Wachaga nini siri ya mafanikio yenu?

Wachaga nini siri ya mafanikio yenu?

Wachagga wanafata kauli mbiu ya Fanya kazi, pata kipato, wekeza kwa baadae (miradi, elimu ya watoto, kuwasaidia ndugu), na mwagilia moyoo (mvinyo mvinyoo)
 
Hapa umetushika masikio...

Matambiko na zile mishemishe za kuongea makaburini mkirudi migombani huwa unaona jambo la kawaida sio?
Mkuu unataka kusema kua wachaga ndio kabila pekee nchi hii linalofanya matambiko? Mbona kila kabila na jinsi yake tena wengine ni washirikina wanaosifika ila kwa maendeleo hawawakuti wachaga?

Au tuseme hiyo miungu ya jamaa zetu wameshikilia mifumo ya utajiri/maendeleo
 
Kwa kifupi wachaga na wakinga wanatelezea mulemule kwenye wito Mungu aliowaitia..

Kila mtu/kabila kuna kitu Mungu amewawekea ili kutimiza kusudi lake kwetu na hapo na sisi tunafanikiwa!!

Kwa wasomaji wa biblia mtaungana na mimi kwa kurefer makabila 12 ya Israel (watoto wa Yakobo) pale baba yao alipokua anawabariki, alimtamkia kila mmoja baraka yake. Wengine ni makuhani, wengine ni wafalme nk.

Sasa wewe mnyakyusa usipokua muhubiri na mambo yanayofanana na hayo utakua unapishana na gari la mshahara!!
 
Pia wanaamini mungu kidogo, sio kila saa ibada na kusikiliza upotoshaji wa wapotoshaji.
 
Back
Top Bottom