Wabunge wapinga billlioni 6 kurejeshwa Serikalini

Kanifurahisha Msigwa anasema wamezuiwa kwenda nje kuangalia nyumba za ubalozi.....dah
 
Kweli. Ki uhasibu pale fedha inapobaki kwenye mwaka mmoja wa fedha huwa carried forward kwenye mwaka mwingine wa pesa... Na sio kurudishwa ilipotoka...
unazungumzia fedha za serikali au taasisi binafsi? Kama huu mwak mwingine nao unakuwa na bajeti yake, je hizo zilizobaki zinaingia wap?
 
Wabunge nao ni majipu tu. Wanataka watengewe fedha ili wakaangalie nyumba za ubalozi? Watoto hawana madawati wao wanataka kwenda kuangalia nyumba?
 
Tulia katulizwa pale na muzee sasa ataacha kufuata maelekezo kutoka juu?
Lkn bunge ni muhimili unaojitegemea so ni vizuri wabunge wangeshirikishwa.
Utawashirikisha wabunge wanaotaka kwenda kuangalia nyumba za ubalozi? Wabunge wangekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, ufisadi nchi hii usingefika hapo. Wabunge kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya tatizo la nchi hii
 
Msigwa analalamika kuwa wabunge wameshindwa kusafiri nje ya nchi kwenda kuangalia balozi? Kila mwaka wamekuwa wanasafiri kuangalia kitu hicho hicho, nchi imepata faida gani? Na kwa 'akili kubwa' ya Msigwa bora wabunge wapande ndege kwenda kushangaa majengo Ulaya kuliko watoto kukaa kwenye madawati? Naomba kuuliza kwenye jimbo la huyo mchungaji shida kubwa waliyonayo wananchi ni wabunge kutokwenda Ulaya?

Bunge limekuwa ni chanzo cha umaskini nchi hii.
Hawa si wawakilishi wa wananchi,wanajiwakilisha wao wenyewe na familia zao.Haiwezekani hela kupelekwa kwenye maendeleo watu wanakataa.Vipaumbele vyao ni vipi??
Tatizo bunge imekuwa sehemu ya kutokea kimaisha kwa wengi wao na sehemu ya kutengeneza mtandao wa kujinufaisha badala ya kusaidia wanyonge.Inasikitisha sana.
 
Utawashirikisha wabunge wanaotaka kwenda kuangalia nyumba za ubalozi? Wabunge wangekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, ufisadi nchi hii usingefika hapo. Wabunge kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya tatizo la nchi hii
Basi aamue yeye kila kitu kuhusu bunge hawa kina spika na wenyeviti n.k tupa nje au unasemaje mkuu
 
Kwanza Nakupa Pole ya Kufiwa na Baba Yako Mkubwa!

Pili,Siku ya Jumatatu Tarehe 18/04/2016 Diwani Wangu wa Kata ya Tulya Mhe Willison Kizanga "Kiteka" Akiongozana na Ujumbe Wake Kutoka Kiomboi Walifanya Mkutano Katika Ofisi ya Kijiji Cha Tulya Wakitueleza Kuwa:

a)Tufanye Harambee ya Kuchangia Madawati Katika Kata yetu na Kijiji

b)Harambee Hiyo Ni ya Pesa Na Itatolewa Kwa Hiyari

c)Ni Itazunguka Iramba Nzima Kukusanya Pesa Ili Kuongeza Wingi wa Madawati!

Nakupa Hongera Kwa Wazo Hili, Ila Ile 600M Imeenda Wapi?Hiari Hio Itakuwa Endelevu?Hivi Bajeti Ya Wizara ya Elimu Haipo?Mapato ya Halmashauri Hayapo Mpaka Mzigo Huu Wana Iramba Tuubebe?Na Je Pesa Zetu Zitakuwa Salama?Kama Tu Za Maabara Zililiwa?Hivi Tutapumulia Wapi Mwenge Ungali Njiani Kuja Na Itatubidi Tuuchangie?
 
Tsh 600Milioni x wabunge 300???? Siziamini hizi data, vinginevyo nchi hi haina sababu hata 2 ya kuomba masaada wala mkopo.
 
Kwanza Nakupa Pole ya Kufiwa na Baba Yako Mkubwa!
Pili,Siku ya Jumatatu Tarehe 18/04/2016 Diwani Wangu wa Kata ya Tulya Mhe Willison Kizanga "Kiteka" Akiongozana na Ujumbe Wake Kutoka Kiomboi Walifanya Mkutano Katika Ofisi ya Kijiji Cha Tulya Wakitueleza Kuwa:
a)Tufanye Harambee ya Kuchangia Madawati Katika Kata yetu na Kijiji
b)Harambee Hiyo Ni ya Pesa Na Itatolewa Kwa Hiyari
c)Ni Itazunguka Iramba Nzima Kukusanya Pesa Hili Kuongeza Wingi wa Madawati!
Nakupa Hongera Kwa Wazo Hili,Hila Ile 600 Mills Imeenda Wapi?Hiari Hio Itakuwa Endelevu?Hivi Bajeti Ya Wizara ya Elimu Haipo?Mapato ya Halmashauri Hayapo Mpaka Mzigo Huu Wana Iramba Tuubebe?Na Je Pesa Zetu Zitakuwa Salama?Kama Tu Za Maabara Zililiwa?Hivi Tutapumulia Wapi Mwenge Ungali Njiani Kuja Na Itatubidi Tuuchangie?
Mkuu,walisema kila mbunge atapewa 600milion au atapewa madawati 600 kupeleka jimboni kwake? Maana naona umejichanganya hapo.
 
Changieni, hakuna serikali. Kodi zenu zinafanya mambo mengine ya kutoa show kwenye TV
 
Ndio shida ya uongozi wa bunge kufanya kazi kwa kujipendekeza na unafiki kwa muhimili mwingine yaani serikali.
Wanataka kusema budget kwingine kote huwa haitoshi lakini bunge likapata ziada ya Bil6?
Hivi wabunge wapo serious kweli? Yani moja ya jambo walilotaka kufanya ni kwenda kuangalia nyumba ya balozi nje ya nchi!!!
 
Back
Top Bottom