boya mmoja kwenye comment alisema sijui vitabu rich dad poor dad havina maana,, asichojua wachaga wanatekeleza hizo principle bila wao kujua,,, hicho kitabu kinafundisha jinsi ya kuwa na nidhamu ya pesa

Anayekidharau hicho kitabu huenda hajakielewa, niliandika uzi wa hicho kitabu bht mbaya Siku hizi kushare nyuzi kuna changamoto
 
Wanaendaga kuoga dawa kila mwisho wa mwaka tarhe 25 december to jan 1 pia hufanya matambiko na ibada za kichawi ili mizimu ya babu zao iwape utajiri na wakija humu jukwaani hujifanya wanaponda sana mambo ya waganga na kujifanya wao ni watu wa mungu na degree zao za hapa na pale
Pole sana bidada.

Na hiyo avatar ya mtoto anayevuta bangi imeendana na wewe kabisa.
 
Niseme tu kwanza mimi sio mchaga na wala sina unasaba wowote na kabila hilo ila kiukweli nahusudu sana mafanikio ya wanaotoka kabila hili na kuwaomba watuanikie siri ya mafanikio yao.

Maana kama hizi shule wote tunasoma nao shule hizihizi tena wengi wao wala hawana maajabu huko madarasani ila wenzetu hawa mkikutana miaka kadhaa baadaye unakuta wewe upo hapa yeye yupo kuleee.

Siri nini wakuu? wengine tunakosea wapi?

Sababu ya kutokuwa na uchawi na ushirikina miongoni mwa jamii zao (Uchagani).

Wana bahati sana wenzetu.

Kule mafanikio ya mtoto niwa jirani ni fahari ya jamii yao yote.
 
Pitieni hapa mtakuwa kama wachaga

Ni

Nidhamu ya PESA ni kuwa na kiasi katika kipato chako unachopata ah unachoingiza kupitia katika biashara yako, kazi n.k

Ili kufika hatua ya kuwa na nidhamu ya pesa huenda sambamba na kujinyima starehe za muda mfupi Kama 👇🏾

@ Pombe
@ Bangi, sigara
@ wanawake ,kuhonga PESA n.k
@ mitoko ya weekend , party n.k
@ kukaa mbali na liabilities

Baada ya hapo hela utakayofanikiwa kuipata utaweka AKIBA then utaangalia wapi uendelee kufanya uwekezaji

Nb kuwa na nadhamu ya pesa hutegemea zaidi na kiwango chako cha kuzikabili hisia zako na za watu wengine Emotional intelligence.
Kifupi ni ubahili
 
Back
Top Bottom