Kwanini msiseme mna mafanikio makubwa kwa SABABU wakoloni waliwekeza sana huko?
Mkuu,
Wakoloni waliwekeza Moshi kuliko Bukoba? wakoloni waliwekeza Iringa, Bukoba, Arusha, Njombe nk
Tofauti na mikoa mingine mandeleo unayoyaona Kilimanjaro yameletwa na wazawa wanajenga shule wenyewe hospitali, barabara na wanahakikisha watoto wanakula shuleni (kitu ambacho kimeshindikana maeneo mengi Tanzania) Kilimanjaro Elimu ni kipaumbele namba 1
Kuna nyuzi nyingi humu zinaeleza mfano;
Kuna uzi humu wananchi wa Vunjo walichanga bilioni 7 ili kujenga barabara yao (ulishawahi kuona hiki pengine?)
Marehemu mzee Mengi alikuwa anatoa maziwa kwa wanafunzi mashuleni, anasomesha na kujenga miundombinu.
Angalia pia Millard Ayo Tajiri Laswai alichofanya mashuleni Rombo.
Wilaya ya Rombo ndio inaongoza kuwa na shule nyingi Tanzania nzima
Zimejengwa na wananchiwananchi na wanahakikisha walimu wanapatikana kwa namna yoyoye hakuna kukaa kinyonge
Watu wa Kilimanjaro hawasubiri Serikali iwafanyie wanafanya wenyewe.
Hivi vyote ni wananchi wanafanya na wanasimamia wenyewe.
Hivi unajua mafundi wa magari wa kuaminika Tanzania nzima wako Moshi?, wanatengeneza yaliyoharibika, wanatengeneza matela mapya, wanaunga magari ya watalii nk
Gari inaweza ikashindikana Dar lakini sio Moshi, unadhani ni mkoloni? Nyumba nzuri zilizojengwa huko migombani zimejengwa na wakoloni?
NENDA KAJIFUNZE.!!